Mchezaji raga mpenzi wa jinsia Kenneth Macharia ahofia unyanyasaji akirudishwa Kenya

Kenneth Macharia, member of Bristol Bisons RFC

Chanzo cha picha, Phillip Rogerson

Maelezo ya picha, Kenneth Macharia anasema atakabiliwa na unyanyasaji akilazimishwa kurudi nyumbani Kenya.
Muda wa kusoma: Dakika 2

Mchezaji raga ambaye ni mpenzi wa jinsia moja, aliyekataliwa ombi la kupata hifadhi Uingereza, anasema atakabiliwa na unyanyasaji akilazimishwa kurudi nyumbani Kenya.

Mchezaji wa timu ya Bristol Bisons Kenneth Macharia anazuiwa ukisubiriwa uamuzi wa iwapo atarudishwa Kenya.

Timu hiyo ya wapenzi wa jinsia moja imeeleza kwamba Macharia anahofia " kukandamizwa na kukabiliwa na ghasia Kenya kwasababu ya kuwa mpenzi wa jinsia moja".

Katika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter, wachezaji wenzake wamesema yeye ni "kiungo muhimu" wa kundi lao.

"Uwajibikaji wake kwa maadili ya mchezo wa raga ni wa kupigiwa upatu. Tupo katika hatari ya kupoteza mojawapo ya wachezaji wa timu inayoshirikisha wapenzi wa jinsia moja," imesema taarifa ya timu hiyo.

Thangam Debbonaire, mbunge wa Macharia anakoishi Uingereza, pia ameahidi kutoa usaidizi wake.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Macharia aliwasiliana na wachezaji wenzake kwa njia ya ujumbe mfupi kuwaomba usaidizi siku ya Ijumaa.

Tangu hapo amezuiwa katika kituo cha uhamiaji cha Colnbrook karibu na uwanja wa ndege wa Heathrow.

BBC imewasiliana na wizara ya mambo ya ndani kupata tamko.

Meneja wa Bristol Bisons Lee Penfold, amesema Macharia amekuwa na "timu hiyo kwa muda mrefu" na iwapo atarudishwa nyumbani Kenya huenda 'akakabiliwa bila ya shaka na ukandamizaji'.

"Hakuna anayestahili kuyapitia haya," Penfold ameongeza.

Miaka gerezani

Mapenzi ya jinsia moja ni kinyume na sheria Kenya na mtu anaweza kuadhibiwa kwa hadi miaka 14 gerezani.

Mnamo 2016, shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu limegundua kwamba wapenzi wengi wa jinsia moja wanaoishi nchini Kenya wanakabiliwa na 'wasiwasi wa usalama kila siku'.

Gay rights protesters outside Commonwealth House on 19 April 2018.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Huenda Kenneth Macharia akakbiliwa na kifungo cha hadi miaka 14 Kenya kwa kuwa mpenzi wa jinsia moja.

Macharia pia ni mfuasi wa kundi la wapenzi wa jinsia moja kwa jina Kiki, linalowaunga mkono wapenzi wa jinsia moja ambao pia ni wa asili ya Kiafrika na wa makundi ya makabila ya wachache.

Katika taarifa, kundi hilo linasema "limesikitishwa kusikia kuhusu uamuzi unaotarajiwa kuhusu kurudishwa nyumbani kwa Kenneth".

"Uamuzi wa wizara ya mambo ya ndani kumrudisha kutamueka bwana Macharia katika hatari ya kukandamizwa na kushambuliwa" kundi hilo limesema.