Wanajeshi wa Israel waliojifanya kuwa madaktari wavamia hospitali na kuwaua wanamgambo 3
Wanajeshi wa Israel wamewauwa wanamgambo watatu ndani ya hospitali ya Jenin, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.
Moja kwa moja
Asha Juma and Abdalla Seif Dzungu
Kwa picha: Mazishi ya Wapalestina 3 waliouawa kwa kupigwa risasi na jeshi la Israel huko Jenin
Chanzo cha picha, Getty Images
Duru za kimatibabu za Palestina zimesema kuwa kikosi maalumu cha Israel kimewaua Wapalestina watatu asubuhi ya leo ndani ya hospitali ya Ibn Sina katika mji wa Jenin.
Habari zilieleza kuwa vijana hao watatu waliuawa baada ya kikosi hicho maalum kuvamia orofa ya tatu ya hospitali hiyo wakiwa wamevalia kiraia na kutumia silaha zilizokuwa na vifaa vya kuzuia sauti.
Vijana hao watatu ni ndugu wawili Muhammad na Basil Al-Ghazawi na Muhammad Jalamna.
Jeshi la Israel lilithibitisha kuwa vijana hao watatu ni wa "seli ya kigaidi" yenye uhusiano na Hamas, na operesheni hii ni ya kwanza ya aina yake nchini humo.
Chanzo cha picha, Getty Images
Chanzo cha picha, Getty Images
Chanzo cha picha, Getty Images
Waziri wa Ulinzi wa Israel: Jeshi litahamia mpakani na Lebanon hivi karibuni
Chanzo cha picha, Reuters
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Galant alisema jana usiku kwamba jeshi la Israel "litaanza hivi karibuni" harakati kwenye mpaka wa kaskazini na Lebanon.
Gallant aliwafahamisha wanajeshi walioko karibu na mpaka na Gaza kwamba wangeondoka eneo hilo na kuelekea kaskazini, na akasema kwamba askari wa akiba wataondolewa hatua kwa hatua "kujiandaa kwa operesheni zijazo.
"Hapo jana, Hezbollah ilitangaza kulenga maeneo 12 ya Israel, na pia kuwaomboleza wanachama wake wawili.
Mpaka kati ya Lebanon na Israel unashuhudia mashambulizi ya mabomu kati ya jeshi la Israel na Hezbollah.
Inafaa kukumbukwa kuwa jeshi la Israel lilitangaza mapema kwamba litafanya mazoezi ya kijeshi kwenye mpaka na Lebanon ili kuongeza utayari wake, kwa kuzingatia hali ya wasiwasi inayoendelea na hivi karibuni Hezbollah kuongeza kasi ya mashambulizi yake.
Polisi wa Uingereza wamemkamata mtu aliyehusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda
Mwanamume mmoja amekamatwa huko Gateshead na polisi wanaochunguza mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu yaliyotokea miaka 30 iliyopita nchini Rwanda.
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 69 alihojiwa kuhusu mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo watu 800,000 waliuawa.
Wataalamu kutoka Timu ya Kukabiliana na Uhalifu wa Kivita wa Kupambana na Ugaidi walifanya kazi na Polisi wa Kukabiliana na Ugaidi Kaskazini Mashariki ili kukamata watu hao Alhamisi iliyopita.
Maafisa walisema kuwa mwanamume huyo ameachiliwa kwa dhamana huku uchunguzi ukiendelea.
Timu ya Uhalifu wa Kivita ni kitengo cha kitaifa kinachoendeshwa ndani ya afisi Kupambana na Ugaidi ya Polisi wa mijini.
Kamanda Dominic Murphy alisema uchunguzi huo unafuatia "tuhuma za makosa makubwa zaidi unaweza kufikiria" na yeyote aliyefanya ukatili huo "atakabiliwa na haki popote alipo duniani".
Aliongeza: “Kukusanya ushahidi wa kuunga mkono uwezekano wa kufunguliwa mashitaka siku za usoni ni mchakato mgumu unaohitaji bidii na usahihi.
"Wakati kukamatwa ni hatua muhimu katika uchunguzi wowote, maafisa wataendelea kufanya kazi ili kuendeleza uchunguzi huu."
Uchunguzi huo hauhusiani na uchunguzi unaoendelea wa uhalifu wa kivita ambao ulizinduliwa mnamo 2018, ukiangazia watu wengine watano wa Uingereza.Kati ya Aprili na Juni 1994, inakadiriwa kuwa Wanyarwanda 800,000 waliuawa katika muda wa siku 100.
Habari za hivi punde, Video: Tazama jinsi Wanajeshi wa Israel waliojifanya kuwa madaktari walivyovamia hospitali na kuwaua wanamgambo 3
Maelezo ya video, Wanajeshi wa Israel waliojifanya kuwa madaktari wavamia hospitali ukingo wa magharibi
Wanajeshi wa Israel wamewauwa wanamgambo watatu ndani ya hospitali ya Jenin, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.
Kanda za CCTV zilionyesha washiriki wa kitengo cha siri wakiwa wamejigeuza kama matabibu na raia wengine wakipita kwenye korido wakiwa na bunduki zilizoinuliwa.
Jeshi la Israel lilisema wanamgambo hao walikuwa wamejificha katika hospitali hiyo, na kwamba mmoja alikuwa karibu kutekeleza shambulio hilo.
Wizara ya afya ya Mamlaka ya Palestina iliishutumu Israel kwa kutekeleza "mauaji mapya ndani ya hospitali".
Hamas, kundi la Wapalestina wenye silaha ambalo linapigana vita na Israel huko Gaza vilivyochochewa na mashambulizi yake dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba, lilisema kuwa jeshi la Israel "limewaua wapiganaji watatu", akiwemo mmoja wa wanachama wake.
Angola yakanusha kuhusika na meli iliyoshambuliwa na wapiganaji wa Houthi
Chanzo cha picha, Jeshi la Wanamaji la India
Maelezo ya picha, Meli hiyo iliteketea kwa saa kadhaa Ijumaa iliyopita katika Ghuba ya Aden
Kampuni ya
mafuta inayomilikiwa na serikali ya Angola ya Sonangol imepuuza ripoti kwamba
meli iliyolengwa na wapiganaji wa Houthi wiki iliyopita katika Ghuba ya Aden
ilikuwa sehemu ya meli zake.
Meli hiyo
yenye uhusiano na Uingereza iliwaka moto kwa saa kadhaa Ijumaa iliyopita
katika Ghuba ya Aden baada ya kushambuliwa kwa kombora lililorushwa na Wahouthi.
Kundi hilo lenye
kuungwa mkono na Iran ambalo makao yake yako Yemen, limesema lililenga meli
hiyo kwa jina Marlin Luanda kama hatua ya kujibu "uchokozi wa Marekani na
Uingereza".
Taarifa ya
kukana kuwa na uhusiano nayo imewadia baada ya vyombo vya habari vya Angola
kuhusisha meli hiyo na Sonangol.
"Sonangol
inaarifu umma kwamba meli ya Marlin Luanda, iliyoshambuliwa hivi majuzi na
kombora katika Bahari ya Shamu, si sehemu ya meli zinazomilikiwa na kampuni au
za kukodi," kampuni hiyo ilisema katika taarifa iliyoonekana na vyombo vya
habari vya ndani.
Marlin
Luanda, inayoendeshwa kwa niaba ya mfanyabiashara wa bidhaa mwenye makao yake
Singapore Trafigura, inapeperusha bendera ya Visiwa vya Marshall.
Trafigura ni mmoja wa wasambazaji wakuu wa dizeli na
dizeli ya baharini nchini Angola.
Pia ni mbia katika kampuni ya Puma Energy, ambayo
inadhibiti vituo vya mafuta vya Pumangol nchini Angola.
Wanahisa wengine katika kampuni ya Puma Energy ni pamoja
na Sonangol.
Tazama Video: Afisa wa trafiki anasurika kifo kimiujiza baada ya gari alilolisimamisha kugongwa
Contains some violence.
Maelezo ya video, Video: Tazama jinsi afisa huyu wa trafiki ilivyonusurika kifo
Video ya Dashcam iliyotolewa na Polisi wa barabara kuu ya Oklahoma nchini Marekani inaonyesha mmoja wa maafisa wake akinusurika kifo baada ya gari alilolisimamisha kugongwa
Katika video hiyo, askari Gregory anaonekana akizungumza na dereva wa gari lililoegeshwa wakati gari lingine linapowagonga, na kumpelekea afisa huyo kuruka.
"Natumai hii ni hofu yangu ya kazi," Gregory alisema.
Hakuna aliyepata majeraha mabaya.
Katika chapisho kwenye Facebook, Doria ya Barabara Kuu ya Oklahoma ilionya dhidi ya "uendeshaji mbaya" na kuwataka madereva kupunguza mwendo na kusogea ikiwa watasimamishwa na trafiki.
CHADEMA: Maoni yetu yamepuuzwa
Katibu wa chama kikuu
cha upinzani Tanzania Chadema, John Mnyika amesema kuwa
maoni yao na ya wadau juu ya kushughulikia miswada ya uchaguzi nchini Tanzania
yamepuuzwa.
Moja ya agenda ya
maandamano yaliyofanywa na chama hiko siku chache zilizopita ni kushinikiza
miswada hiyo kuondolewa bungeni.
Kupitia ujumbe alioweka
katika mtandao wa X, Mnyika ameelezea ratiba iliyowekwa kwenye tovuti ya Bunge,
akisema kuwa ‘’miswada mibovu ya uchaguzi na vyama itajadiliwa kuanzia leo mpaka
tarehe 2 Februari 2024’’.
‘’Inakwenda kupitishwa
bila kuanza na mabadiliko au marekebisho ya katiba’’ Mnyika alisema.
Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe wiki iliyopita alisema maandamano hayo yalilenga kuishinikiza serikali
kuzingatia maoni na mapendekezo ya wadau mbalimbali kuhusu masuala ya uchaguzi.
Vilevile chama hicho
kiliitaka serikali iondoe Bungeni miswaada inayohusu vyama vya siasa na
uchaguzi, ambayo ni muswada wa Marekebisho ya Sheria za Vyama vya siasa na
Sheria ya gharama za Uchaguzi.
Badala yake, Chadema
iliitaka serikali iwasilishe muswada wa kukwamua mchakato wa Katiba mpya kwa
kuzingatia mwafaka wa kitaifa.
Kadhalika, Chadema
iliitaka serikali iwasilishe bungeni muswada wa kufanya marekebisho ya mpito ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ili uchaguzi wa
serikali za mitaa wa 2024 na ule mkuu wa 2025 uwe huru na haki.
Katika taarifa ya Bunge
la Tanzania, mkutano huo umeongezewa wiki moja ya ziada ili kujadili kwa uzito
miswada hiyo.
‘’Mkutano huu
umeongezewa wiki moja kutokana na uzito wa majukumu yaliyopangwa ikiwemo
uzito wa Miswada itakayoshughulikiwa”
Habari za hivi punde, Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan afungwa jela kwa kuvujisha siri za serikali
Chanzo cha picha, EPA
Aliyekuwa
waziri mkuu wa Pakistan Imran Khan amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela katika
kesi ambayo alishtakiwa kwa uvujaji wa siri za serikali.
Bw Khan,
ambaye alitimuliwa na wapinzani wake kama Waziri Mkuu mnamo 2022, tayari
anatumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya
ufisadi.
Ametaja
mashtaka yote dhidi yake kuwa ya kisiasa.
Hukumu chini
ya sheria ya siri inawadia wiki moja kabla ya uchaguzi mkuu ambapo amezuiwa
kugombea.
Waziri wa
zamani wa mambo ya nje Shah Mahmood Qureshi - makamu mwenyekiti wa chama cha Bw
Khan cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) - pia alihukumiwa kifungo cha miaka 10
jela na mahakama maalum.
Kinachojulikana
kama kesi ya siri inahusu madai ya uvujaji wa barua za siri za kidiplomasia
zilizotumwa na balozi wa Pakistan mjini Washington kwenda Islamabad wakati Bw
Khan alipokuwa waziri mkuu.
Inahusiana
na kuonekana kwake katika mkutano wa Machi 2022, mwezi mmoja kabla ya mchezaji
huyo wa zamani wa kriketi kuondolewa mamlakani kwa kura ya kutokuwa na imani
naye. Imran Khan alionekana jukwaani, akipunga karatasi ambayo anasema
ilionyesha njama za kigeni dhidi yake.
Alisema
ilieleza kwa kina kwamba "wote watasamehewa ikiwa Imran Khan ataondolewa
madarakani". Hakutaja nchi hiyo - lakini aliikosoa sana Marekani.
Upande wa
mashtaka ulisema kwamba hatua za Bw Khan ni sawa na kuvujisha waraka wa siri na
kuharibu uhusiano wa kidiplomasia.
Shtaka la
mwisho linaweza kusababisha kifungo cha maisha au hata adhabu ya kifo.
Kesi hiyo
imesikilizwa kwa muda wa miezi michache iliyopita ndani ya mahakama maalum
iliyoundwa ndani ya jela ambayo Bw Khan amekuwa akishikiliwa tangu
Agosti. Vyombo vya habari vya kimataifa havikuruhusiwa kuhudhuria.
Vyombo vya
habari vya eneo viliripoti kwamba hakimu aliambiwa hivi majuzi kuharakisha kesi
hiyo.
Chama cha Bw
Khan cha PTI kilisema kitapinga uamuzi wa mahakama na kuuita dhihaka.
Uchaguzi
mkuu utafanyika tarehe 8 Februari, huku kukiwa na madai kuwa PTI inazuiwa na
mamlaka kufanya kampeni. Bw Khan anapambana na kesi nyingine nyingi za
kisheria.
Zimbabwe yaanzisha kampeni ya chanjo ya nyumba hadi nyumba ya kipindupindu
Chanzo cha picha, WHO Zimbabwe/X
Zimbambwe
imeanzisha kampeni ya chanjo ya ugonjwa wa kipindupindi wakilenga zaidi ya watu
milioni mbili dhidi ya ugonjwa huo unaoenezwa kupitia maji.
Mlipuko wa
sasa ambao ulianza mapema mwaka jana umehusishwa na zaidi ya vifo 400 huku
zaidi ya watu 21,000 wakisemekana kuambukizwa. Takriban nusu ya idadi hiyo
ilihusisha watoto.
Kampeni ya
chanjo inafanywa nyumba hadi nyumba kwa ushirikiano na mashirika ya Umoja wa
Mataifa na inalenga raia kuanzia umri wa mwaka mmoja na zaidi.
Maafisa wa
Afya wanatoa kipaumbele kwa wilaya 26 zinazochukuliwa kuwa kitovu cha ugonjwa
huo.
Mlipuko huo
umesababisha zaidi ya maambukizi 188,000 na zaidi ya vifo 3,000, hasa Zimbabwe,
Msumbiji na Zambia, Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kibinadamu, Ocha,
linasema.
Ecowas: Nigeria yazikosoa nchi zilizojiondoa kutoka jumuiya ya kikanda
Chanzo cha picha, AFP
Nigeria
imezishutumu Mali, Burkina Faso na Niger kwa kuwakatisha tamaa watu wao baada
ya kujiondoa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (Ecowas).
Ni maoni ya
kwanza kutoka kwa mwenyekiti wa bodi ya kiuchumi na kisiasa tangu serikali tatu
kutangaza uamuzi wao wa kuondoka kwenye Jumuiya hiyo siku ya Jumapili.
Nchi hizo tatu
tayari zilikuwa zimesimamishwa kuendesha shughuli zake kwa Ecowas baada ya
mapinduzi ya hivi majuzi.
Watawala wao wa kijeshi wamejitenga na ukoloni wa zamani
wa Ufaransa na kuimarisha uhusiano na Urusi.
Wakisema kwamba walitaka kurejesha usalama kabla ya
kuandaa uchaguzi, waliunda makubaliano ya ulinzi wa pande zote mnamo Septemba
yaliyoitwa Muungano wa Nchi za Sahel.
Wanaishutumu Ecowas kwa kushawishiwa na mataifa ya nje na
kushindwa kuwasaidia kukabiliana na ghasia za wanajihadi katika nchi zao.
Ripoti
kutoka Niger siku ya Jumatatu zilisema watu 22 wameuawa katika shambulio
linaloshukiwa kuwa la wanajihadi kwenye kijiji karibu na mpaka na Mali.
Afisa wa
eneo hilo alisema watu walikuwa wamewasili Motagatta katika eneo la Tillaberi
kwa pikipiki na kuanza kuwafyatulia risasi raia.
Kujiondoa
kwao kutakuwa na madhara makubwa ikizingatiwa kwamba jumuiya inahakikisha
usafiri bila visa na haki ya makazi na kufanya kazi katika nchi wanachama,
kulingana na uchambuzi wa shirika la habari la AFP.
Mali,
Burkina Faso na Niger zote zilikuwa wanachama waanzilishi wakati Ecowas
ilipoanzishwa karibu miaka 50 iliyopita.
Uhusiano
kati ya nchi hizo tatu na Ecowas ulikuwa wa wasiwasi baada ya mapinduzi
yaliyofanyika Niger mwezi Julai, Burkina Faso mwaka 2022 na Mali mwaka 2020.
Ecowas ilitoa wito kwa nchi zote tatu kurejea kwenye utawala wa kiraia.
Katika
taarifa yake kuhusu kuondoka kwa nchi hizo tatu, wizara ya mambo ya nje ya
Nigeria ilizishutumu kwa kutochukua hatua kwa nia njema na kuwakosoa viongozi
wao wa kijeshi.
Wiki
iliyopita, Burkina Faso ilitangaza kupokea tani 25,000 za ngano ya bure kutoka
Urusi, ambayo ilifungua tena ubalozi wake huko mnamo mwezi Desemba. Ubalozi
huo ulikuwa umefungwa tangu kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti.
Mauzo ya silaha ya Marekani nje ya nchi yafikia rekodi ya juu zaidi 2023, yakiimarishwa na vita vya Ukraine
Chanzo cha picha, Getty Images
Mauzo ya
silaha ya Marekani katika nchi za nje yaliongezeka kwa kasi, na kufikia rekodi
ya jumla ya $238bn (£187bn), huku uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine ukizidisha
mahitaji.
Serikali ya
Marekani ilifanya majadiliano ya moja kwa moja ya $81bn katika mauzo, ikiwa ni
nyongeza ya 56% kutoka mwaka 2022, Idara ya Ulinzi ilisema.
Mengine
yalikuwa mauzo ya moja kwa moja ya makampuni ya Idara ya ulinzi ya Marekani kwa
mataifa ya nje.
Jirani ya
Ukraine, Poland, ambayo kwa sasa iko kwenye harakati za kupanua jeshi lake,
ilifanya ununuzi mkubwa zaidi.
Poland
ilinunua helikopta za Apache kwa $12bn, na pia ililipa $10bn kwa mifumo ya
makombora ya (Himars) na $3.75bn kwa vifaru vya M1A1 Abrams, idara hiyo ilisema
katika ripoti ya mwaka wa fedha wa serikali ya Marekani uliomalizika Oktoba.
Pia ilitumia
$4bn kwa mifumo ya silaha zilizounganishwa za ulinzi wa angani.
Waziri Mkuu
Donald Tusk ameapa kuendeleza kuboresha mpango wa kisasa wa kijeshi wa serikali
ya awali ya kihafidhina, ambao ulilenga kuifanya Poland kuwa "kikosi
chenye nguvu zaidi cha ardhini barani Ulaya".
Afcon 2023: Mashabiki walivyosherehekea ushindi wa Ivory Coast dhidi ya Senegal
Maelezo ya video, Tazama: Jinsi mashabiki walivyosherehekea ushindi wa Ivory Coast dhidi ya Senegal
Shuhudia nyuso za watu zikipatwa na furaha baada ya
mikwaju ya penati kupigwa ambapo iliwapelekea Ivory Coast kushinda 5 kwa 4
dhidi ya Senegal.
Hawa ni mashabiki kutoka katika mji wa San Pedro
waliokuwa wakifuatilia mpira kupitia runinga kubwa zilizowekwa kwenye eneo
lililotengwa kwaajili ya mashabiki kuangalizia mpira bure.
Mataifa hasimu haya kisoka yalishuka dimbani katika
uwanja wa Charles Konan Banny katika mji wa Yamoussoukro.
Mwandishi wa BBC @frankmavura aliyepo nchini Ivory
alishuhudia shangwe hizo.
Polisi wawakamata wanaume watano juu ya miili iliyopatikana katika jangwa la California
Chanzo cha picha, CBS
Polisi
wamewakamata watu watano baada ya miili kadhaa kupatikana imepigwa risasi
katika eneo la mbali kusini mwa Jangwa la Mojave huko California.
Miili sita
ilipatikana baada ya mwathiriwa aliyepigwa risasi aitwaye 911, kutuma helikopta
ya polisi kwenye eneo la uhalifu mbaya.
Wachunguzi
wa Ofisi ya San Bernardino Sherriff walisema Jumatatu kwamba mzozo huo
unaonekana kuhusishwa na uzalishaji haramu wa bangi.
Wanne kati
ya waathiriwa sita wametambuliwa hadi sasa, polisi walisema.
Miili hiyo -
yote ya wanaume - ilipatikana mnamo Januari 23 nje ya barabara kuu karibu na
mji wa El Mirage, ulioko katika Kaunti ya San Bernardino. Waathiriwa
wote sita walifariki kutokana na majeraha ya risasi, polisi walisema.
Wanne kati ya waathiriwa pia walikuwa wameungua vibaya
sana, Sgt Michael Warrick aliwaambia wanahabari siku ya Jumatatu.
Uchunguzi ulianza wakati wahudumu wa dharura wa 911
walipopokea simu kutoka kwa mmoja wa waathiriwa akiripoti kwamba alikuwa na
jeraha la risasi.
Helikopta ya polisi ilitolewa na kuwapata waathiriwa,
pamoja na SUV na gari dogo lililojaa risasi saa 20:15 saa za eneo (04:15 GMT),
takriban 144km kaskazini mashariki mwa Los Angeles.
Wanaume
wanne kati ya hao walipatikana karibu na kila mmoja, huku mwingine akiwa ndani
ya gari. Maafisa waligundua mwili wa mwisho umbali mfupi.
Picha za
angani za eneo la tukio zilionekana kuonyesha gari hilo aina ya SUV likiwa na
risasi na alama ya madirisha yaliyopasuka na mabaki ya moto.
"Kulingana
na nia, tuna imani kuwa huu unaonekana kuwa mzozo kuhusu bangi," Sgt
Warrick alisema.
Katika
taarifa ya habari, ofisi ya sheriff ilisema kwamba "wachunguzi walidhania
waathiriwa walikuwa wamepanga kukutana katika eneo hilo kwa mabadilishano ya bangi".
Wanaume
watano ambao wamekamatwa "walifika katika eneo hilo, na kwa sababu ambazo
bado zinachunguzwa, waliwapiga risasi waathiriwa sita".
Bunduki nane zimetwaliwa na wachunguzi na zinafanyiwa uchunguzi
kubaini iwapo zilitumika katika mauaji hayo.
Maafisa walikataa kutoa maoni yao iwapo mauaji hayo
yalihusiana na genge, badala yake waliyahusisha na "uhalifu
uliopangwa".
Bangi imehalalishwa kununuliwa na watu wazima na kwa matumizi
huko California tangu 2016, lakini soko haramu bado linaendeleza bangi
isiyotozwa ushuru.
Elon Musk atangaza kipandikizi cha kwanza kwenye ubongo wa binadamu kisichotumia nyaya
Chanzo cha picha, Getty Images
Bilionea wa
kiteknolojia Elon Musk amesema kwa mara ya kwanza kampuni yake ya Neuralink
imefanikiwa kupandikiza kifaa maalum cha eletroniki kwenye Ubongo wa binadamu
kisichotumia nyaya.
Inatarajiwa
kuwa kifaa hicho kuwa kiunganishi cha ubongo na kitawasaidia watu waliopooza
viungo vyote kudhibiti vifaa kwa kutumia mawazo yao pekee.
Akiandika
kwenye mtandao wake wa X, Musk alisema matokeo ya awali yamegundua kuimarika
kwa mishipa ya neva na kwamba mgonjwa aliyefanyikwa upasuaji huo aliripotiwa
kupona vizuri kutokana na operesheni ya Jumapili.
Lengo la
kifaa hicho ni kutenda kama kiunganishi na ubongo kwa kusaidia kukabiliana na
hali matatizo ya neva, kama vile kuruhusu watu waliopooza kudhibiti vifaa kama
simu na kompyuta wakitumia fikra zao.
Wenyeji Ivory Coast wawaondoa mabingwa watetezi Senegal kutoka Afcon
Chanzo cha picha, Getty Images
Wenyeji
Ivory Coast waliwaondoa mabingwa watetezi Senegal kwa mikwaju ya penalti ili
kujikatiatiketi ya robo-fainali ya
Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 kufuatia sare ya 1-1 baada ya muda wa ziada
mjini Yamoussoukro.
Franck
Kessie, ambaye alifunga mkwaju wa penalti dakika nne kabla ya mechi kukamilika muda
wa kawaida, na kuwapatia wenyeji ushindi muhimu, ambaouliwawezesha kujikomboabaada yamwanzo mbaya katika hatua ya makundi na kupelekea kushindwa mara mbili.
Senegal
walikuwa wamenzavizuribaada ya Habib Diallo kufunga dakika ya nne
kutoka kwa krosi ya Sadio Mane.
Robo fainali
ya The ElephantsJumamosi (17:00 GMT)
itawakutanisha na Mali au Burkina Faso, ambao watacheza mechi yao ya hatua ya
16 bora huko Korhogo Jumanne (17:00 GMT).
Wanajeshi watatu wa Marekani waliouawa katika shambulizi la Jordan watambuliwa
Chanzo cha picha, Idara ya Ulinzi ya Marekani
Serikali ya
Marekani imetoa majina ya wanajeshi watatu waliouawa katika shambulizi la ndege
isiyo na rubani huko Jordan siku ya Jumapili.
Sgt William
Jerome Rivers, 46, Mtaalamu Kennedy Ladon Sanders, 24 na Mtaalamu Breonna
Alexsondria Moffett, 23 waliuawa wakati ndege isiyo na rubani iliposhambulia eneo
lao la makazi.
Marekani
imelaumu makundi yanayoungwa mkono na Iran kwa shambulio hilo na Pentagon na
kusema limefuata "nyayo" za Hezbollah.
Pentagon pia ilisisitiza kuwa Marekani haitaki vita na
Iran.
"Hatutafuti vita, lakini tutachukua hatua, na kujibu
mashambulizi dhidi ya vikosi vyetu," alisema msemaji wa Pentagon Sabrina
Singh.
CBS News, mshirika wa BBC wa Marekani, alisema iliambiwa
na afisa wa Marekani kwamba ndege isiyo na rubani iliyotumiwa katika shambulio
hilo inaonekana kuwa ya Iran.
Afisa huyo alisema ni "aina ya ndege isiyo na rubani
ya Shahed," droni ambayo Iran imekuwa ikitoa kwa Urusi.
Hata hivyo, Iran imekanusha shutuma za Marekani na
Uingereza kwamba inaunga mkono makundi ya wanamgambo wanaolaumiwa kwa shambulizi
hilo.
Pentagon ilisema wanajeshi watatu waliouawa Jumapili
asubuhi walitoka katika kitengo cha wanajeshi wa akiba kilichopo Fort Moore,
katika jimbo la Georgia.
Lt Jenerali Jody Daniels, Mkuu wa Hifadhi ya Jeshi na
Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Akiba ya Marekani, alitoa pongezi kwa wanajeshi
waliofariki.
"Kwa niaba ya Jeshi la Akiba, ninashiriki katika
majonzi waliyonayo marafiki, familia, na wapendwa wao. Utumishi na kujitolea kwao
havitasahaulika, na tumejitolea kusaidia wale walioachwa nyuma kutokana na
mkasa huu". Alisema Gen Daniels.
Shambulio
hilo la ndege zisizo na rubani lilifanyika Rukban, kaskazini-mashariki mwa
Jordan, karibu na mpaka wa Syria. Kituo hicho kilitajwa
baadaye na maafisa wa Marekani kama Tower 22.