Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 28.04.2019: Pogba, De Gea, Van Dijk, Maguire, Bale, Hazard

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati Manchester United Paul Pogba,26, ameidokezea klabu hiyo mpango wake wa kujiunga na Real Madrid msimu ujao.
Tayari Pogba amekubali masharti ya mkataba wakujiunga miamba hao wa soka wa Uhispania. (AS - in Spanish)
Juventus wanataka kumregesha Pogba,Turin lakini watalazimika kuwauza wachezaji watatu muhimu ili wawaeze kumnunua mchezaji huyo wa Manchester United raia wa Ufaransa kwa kima cha pauni milioni 130.(Guadian)
Mabingwa hao wa Italia pia huenda wakajaribu kuipiku Paris St-Germain katika kinyang'anyiro cha usajili wa kipa wa United,28, David de Gea. (Le10 Sport in French)

Chanzo cha picha, Getty Images
Klabu ya Lyon inayoshiriki Ligue 1 ya Ufaransa imewasiliana na kocha wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger kuhusu uwezekano wa yeye kushikilia usukani kutoka kwa Bruno Genesio ambaye anaondoka klabu hiyo mwisho wa msimu huu.(L'Equipe-in French)
Kocha wa Real Madrid Zinadine Zidane anasema Gareth Bale na mchezaji nyota wa Chelsea Eden Hazard ambaye amehusishwa na tetesi za kuhamia uwanja wa Bernabeu,watashirikiana vizuri wakiwa katika timu moja.( Marca)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Napoli Carlo Ancelotti amesema hatamzuia beki wake wa kati Kalidou Koulibaly,27, kujiunga na Manchester United,huku mshambuliaji Lorenzo Insigne,27, nae akihusishwa na uhamisho wa Chelsea na Liverpool msimu huu wa joto.(Mail)
Kiungo wakati wa Real Madrid Brahim Diaz,19, ambaye alijiunga na Manchester City mwezi Januari mwaka huu atatolewa kwa mkopo msimu ujao.(Marca)

Chanzo cha picha, Getty Images
Klabu ya DC United inayoshiriki ligi ya MSL inatapania kumsajili bei wa nyuma wa Wales Ashley Williams ambaye yuko Stoke kwa mkopo kutoka Everton. Huddersfield na Aston Villa pia zinamyatia kiungo huyo wa miaka 34. (Sun)
Bunley na Wolves wanapania kuweka dau la kumnunua beki wa kati wa Hamilton Academical Jamie Hamilton ambaye ni nahodha wa timu ya Uskochi ya wachezaji wa chini ya miaka 17(Mail)
Kocha wa Crystal Palace Roy Hodson anasema kuwa hana ufahamu atapewa kiasi gani cha fedha kwa ajili ya uhamisho wa wachezaji msimu huu wa joto. (Evening Standard)

Chanzo cha picha, Reuters
PSG imeipatia Juventus ofa ya euro milioni 70 kumunua kiungo wa kati Miralem Pjanic, 29 , lakini miamba hao wa Ligi ya serie A wanataka euro milioni 100. (Corriere dello Sport-in Italian)
Tetesi Bora Jumamosi
Paul Pogba amekataa kukamilisha taratibu za visa ya klabu ya Manchester United kabla ya timu hiyo kwenda kwa matembezi Barani Asia, huku Real Madrid wakisema wanaimani kuwa watasaini mkataba na Mfaransa huyo anayecheza katika safu ya kati mwishoni mwa msimu huu . (Sun)

Chanzo cha picha, Reuters
Juventus wanamfuatilia kwa karibu mlizi wa timu ya Tottenham Mbelgiji Toby Alderweireld, mweney umri wa miaka 30, ambaye ana weza kutoka kwenye kikosi hicho iwapo atalipa £25m. (Calciomercato)
Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers anajiandaa kuvunja rekodi ya Foxe t kwa dau la £40m ili kumuingiza klabuni kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans mwenye umri wa miaka 21ambaye ana mkataba wa kudumu kutoka Monaco. (Mirror)














