Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mohamed Elneny: Mwili wapatikana nyumbani kwa kiungo wa kati wa Arsenal nchini Misri
Mwili wa mtu umepatikana nyumbani kwa kiungo wa kati wa Arsenal Mohamed Elneny nchini Misri.
Babake Elneny, Nasser aliupata mwili huo wakati alipotembelea nyumba hiyo mjini Mahalla al-Kubra , ambayo iko takriban kilomita 100 kaskazini mwa Cairo.
Kisa hicho kiliripotiwa kwa polisi, ambaye wanasema mtu huyo alikuwa akijaribu kuiba nyaya za umeme.
Inaaminika kwamba alichomwa na umeme wakati wa wizi huo. Nyumba hiyo ni mali mpya ambayo ilitolewa na familia ya Elneny kutumika kama ofisi.
Elneny ambaye amerudi Arsenal baada ya kuichezea Misri katika kombe la mataifa ya Afcon , aliambiwa kuhusu kisa hicho kupitia simu.