Afcon 2023: Wanasoka wa Afrika wanaocheza uwanjani licha ya kuhatarisha maisha yao

.

Mchezaji mmoja alikosekana wakati wa michezo miwili ya kwanza ya Zambia kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika 2023, lakini kutochaguliwa kwa Enock Mwepu hakukuwa na uhusiano wowote na uwezo wake.

Badala yake, ni kwa sababu kiungo huyo, ambaye alikuwa nahodha wa nchi yake katika mechi mbili za kwanza za kufuzu mwezi Juni 2022, alilazimika kustaafu soka baada ya kugundulika kuwa na ugonjwa wa moyo.

Wakati huo, mnamo mwezi Septemba akiwa na miaka 24, aliugua nchini Mali na akafanyiwa vipimo aliporejea katika iliyokuwa klabu yake, Brighton ya Ligi Kuu ya Uingereza, na kupokea matokeo hayo mabaya zaidi ambayo hakuwahi kufikiria.

Seagulls walisema Mwepu atakuwa katika "hatari kubwa sana ya kupatwa na mshtuko mbaya wa moyo" ambayo inaweza kusababisha hata kifo ikiwa ataendelea kucheza.

"Ni pigo kubwa kwa Enock, lakini anapaswa kuweka afya yake na familia yake mbele," mkuu wa masuala ya tiba wa Brighton alisema wakati huo.

"Hili ni chaguo sahihi, ingawa ni vigumu kuacha mchezo anaoupenda."

Hata hivyo si uamuzi ambao wanasoka wote wa Afrika katika nafasi ya Mwepu wangefanya.

Miezi miwili tu iliyopita, mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ghana Raphael Dwamena alifariki dunia baada ya kuanguka uwanjani nchini Albania, alipochagua kucheza baada ya kutoa kifaa cha kupandikizwa cha kufuatilia mapigo ya moyo kila mara yaani cardioverter-defibrillator (ICD), kilichowekwa mwaka 2020, ambacho kingeweza kuzuia mshtuko wake mbaya wa moyo.

Kiungo wa kati wa Manchester United Christian Eriksen aliwekewa kifaa kama hicho baada ya kuzimia alipokuwa akiichezea Denmark kwenye michuano ya Euro 2020.

Moja ya vilabu vya zamani vya Dwamena, FC Zurich, iligundua matatizo ya moyo wake kwa mara ya kwanza mwaka 2017 na kushauriwa na wataalam mbalimbali na madaktari wa magonjwa ya moyo kwamba angeweza kuendelea - jambo ambalo alifanya - huku timu hiyo ya Uswisi Super League ikihakikisha kila mara ina kifaa cha kufanya moyo upige tena wakati akiwa uwanjani iwapo kutatokea dharura.

Lakini hakukuwa na kipengele kama hicho katika klabu ya Egnatia FC ya Albania, ambao hawakupata mawasiliano na BBC lakini wakaiambia Athletic mwaka jana kwamba walikuwa na furaha kwa Dwamena kucheza "ili mradi majaribio yote yalifanywa na klabu".

Cha kusikitisha ni kwamba mshambuliaji huyo wa zamani wa Black Stars hakuwa Mwafrika pekee aliyefariki uwanjani mwaka jana.

Kombe la Mataifa ya Afrika 2023

Ratiba ya Mechi & Matokeo
Awamu ya Makundi
Kundi
  • P - Imecheza
  • W - Imeshinda
  • L - Imeshindwa
  • D - Imetoka Sare
  • GD - Tofauti ya bao
  • Pts - Alama
    • Kundi A
      Nchi P W L D GD Pts
      Equatorial Guinea 320167
      Nigeria 320127
      Ivory Coast 3120-33
      Guinea Bissau 3030-50
      • 13/01/2024, 20:00
        Ivory Coast 2
        -
        0 Guinea Bissau
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
      • 14/01/2024, 14:00
        Nigeria 1
        -
        1 Equatorial Guinea
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
      • 18/01/2024, 14:00
        Equatorial Guinea 4
        -
        2 Guinea Bissau
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
      • 18/01/2024, 17:00
        Ivory Coast 0
        -
        1 Nigeria
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
      • 22/01/2024, 17:00
        Equatorial Guinea 4
        -
        0 Ivory Coast
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
      • 22/01/2024, 17:00
        Guinea Bissau 0
        -
        1 Nigeria
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
    • Kundi B
      Nchi P W L D GD Pts
      Cape Verde 320147
      Misri 300303
      Ghana 3012-12
      Msumbiji 3012-32
      • 14/01/2024, 17:00
        Misri 2
        -
        2 Msumbiji
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
      • 14/01/2024, 20:00
        Ghana 1
        -
        2 Cape Verde
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
      • 18/01/2024, 20:00
        Misri 2
        -
        2 Ghana
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
      • 19/01/2024, 14:00
        Cape Verde 3
        -
        0 Msumbiji
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
      • 22/01/2024, 20:00
        Cape Verde 2
        -
        2 Misri
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
      • 22/01/2024, 20:00
        Msumbiji 2
        -
        2 Ghana
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
    • Kundi C
      Nchi P W L D GD Pts
      Senegal 330079
      Cameroon 3111-14
      Guinea 3111-14
      Gambia 3030-50
      • 15/01/2024, 14:00
        Senegal 3
        -
        0 Gambia
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
      • 15/01/2024, 17:00
        Cameroon 1
        -
        1 Guinea
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
      • 19/01/2024, 17:00
        Senegal 3
        -
        1 Cameroon
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
      • 19/01/2024, 20:00
        Guinea 1
        -
        0 Gambia
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
      • 23/01/2024, 17:00
        Gambia 2
        -
        3 Cameroon
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Bouaké)
      • 23/01/2024, 17:00
        Guinea 0
        -
        2 Senegal
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
    • Kundi D
      Nchi P W L D GD Pts
      Angola 320137
      Burkina Faso 3111-14
      Mauritania 3120-13
      Algeria 3012-12
      • 15/01/2024, 20:00
        Algeria 1
        -
        1 Angola
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Bouaké)
      • 16/01/2024, 14:00
        Burkina Faso 1
        -
        0 Mauritania
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Bouaké)
      • 20/01/2024, 14:00
        Algeria 2
        -
        2 Burkina Faso
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Bouaké)
      • 20/01/2024, 17:00
        Mauritania 2
        -
        3 Angola
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Bouaké)
      • 23/01/2024, 20:00
        Angola 2
        -
        0 Burkina Faso
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
      • 23/01/2024, 20:00
        Mauritania 1
        -
        0 Algeria
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Bouaké)
    • Kundi E
      Nchi P W L D GD Pts
      Mali 310225
      Afrika Kusini 311124
      Namibia 3111-34
      Tunisia 3012-12
      • 16/01/2024, 17:00
        Tunisia 0
        -
        1 Namibia
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly)
      • 16/01/2024, 20:00
        Mali 2
        -
        0 Afrika Kusini
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly)
      • 20/01/2024, 20:00
        Tunisia 1
        -
        1 Mali
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly)
      • 21/01/2024, 20:00
        Afrika Kusini 4
        -
        0 Namibia
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly)
      • 24/01/2024, 17:00
        Namibia 0
        -
        0 Mali
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Laurent Pokou)
      • 24/01/2024, 17:00
        Afrika Kusini 0
        -
        0 Tunisia
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly)
    • Kundi F
      Nchi P W L D GD Pts
      Morocco 320147
      DR Congo 300303
      Zambia 3012-12
      Tanzania 3012-32
      • 17/01/2024, 17:00
        Morocco 3
        -
        0 Tanzania
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Laurent Pokou)
      • 17/01/2024, 20:00
        DR Congo 1
        -
        1 Zambia
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Laurent Pokou)
      • 21/01/2024, 14:00
        Morocco 1
        -
        1 DR Congo
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Laurent Pokou)
      • 21/01/2024, 17:00
        Zambia 1
        -
        1 Tanzania
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Laurent Pokou)
      • 24/01/2024, 20:00
        Tanzania 0
        -
        0 DR Congo
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly)
      • 24/01/2024, 20:00
        Zambia 0
        -
        1 Morocco
        -
        (Penati)
        (Uwanja wa Laurent Pokou)
Awamu ya Mtoano
  • Hatua ya 16 Bora
    • 27/01/2024, 17:00
      Angola 3
      -
      0 Namibia
      -
      (Penati)
      (Uwanja wa Bouaké)
    • 27/01/2024, 20:00
      Nigeria 2
      -
      0 Cameroon
      -
      (Penati)
      (Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
    • 28/01/2024, 17:00
      Equatorial Guinea 0
      -
      1 Guinea
      -
      (Penati)
      (Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
    • 28/01/2024, 20:00
      Misri 1
      -
      1 DR Congo
      7
      -
      8
      (Penati)
      (Uwanja wa Laurent Pokou)
    • 29/01/2024, 17:00
      Cape Verde 1
      -
      0 Mauritania
      -
      (Penati)
      (Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
    • 29/01/2024, 20:00
      Senegal 1
      -
      1 Ivory Coast
      4
      -
      5
      (Penati)
      (Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
    • 30/01/2024, 17:00
      Mali 2
      -
      1 Burkina Faso
      -
      (Penati)
      (Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly)
    • 30/01/2024, 20:00
      Morocco 0
      -
      2 Afrika Kusini
      -
      (Penati)
      (Uwanja wa Laurent Pokou)
  • Robo- Fainali
    • 02/02/2024, 17:00
      Nigeria 1
      -
      0 Angola
      -
      (Penati)
      (Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
    • 02/02/2024, 20:00
      DR Congo 3
      -
      1 Guinea
      -
      (Penati)
      (Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
    • 03/02/2024, 17:00
      Mali 1
      -
      2 Ivory Coast
      -
      (Penati)
      (Uwanja wa Bouaké)
    • 03/02/2024, 20:00
      Cape Verde 0
      -
      0 Afrika Kusini
      1
      -
      2
      (Penati)
      (Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro)
  • Nusu- Fainali
    • 07/02/2024, 17:00
      Nigeria 1
      -
      1 Afrika Kusini
      4
      -
      2
      (Penati)
      (Uwanja wa Bouaké)
    • 07/02/2024, 20:00
      Ivory Coast 1
      -
      0 DR Congo
      -
      (Penati)
      (Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
  • Nafasi ya 3 na ya 4
    • 10/02/2024, 20:00
      Afrika Kusini 0
      -
      0 DR Congo
      6
      -
      5
      (Penati)
      (Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny)
  • Fainali
    • 11/02/2024, 20:00
      Nigeria 1
      -
      2 Ivory Coast
      -
      (Penati)
      (Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara)
Nyakati zote ni saa za Ivory Coast na zinaweza kubadilika. BBC haiwajibikii mabadiliko yoyote

Hatari inayowatokea

.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Moustapha Sylla alifariki dunia Machi mwaka jana alipokuwa akiichezea timu ya Racing Club d'Abidjan ya Ivory Coast, nchi ambayo kwa sasa ni mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoendelea.

Kama Dwamena, Sylla pia angefahamu kwamba alikuwa akihatarisha maisha yake kwa kuingia uwanjani, kwani beki huyo alitolewa katika ligi ya Mali mnamo 2022 baada ya uchunguzi wa lazima wa kiafya kabla ya msimu mpya kufichua hali yake.

Kifo chake, akiwa na umri wa miaka 21 tu, kilimsukuma nahodha wa zamani wa Ivory Coast Didier Drogba kutoa ombi kwa niaba ya wachezaji wote wa ligi ya ndani ya nchi yake baada ya kutokea kwa kifo cha tatu kutokana na ugonjwa wa moyo tangu 2019.

"Rambirambi kwa soka la Ivory Coast... vifo 3 vya wachezaji katika ligi kuu ya Ivory Coast katika muda wa chini ya miaka 4…," Drogba alichapisha ujumbe huo kwenye mtandao wa X, wakati huo ukijulikana kama Twitter.

"Ni lini kutakuwa na uchunguzi wa lazima wa kiafya kwa wachezaji "wataalamu"?... Kipimo cha damu, ECG [Echocardiogram], vipimo vya msongo wa mawazo? Dawa kwa ajili ya wachezaji zitafika lini?"

Huku takriban wanasoka zaidi ya 10 wa Kiafrika wakijulikana kufariki kutokana na matatizo ya moyo kwa miaka mingi, mtazamo wa Drogba kuhusu kuhitaji masharti magumu zaidi ya matibabu kwa ajili ya matatizo ya moyo ni moja ambayo nyota mwingine wa zamani wa Chelsea anakubaliana nayo.

"Nilicheza Ulaya mara kadhaa na ninajua kuwa unaposaini mkataba, lazima upite mchakato wa matibabu," Geremi, mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Cameroon ambaye sasa ni mwakilishi wa chama cha wachezaji.

"Tunapaswa kutekeleza hilo hapa Afrika."

Ingawa hii hutokea katika baadhi ya vilabu vya Afrika, haifanyiki kote - sababu moja ya ombi la Drogba.

Kama vile Geremi, ambaye alimpoteza mchezaji mwenzake Marc-Vivien Foe uwanjani mwaka wa 2003, Drogba pia alimpoteza mchezaji mwenzake wa kimataifa kutokana na tatizo la moyo. Cheick Tiote, bingwa wa Afrika mwaka 2015 ambaye alikuwa naye uwanjani mara kadhaa.

Samahani, mtandao wako hauendani
.
Maelezo ya picha, Didier Drogba, ambaye alishindwa katika nia ya kuwa rais wa shirikisho la soka la Ivory Coast mwaka 2022, ametoa wito wa kuwa lazima kwa wachezaji kuchunguzwa afya yao.

Suala moja kuu ni kwamba moyo wa Kiafrika unaaminika kukabiliwa zaidi na matatizo ya moyo, huku timu ya utafiti wa kimatibabu ikiungwa mkono na shirikisho la soka duniani Fifa, mwaka 2009, ikiamua kwamba "wanariadha weusi wa Kiafrika wanaonekana kuwa na hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa ya moyo wakati wa matukio ya michezo".

Suala lingine la msingi ni kukataa kwa baadhi ya wachezaji wenye matatizo ya moyo kutii ushauri wa matibabu.

Daktari wa Afrika Kusini Lervasen Pillay ni mtu ambaye anajua hili vizuri sana, baada ya kuwashauri wanasoka watano tofauti kuacha kucheza kwa sababu ya matatizo yanayohusiana na moyo.

"Sio mazungumzo rahisi kamwe, kwa sababu mtu amekuwa akifanya kazi hii kwa miaka 10-15 na sasa umempa habari ya kusema, 'Sikiliza, huwezi kufanya hivi tena, unahitaji kuwa na mpango mwingine wa maisha', " Dkt Pillay aliiambia BBC Sport Africa.

"Wachezaji kandanda wengi hawajaanzisha Mpango Mwingine wanapokuwa na umri wa miaka 25, na mazungumzo mara nyingi yanatokana na swali hilo kamili: 'Nitafanya nini ikiwa nitaacha kucheza soka?'

Kwa Dk Pillay, ni vigumu kutazama wakati wachezaji ambao wameambiwa wasicheze bado wanashikilia Mpango wao wa awali wa kuingia uwanjani licha ya kujua hatari inayowakodolea macho.

"Unapoona jina la kijana huyo kwenye kikosi cha wachezaji wanaoanza kucheza unashtuka - na ikiwa itakuwa mechi ya kutazamwa kwenye televisheni, nitabadilisha chaneli," alisema.

Mgonjwa mmoja, ambaye jina lake haliwezi kutajwa bila kukiuka sheria za usiri, alifariki miaka miwili baada ya kushindwa kumsikiliza Dk Pillay, na kumwacha na "huzuni kwa muda".

"Ukipata mtu mwenye tatizo la moyo, basi hakikisha huduma yake ya matibabu inakuwa karibu - ili (ili) uwe na vitu kama vile Kifaa cha kufanya moyo uanze kupiga tena, ufikiaji wa hospitali kwa haraka na magari ya dharura, kwa sababu kama huna, unatafuta matatizo."

Wakati FC Zurich ilichukua hatua hiyo haswa kuhusiana na Dwamena, vilabu vingine vingi havijafanya hivyo.

Kumekuwa na matukio ya kukumbukwa hapo awali ambapo masharti ya kimsingi ya matibabu hayakupatikani katika viwanja vya kucheza vya Waafrika, kama vile wakati mwanasoka wa ndani wa Nigeria Chineme Martins alipofariki mwaka wa 2020 kufuatia kushindwa kupatikana kwa matibabu.

Imefasiriwa na Asha Juma