Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Sancho, Hazard, Mourinho, Bale, Karius, Courtois
Manchester United inatarajiwa kumsajili winga wa Borussia Dortmund muingereza Jadon Sancho.
Klabu hiyo ya ligi ya primia pia imewasiliana na Barcelona kuhusiana na uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho, 28. (Independent)
Huku hayo yakijiri meneja wa muda wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer anajiandaa kuwapatia walinzi wake nafasi ya kujidhihirisha kuwa wanaweza kufikia matarajio yake kabla ya uamuzi kutolewa wa kumnunua beki wa kati kwa kima cha £80m msimu huu wa joto. (Sun)
Chelsea inahofia kuwa haina uwezo wa kumzuia mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard kuhamia Real Madrid.
The Blues wanatarajiwa kumuuza nyota huyo wa miaka 28 kwa angalau £100m. (ESPN)
Mchezaji mwenzake Emerson amekiri kuwa wachezaji wote wa Chelsea "wanahofia" kumpoteza Hazard msimu huu wa joto, lakini anaamini huenda akabadili msimamo.(Sky Sport)
Kipa wa Liverpool Loris Karius ataendelea kuichezea Besiktas kwa mkopo licha ya ya kocha wa klabu hiyo kusema "hajaridhishwa" na utendakazi wa mchezaji huyo wa miaka 25. (ESPN)
Karius huenda akaishitaki Besiktas kwa kutomlipa marupurupu yake baada ya kuenda miezi minne bila mshahara. (Goal)
Crystal Palace na Brighton ni miongoni mwa vilabu vinavyopania kumsajili kiungo wa kati wa Newcastle mfaransa Mo Diame 31. (Star)
Walinzi Sergio Ramos wa Uhipania na Karim Benzema wa Ufaransa walidhani kuwa Jose Mourinho angeliteuliwa kuwa meneja wa Real Madrid.
Zinedine Zidane hata hivyo alipewa nafasi hiyo siku ya Jumatatu miezi 10 baada ya kuondoka klabu hiyo. (Sport)
Bayern Munich itafanya mazungumzo na mshambuliaji wa Poland,Robert Lewandowski kuhushiana na kurefushwa kwa mkataba wake.
Kiungo huyo wa miaka 30 amehusishwa na tetesi kuwa huenda akajiunga na Real Madrid. (Goal)
Kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice anatarajia kujiunga na timu ya taifa ya England katika mechi za kufuzu kwa kombe Euro mwaka 2020 dhidi ya Czech Republic na Montenegro. (Guardian)
Baba yake kipa wa Real Madrid goalkeeper Thibaut Courtois amevishutumu vyombo vya habari vya Uhispania na Ubelgiji kwa kumnyanyasa mwanawe. (Independent)
Arsenal wameingia katika kinyan'ganyiro cha kumsaini beki wa kushoto wa Ajax Nicolas Tagliafico.
Gunners wamejiunga na Real Madrid, Atletico Madrid, Manchester United na Liverpool katika harakati ya kupata saini ya nyota huyo wa miaka 26. (Footy Cosmos)
Tetesi Bora Jumanne
Zinedine Zidane amerejea tena Real Madrid miezi kumi baada ya kuondoka klabu hiyo.
Miamba hao wa soka wanapania kuwasajili wachezaji kadhaa ikiwa ni pamoja na mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 28, na kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 27. (Independent)
Zinedine Zidane aliichezea Real Madrid kati ya mwaka 2001 na 2006 na baadae akaiongoza klabu hiyo kuanzia mwaka 2016 hadi 2018.
Gareth Bale, 29, na Luka Modric, 33, ni miongoni mwa wachezaji wanaojiandaa kuondoka uwanjwa wa Bernabeu msimu huu wa joto. (Independent)
Meneja wa England Gareth Southgate anatafakari uwezekano wa kumrudisha kikosini kiungo wa kati wa Southampton James Ward-Prowse, 24 baada ya mchezaji huyo kuimarika.
Southgate, Jumatano hii anatarajiwa kutangaza kikosi chake kitakachoshiriki michuano ya kufuzu kwa kombe la Euro mwaka 2020 dhidi ya Czech Republic na Montenegro. (Mirror)