Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Christian Eriksen kuwekewa kifaa maalumu cha moyo baada ya kuanguka uwanjani
Mchezaji wa kimataifa wa Denmark Christian Eriksen anatarajiwa kuwekewa kifaa maalumu cha moyo, kufuatia kuanguka kwake uwanjani wakati wa mchezo wa Euro 2020.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 alipata na mshtuko wa moyo na kudondoka uwanjani siku ya Jumamosi katika mchezo ambao Denmark ililala kwa bao 1-0 dhidi ya Finland huko Copenhagen on Saturday.
Daktari wa timu ya taifa ya Denmark, Morten Boesen, anasema kifaa hicho kinachojulikana kitaalamu kwa kifupi 'ICD', ni muhimu hasa wakati huu ambapo moyo wa mchezaji huyo una mipigo isio ya kawaida.
Mpaka sasa Eriksen yuko bado hosipyali akiendelea na tiba, ingawa mwenyewe anasema anaendelea vizuri kwa sasa.
Leo timu yake ya Denmark, inarejea uwanjani kucheza na Ubelgiji, ambapo Ubelgiji imesema itasimamiosha mchezo huo katika dakika ya 10, na kutumia dakika moja kupiga makofi kama sehemu ya kukumbuka na kumtakia heri Eriksen
Mlinzi wa Uhoplanzi, Daley Blind aliwahi kupata tatizo la moyo mwaka 2019 lakini alirejea uwanjani February 2020 baada ya kuwekewa kifaa hicho cha ICD. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 yuko na timu yake hiyo ya taifa kwenye Euro 2020 , ambapo alicheza kwenye mchezo wa kufungua dimba, Uholanzi ikiizaba Ukrain 3-2.
Hata hivyo mchezaji wa zamani wa Kriketi wa England, James Taylor, 31, alilazimika kukatisha maisha yake ya kriketi, baada ya kuwekewa kifaa hicho,kufuatia matatizo ya moyo aliyoyapata mwaka 2016