Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Muethiopia Ayana atwaa dhahabu na rekodi Rio
Raia wa Ethiopia Almaz Ayana ameishindia Afrika dhahabu ya kwanza Michezo ya Olimpiki mjini Rio na kuvunja rekodi ya dunia mbio za mita 10000 wanawake.
Ayana aliwaacha nyuma wapinzani wake mbio zikiwa katikati na kuendelea hadi mwisho, muda wake ukiwa dakika 29 sekunde 17.45.
Rekodi ya awali iliwa 29:31.78 na iliwekwa na Mchina Wang Junxia mwaka 1993. Mkenya Vivian Cheruiyot ameshinda fedha naye raia mwingine wa Ethiopia Tirunesh Dibaba akachukua shaba.