Premier League: Liverpool yaongoza mbele ya mabingwa Man City

Wachezaji wa Liverpool na Manchester City

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Liverpool ilikaribia kushinda ligi ya Uingereza tangu 1990

Liverpool ilijipatia zaidi ya takriban £152m kutoka kwa ligi ya Uingereza msimu huu ikiwa ni £1.44m zaidi ya mabingwa Manchester City, baada ya kushiriki katika mechi nyingi za moja kwa moja katika mechi zilizopeperushwaa na runinga Uingereza

The Reds, ambao walimaliza wa pili katika jedwali la Uingereza wakiwa na jumla ya pointi 97 walionyeshwa wakicheza moja kwa moja mara 29 katika Sky Sports ama BT Sport ikiwa ni mara tatau zaidi ya Man City.

Kikosi hicho cha Pep Guardiola kilipokea £38.4m kwa kumaliza juu ikiwa ni zaidi ya takriban £2m zilizopokewa na kikosi cha Jurgen Klopp.

Klabu ya Huddersfield ambayo ilishushwa daraja ilipokea £96.6m baada ya kumaliza wa mwisho.

Klabu zote ishirini zilipokea mapato sawa ya £34.4m, pamoja na £43.2m kutoka kwa runinga za kimataifa kila moja na £5m za mauzo