Lionel Messi: 'Tulitaka kukaa Barcelona kuliko kitu chochote'

Messi aangua kilio akiaga klabu ya Barcrlona

Chanzo cha picha, Reuters

Muda wa kusoma: Dakika 3

Mshambuliaji nyota wa Argentina Lionel Messi hatimaye ametangaza rasmi kuondoka kwake klabu ya Barcelona baada ya kuichezea kwa takriban miaka 21.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Jumapili katika uwanja wa Nou Camp Messi aliyeshindwa kujizuia aliangua kilio wakati alipokuwa akiaga klabu hiyo.

"Familia yangu na mimi tuliamini kuwa tutakaa hapa nyumbani, ndivyo sote tulitaka zaidi ya kitu chochote.

"Tulifanya hapa kuwa nyumbani na tulifikiri tutaishi Barcelona.

"Wakati ambao nimekuwa nao hapa umekuwa mzuri usiokuwa na kifani lakini leo lazima nisema kwaheri. Nimekuwa hapa miaka mingi sana, maisha yangu yote tangu nilipokuwa na miaka 13. "

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Tayari Lionel Messi aliye n aumri wa miaka 34 na Paris St-Germain wamekubaliana mkataba wa miaka miwili.

"Ningelipendelea kushinda taji lingine la Ligi ya Mabingwa, naamini tungeliweza kushinda tena kwa maoni yangu '' aliendelea kusema.

Pia alizungumzia uhusiano wake na Barcelona akisema: "Nilijitolea kupunguza mshahara wangu kwa 50%, lakini hawakuniuliza kitu kingine chochote. Habari nilizoomba 30% zaidi ni uwongo, mambo mengi ambayo watu wanasema sio kweli."

Mamia ya mashabiki wa Barcelona walikusanyika nje ya Nou Camp wakati wa mkutano wa Lionel Messi na waandishi wa habari.

Kuondoka kwa Lionel Messi sio pigo tu kwa Barcelona, ​​pia ni pigo kwa La Liga, ambayo imepoteza mfungaji mabao wake hodari.

Gazeti la Ufaransa la L'Equipe linaripoti kuwa Messi atafanyiwa uchunguz wa kimatibabu mjini Paris Saint-Germain Jumapili usiku au Jumatatu asubuhi.

Messi akilia

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwanzo wa safari ya Messi

Alizaliwa na kukulia katikati mwa Argentina, Messi alihamia Uhispania na kujiunga na Barcelona akiwa na umri wa miaka 13, na kuichezea klabu hiyo kw mara ya kwanza Oktoba tarehe 17 mwaka wa 2004.

Alijiimarisha kama mchezaji muhimu wa klabu ndani ya miaka mitatu iliyofuata, na katika msimu wake wa kwanza bila kukatizwa mnamo 2008-09 aliisaidia Barcelona kufanikiwa kushinda mataji matatu ya soka nchini na akiwa na umri wa miaka 22, Messi alishinda tuzo yake ya kwanza ya Ballon d'Or.

Misimu mitatu ya mafanikio ilifuata, na Messi kushinda Ballons d'Or nne mfululizo, na kumfanya kuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo hiyo mara nne mfululizo. Wakati wa msimu wa 2011-12, aliweka rekodi za La Liga na Uropa kwa mabao mengi yaliyofungwa katika msimu mmoja, huku akijitambulisha kama mfungaji bora wa wakati wote wa Barcelona.

Lionel Messi

Chanzo cha picha, Getty Images

Misimu miwili iliyofuata, Messi alimaliza wa pili kwa tuzo ya Ballon d'Or nyuma ya Cristiano Ronaldo (mpinzani wake katika taaluma), kabla ya kupata hali yake bora kimchzo katika kampeni ya 2014-15, kuwa mfungaji bora wa muda wote La Liga na kuongoza Barcelona kushinda mataji matatu kwa mara ya pili , baada ya hapo alipewa tuzo ya tano ya Ballon d'Or mnamo 2015. Messi alishika unahodha wa Barcelona mnamo 2018, na mnamo 2019 alishinda tuzo ya sita ya Ballon d'Or.

Mafanikio ya hivi karibuni

Lionel Messi alimaliza kusubiri taji kuu la kwanza la kimataifa wakati Argentina ilipoifunga Brazil kwenye fainali ya Copa America kwenye uwanja wa Rio wa Maracana kwa bao moja kwa nunge tarehe 13 mwezi julai .

Messi, 34, alianguka chini kwa furaha wakati kipenga cha mwisho kilipopulizwa na alikimbiiwa kwa haraka na wachezaji wenzake, kabla ya kurushwa hewani kwa sherehe, kwani mwishowe alipata heshima ya kiwango cha juu na nchi yake katika mashindano ya 10 muhimu kwake .