Uchaguzi wa Malawi kwa picha

Wapigaji kura waliochoka kusubiri kwenye foleni waliamua kuteketeza karatasi na sanduku za kupigia kura

Uchaguzi wa Malawi umefanyika leo Jumanne ukisemekana kuwa wenye ushindani mkali
Maelezo ya picha, Uchaguzi wa Malawi umefanyika leo Jumanne ukisemekana kuwa wenye ushindani mkali
Rais aliye mamlakani Joyce Banda na wagombea wengine sita ndio wanawania kutawala nchi hiyo.
Maelezo ya picha, Rais aliye mamlakani Joyce Banda na wagombea wengine sita ndio wanawania kutawala nchi hiyo.
Mpigaji kura huyu alikuwa kwenye foleni asubuhi na mapema kumchagua mgombea wake
Maelezo ya picha, Mpigaji kura huyu alikuwa kwenye foleni asubuhi na mapema kumchagua mgombea wake
Foleni ndefu zilishuhudiwa katika maeneo mengi ya nchi huku ushindani katika uchaguzi huo ukisemekana kuwa mkali
Maelezo ya picha, Foleni ndefu zilishuhudiwa katika maeneo mengi ya nchi huku ushindani katika uchaguzi huo ukisemekana kuwa mkali
Katika baadhi ya maeneo shughuli ya upigaji kura ilianza kwa kuchelewa
Maelezo ya picha, Katika baadhi ya maeneo shughuli ya upigaji kura ilianza kwa kuchelewa
Hali hiyo ilisababisha baadhi ya wapiga kura kuwa na hasira na hata kusababisha vurugu
Maelezo ya picha, Hali hiyo ilisababisha baadhi ya wapiga kura kuwa na hasira na hata kusababisha vurugu
Wasimamizi wa uchaguzi katika vituo vinne mjini Blantyre wameshambuliwa na watu wenye hasira baada ya kukaa muda mrefu kwenye mistari bila kuanza kupiga kura
Maelezo ya picha, Wasimamizi wa uchaguzi katika vituo vinne mjini Blantyre wameshambuliwa na watu wenye hasira baada ya kukaa muda mrefu kwenye mistari bila kuanza kupiga kura
Katika eneo la Nkolokoti watu wamevunjavunja masanduku ya kupigia kura, kompyuta, printer na hata mashine za kuzalishia umeme (Sola Panels)
Maelezo ya picha, Katika eneo la Nkolokoti watu wamevunjavunja masanduku ya kupigia kura, kompyuta, printer na hata mashine za kuzalishia umeme (Sola Panels)
Wakati hali ikiwa namna hiyo huko Blantyre, maeneo mengine ya nchi shughuli ya upigaji kura imeendelea vizuri japokuwa vituo vingi vilichelewa kuanza kupiga kura.
Maelezo ya picha, Wakati hali ikiwa namna hiyo huko Blantyre, maeneo mengine ya nchi shughuli ya upigaji kura imeendelea vizuri japokuwa vituo vingi vilichelewa kuanza kupiga kura.