Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 02.10.2018: Mbappe, Pogba, Mourinho, Ramsey, Sanchez, Diop
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ameka nushataarifa kwamba anataka kumnunua mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 19. (Independent)
Bodi ya Barcelona imagawanyika kuhusu ikiwa itamwendea kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 25 mwezi Januari lakini mabingwa hao wa Uhispania wanaamini wana uwezo wa kifedha wa kutosha kuweza kumsaini Mfaransa huyo mshindi wa Kombe la Dunia. (ESPN)
Real Madrid wamejiunga katika kundi la klabu zinazomzea mate mchezaji wa kimataifa wa Wales Aaron Ramsey, 27, ambaye atondoka Arsenal mwezi January. (Teamtalk)
Arsenal ni kati ya vilabu vinavyommezea mate mchezaji wa Lille, Nicolas Pepe, 23.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye thamani ya pauni milioni 30 amepokelewa vizuri chini Ufaransa kwa mchezo wake mzuri msimu huu baada ya kufunga mabao matano katika mechi nane.
Chelsea wako katika nafasi nzuri ya kumsaini mchezaji mwenye miaka 15 wa Volendam Mholanzi Sam Lautenschutz. (The Sun)
Wolves wanamwinda mlinzi wa Aberdeen raia wa Scotland Scott McKenna. Ofa za Celtic na Aston Villa zimekataliwa kwa mchezaji huyo mwemye miaka 21. (Scottish Sun)
Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United Lee Sharpe anaamini meneja wa klabu Jose Mourinho anastahilia kufutwa ikiwa matokeo yao mabaya yataendelea kwa mechi zao mbili wiki hii. (Talksport)
Meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane anariptiwa kumpigia simu Mourinho kumhakikishia kuwa hakuna mipango ya kuchukua mahala pake. (Mirror)
Mourinho anaaminiwa kutengwa huko Old Trafford baada ya kutofautiana na nahodha wa timu Antonio Valencia. (Mail)
Mshambuliaji wa United Alexis Sanchez, 29, alibaki akiteta baada kuachwa nje ya mechi na Mourinho kwa mechi wa wikendi na West Ham. (Mirror)
Mchezaji anayetafutwa na United Sergej Milinkovic-Savic ameongeza mkataba wake na Lazio hadi mwaka 2023. Mchezaji huyo mwenye miaka 23 raia wa Serbia alihusishwa na kuhamia Old Trafford majira ya joto. (Mail)
West Ham wamewashinda Manchester United, Barcelona, Arsenal, Tottenham na Everton katika kumsaini mlinzi huyo mwenye miaka 21 Issa Diop msimu huu. (Mail)
Kiungo wa kati wa England Danny Drinkwater, 28, hana haraka ya kuondoka Chelsea licha ya kutokuwa kwenye kikosi cha meneja Maurizio Sarri. (Telegraph)
Bora zaidi kutoka Jumatatu
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ana hofu kuhusu hatma yake huko Old Trafford na anaamini kuwa maafisa wa klabu wamewasiliana na meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane. (Sun)
Lakini mchezaji huyo wa zamani kimataifa wa Ufaransa analenga kuwa meneja mpya wa Juventus. (Tuttosport, via Daily Express)
Sintofahamu kuhusu hatma ya Mourinho huko United inamaanisha kuwa wachezaji 12 hawana uhakika kuhusu hatma yao wakati wanaingia mwaka wa mwesho wa mikataba yao. (Daily Mirror)
Mourinho amekosa uvumilivu kwa mshambuliaji raia wa Chile Alexis Sanchez, 29. (London Evening Standard)
Mlinzi wa Manchester United raia wa England Luke Shaw, 23, anasema kikosi kilicheza vibaya wakati kilishindwa na West Ham siku ya Jumamosi. (Daily Telegraph)
Manchester City watangoja kabla ya kumpa ofa mpya kiungo wa kati mwenye miaka 18 Phil Foden ya mkataba mpya wa miaka mitano wa pauni 250,000 kwa wiki. (Daily Star)
Meneja wa City Pep Guardiola amemuonya wing'a mjerumani Leroy Sane, 22, akitaka asipoteze mwelekeo. (Sun)
Maajenti wa Manchester City, Liverpool na Tottenham walimtazama kiungo wa kati wa Lazio raia wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 23, wakati wa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Genoa. (Daily Mirror)