Rwanda: Mahakama ya Rufaa yadumisha kifungo cha miaka 25 dhidi ya Paul Rusesabagina
Mahakama ya Rufaa nchini Rwanda imedumisha hukumu ya kifungo cha miaka 25 kilichotolewa dhidi ya Paul Rusesabagina baada ya kumpata na hatia kwa mashtaka ya ugaidi Jumatatu jioni.
Moja kwa moja
Rwanda: Mahakama ya Rufaa yaidhinisha kifungo cha miaka 25 dhidi ya Paul Rusesabagina

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Paul Rusesabagina Mahakama ya Rufaa nchini Rwanda imeidhinisha hukumu ya kifungo cha miaka 25 kilichotolewa dhidi ya Paul Rusesabagina baada ya kumpata na hatia kwa mashtaka ya ugaidi Jumatatu jioni.
Shujaa wa filamu ya Hollywood kuhusu mauaji ya halaiki ya Rwanda, ‘Hotel Rwanda’, amesusia kwenda mahakamani kuskiza kesi tangu Machi 2021.
Mahakama pia ilimpunguzia kifungo cha miaka 20 hadi 15 jela Callixte Nsabimana anayefahamika kama ‘Sankara’ ambaye alikuwa msemaji wa zamaniwa kundi la waasi FLN linalohusishwa na Bw Rusesabagina
Mahakama ilisema wawili hao walikuwa na hatia ya mashambulizi mabaya yaliyofanywa na kundi la waasi kusini magharibi mwa Rwanda mwaka wa 2019, lakini Bw Nsabimana aliomba msamaha na kushirikiana na mahakama wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Rusesabagina alihadaiwa na kuingizwa kwenye ndege ya kibinafsi kutoka Dubai hadi Kigali mnamo Agosti 2020, akakamatwa na kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari kabla ya kufunguliwa mashtaka
Mahakama ya rufaa pia imedumisha hukumu za mahakama kuu kwa washtakiwa wengine 19, wengi wao wakiwa wanachama wa zamani wa FLN.
Familia ya Bw Rusesabagina inayoishi Ubelgiji na Marekani imelaani kukamatwa na na hatimaye kushatakiwa kwa nchini Rwanda.
Maelezo zaidi:
Elon Musk anunua hisa ya Twitter ya thamani ya dola bilioni tatu

Chanzo cha picha, Reuters
Elon Musk amenunua 9.2% ya hisa za kampuni ya Twitter, kulingana na jalada la dhamana la Marekani.
Taarifa hiyo ilifanya thamani ya hisa za Twitter kupanda kwa 25% kabla ya soko la hisa kufunguliwa.
Mwanzilishi huyo wa Tesla falinunua hisha 73,486,938 za Twitter mnamo Machi 14, kulingana na Tume ya Kubadilishana Dhamana.
Dau hilo lina thamani ya $2.89bn (£2.20bn), kulingana na bei ya mwisho ya Twitter siku ya Ijumaa.
Hisa hizo zinamfanya kuwa mmoja wa wanahisa wakubwa katika kampuni hiyo na ni zaidi ya mara nne ya 2.25% ya mwanzilishi wa Twitter Jack Dorsey.
Musk ni mtumiaji wa kawaida wa Twitter aliye na wafuasi zaidi ya milioni 80, ingawa hivi majuzi alisema "anafikiria sana" kuunda jukwaa mpya la mtandoa wa kijamii.
Mwishoni mwa mwezi uliopita Musk aliuliza wafuasi wake ikiwa wanafikiri mtandao wahimiza una uhuru wa kujieleza.
"Uhuru wa kujieleza ni muhimu kwa demokrasia inayofanya kazi.
Je, unaamini Twitter inafuata kanuni hii kwa dhati?" Kisha akauliza "Je, jukwaa jipya linahitajika?"
Shambulizi la treni ya Kaduna nchini Nigeria: Watu 168 bado hawajulikani walipo

Chanzo cha picha, NRC
Maelezo ya picha, Takriban watu wanane waliuawa katika shambulio hilo wiki moja iliyopita Watu 168 bado hawajulikani walipo nchini Nigeria baada ya shambulio baya la wiki iliyopita dhidi ya treni yenye shughuli, shirika la reli la serikali linasema.
Haijabainika ni watu wanagapi kati ya hao 168 waliotekwa nyara- baadhi yao huenda wameenda nyumbani bila kufahamisha mamlaka
Watu waliokuwa wamejihami kwa silaha walilipua sehemu ya ya treni hiyo ya kutoka mji mkuu, Abuja, na mji wa Kaduna kaskazini mwa Nigeria Jumatatu iliyopita.
Wakati wa mkasa huo abiria wanane waliuawa.
Manusura mmoja aliambia BBC jjinsi uamuzi wa kubadilisha gari ungeweza kuokoa maisha yake, na ya familia yake.
"Nina furaha kuwa niko hai na ni mzima," alisema baada ya kuomba asitambulishwe.
Soma zaidi:
Familia iliyozikwa kwenye kaburi la kina kifupi 'iliteka siku 10 zilizopita'

Miili minne ampatikana katika kaburi lenye kina kifupi katika kijiji cha Motyzhyn baada ya kudaiwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Urusi, mwandishi wa BBC Yogita Limaye anaripoti.
Miili hiyo imetambuliwa kuwa ya mkuu wa kijiji hicho Olha Sohnenko, mumewe na mwanawe. Mwili wa nne haujatambuliwa. Olha Sohnenko alizaliwa mwaka wa 1971. Mume wake, Igor, alikuwa na umri wa miaka mitano, huku mwanawe Oleksander alizaliwa mwaka wa 1996, mwandishi wetu anaripoti.
Familia hiyo iliteka na wavamizi wa Urusi siku 10 zilizopita, mkuu wa kijiji cha Makariv, Vadym Tokar, alisema kwenye Telegram.
Wanajeshi wa Urusi wanadaiwa kufika kwenye nyumba ya Sohnenko ambapo walifanya upekuzi, wakachukua gari na kuondoka.
"Walitaka kumchukua Olha pekee, lakini mumewe alisisitiza angeenda naye - baada ya saa sita, pia walimchukua mtoto wake wa kiume," Naibu Mkuu wa Halmashauri ya Mkoa wa Kyiv Tetiana Semenova alinukuliwa na vyombo vya habari vya Ukraine akisema.
Alisema kuwa anashuku msaliti alikuwa mwiigizaji kijijini, ambaye aliwaambia wavamizi, mahali wanapoishi wakuu wa wanakijiji"
Unaweza pia kusoma
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
Mzozo Ukraine: 'Mtoto wangu anaficha mikate, akihofia chakula kukosekana'

Maelezo ya picha, Nadia na watoto wake waliweza kutoroka Mariupol baada ya kujificha kwenye handaki kwa wiki tatu. Makumi na maelfu ya raia wamebaki nchini Ukraine wamekwama katika mji wa Mariupol wa Ukraine uliozingirwa, bila umeme, maji ya bomba au gesi.
Uganda yamtimua kiongozi wa kundi la Rwandan National Congress-RNC

Chanzo cha picha, ROBERT MUKOMBOZI/FACEBOOK
Serikali ya Uganda imemumtimua kiongozi mmoja wa kundi la Rwandan National Congress-RNC linalodaiwa kuwa wapinzani wa utawala wa wa Rais Paul Kagame walioko uhamishoni nchini Afrika kusini.
Katika ujumbe wa Tweeter wa Jenerali Muhoozi ambaye ni mkuu wa kikosi cha jeshi la nchi kavu la Uganda ukiambatana na picha ya bwana Robert Mukombozi ikionyesha akipanda ndege kwenye uwanja wa kimataifa wa Entebbe.
Mwanaye Rais Museveni Jenerali Muhoozi Kainerugaba amelezea kutimiza matakwa na serikali ya Rwanda baada ya kukutana na Rais Paul Kagame na kufunguliwa mpaka wa Gatuna wa Rwanda na Uganda uliokuwa umefungwa karibu miaka mitatu.
Haijulikani Robert Mkombozi ambaye alizaliwa Uganda na kufanya kazi nchini Uganda alielekea taifa gani ila aliwasili Uganda akitokea nchini Australia.
Kundi linalopiganisha utawala wa Rwanda la RNC lilianzishwa na waliokuwa maafisa wa serikali ya Rais Kagame, Kayumba Nyamwasa na Patrick Karegeya mnamo mwaka 2010, wakifanya vitendo vyao vya uasi nchini Afrika Kusini wanakoishi.
Hivi karibuni Jenerali Muhoozi alisambaza ujumbe kwenye mtandao wake wa Tweeter akimuonya Nyamwasa akomeshe kuendesha shughuli zake dhidi ya utawala wa Rwanda kupitia Uganda.
Serikali ya Rwanda imekuwa ikilaumu Uganda kuwarusu watu wanaotaka kuagusha serikali ya Kigali kufanya harakati zao nchini Uganda miongoni mwa mada ya Rwanda kurudisha uhusiano wa mataifa hayo mawili.
Mpigania Uhuru Muthoni wa Kirima alinyoa nywele zake baada ya miaka 70

Chanzo cha picha, NATION
Mwishoni mwa juma, Wakenya wengi walisimuliwa kisa cha mpigania uhuru wa zamani mwenye umri wa miaka 92 ambaye alinyolewa nywele zake na Mama Ngina Kenyatta siku ya Jumamosi.
Muthoni wa Kirima anafahamika zaidi kuwa mwanamgambo wa Mau Mau aliyepigana na wakoloni wa Uingereza waliokuwa wakipigania uhuru wa Kenya.
Tofauti na wapiganaji wengine, baada ya kupata uhuru Muthoni wa Kirima hakunyoa nywele zake. Nywele ndefu zilikuwa ni moja ya alama za wapiganaji hao wanaoishi msituni, baada ya kupata uhuru kwa kunyoa shanga hizo ilikuwa ni moja ya mambo mengi ambayo wengi wao walifanya mara moja kama ishara ya uhuru.
Muthoni Wa Kirima amekuwa msituni kwa miaka saba, na historia yake inasema kuwa wanawake wengine waliwekwa kama wakuu wa wapelelezi wa Mau Mau au wasambazaji wa chakula msituni.
Muthoni alikuwa mmoja wa wanawake wachache sana waliopigana katika mstari wa mbele, ambapo aliondoa cheo cha Field Marshal.
Mama Ngina Kenyatta alikuwa rafiki yake wakati huo na aliishi msituni na alifungwa katika Gereza Kuu la Kamiti, kulingana na jarida la Nation.
Katika miaka ya hivi majuzi, Muthoni wa Kirima aliiambia K24 nchini Kenya kwamba ameapa kutonyoa nywele zake.
Katika hafla ya kunyoa nywele nyumbani kwake katika jimbo la Nyeri katikati mwa nchi, Muthoni alisema amenyoa nywele kwa sababu "matakwa yake kama mpigania uhuru yametimizwa na serikali".
Hakusema ni matakwa gani, kwa mujibu wa Nation. Mama Ngina Kenyatta, mke wa rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta, na mama yake rais wa sasa, Uhuru Kenyatta, alisema anajivunia kunyoa nywele zake.
Baada ya kunyoa nywele hizo zenye urefu wa takriban mita 2, Mama Ngina aliizungushia bendera ya Kenya akisema itahifadhiwa katika jumba la makumbusho.
Muthoni wa Kirima, baada ya kunyoa nywele, alitoa wito kwa Kenya kuwa na umoja na amani na watu wake. Mau Mau walipigania uhuru wa Kenya kuanzia mwaka 1952 hadi 1960, wakitawaliwa na watu wa kabila la Wakikuyu kwa msaada wa makabila mengine kama vile Wameru na wengine.
Kenya ilipata uhuru mwaka wa 1963. Muthoni wa Kirima ni mmoja wa wapiganaji wachache wa Mau Mau ambao bado wako hai.
Moto wasoko la Hargeisa,Somaliland ulisababisha hasara ya takriban dola bilioni moja

Chanzo cha picha, FAHAD KARIE
Maelezo zaidiyanaibuka kuhusu uharibifu uliosababishwa na moto mkubwa ambao uliteketeza soko kuu la wazi huko Hargeisa, mji mkuu Somaliland siku ya Ijumaa.
Tume iliyoundwa na utawala wa eneo hilo inasema kuwa moto huo huenda uliharibu mali yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni moja huku msaada kutoka nchi jirani ukianza kuwasili.
Sehemu za video za baada ya uharibifu mkubwa ulioachwa na moto huo zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii wikendi huku wafanyabiashara wanyonge wakihesabu hasara.
Ilichukua masaa kuzima moto huo, ambao ulianza Ijumaa jioni na kuteketeza Soko lote- njia ya maisha ya mamia ya maelfu ya familia za kipato cha chini huko Hargeisa.
Tume iliyopewa jukumu na Rais wa Somaliland Muse Bihi Abdi kutathmini uharibifu uliosababishwa na moto huo ilisema kuwa zaidi ya dola bilioni moja huenda zilipotea.
"Kulingana na takwimu za awali, uharibifu na uliosababishwa na maafa hapa unakadiriwa kuwa kati ya dola moja na nusu na bilioni mbili," alisema Meya wa Hargeisa Abdikarin Ahmed Mooge.
Akizungumza Jumapili baada ya kukutana na jumuiya ya wafanyabiashara mjini Mogadishu, Waziri Mkuu wa Somalia, Mohamed Hussein Roble, alitangaza kwamba serikali ya shirikisho ya Somalia itatoa msaada wa dola milioni 11.7 kama sehemu ya jibu la dharura kwa moto mbaya ulioharibu soko kuu la kibiashara la Hargeisa, Waheen, Jumamosi. .
Kwa upande mwingine, viongozi wa Dunia, akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, Abiy Ahmed wa Ethiopia na Mbunge wa Marekani Ilhan Omar, wameonyesha huruma kwa watu wa Hargeisa na kuahidi kusimama nao katika wakati huu mgumu.
Soko hili linahudumia Ethiopia, Djibouti na Baadhi ya maeneo ya Somalia na ni soko la 3 kwa ukubwa katika Pembe ya Afrika.
Wanafunzi milioni nne kufaidika na mpango wa 'Shule Bora' Tanzania

Chanzo cha picha, Twitter-Ikulu
Waziri wa Uingereza barani Afrika, Amerika kusini na Caribbean, Bi Vicky Ford anatarajia kuzindua mpango wa miaka mitano wa elimu ‘Shule Bora’ ambao unafadhiliwa na serikali ya Uingereza.
Mpango huo umegharimu pauni milioni 89 na utadumu kwa miaka mitano, ambapo umetoa kipaumbele kwa wanafunzi wenye ulemavu, wanafunzi wa kike na wale wanaotoka katika kaya masikini.
Katika taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania, Bi ford ataungana na mawaziri wa elimu nchini humo akiwemo waziri wa Elimu Adolf Mkenda.
Mpango huo unatarajia kuwafikia wanafunzi milioni nne, katika mikoa tisa ya Tanzania, wengi wakiwa kutoka familia duni, wenye ulemavu na Watoto wa kike.
Bi Ford atafanya pia ziara mbalimbali na kugusia mausala la maadiliko ya tabia nchi na biashara.
Ilisema taarifa hiyo. Bi Ford amefika Tanzania kwa ziara ya siku tatu, alikutana pia na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan siku ya Jumapili. Vicky Ford aliteuliwa kuwa Waziri wa masuala ya Afrika mwaka 2021.
Foleni ndefu zashuhudiwa Kenya huku tatizo la mafuta likiendelea

Chanzo cha picha, AFP
Uhaba wa mafuta katika nchi nzima unaendelea kutanda nchini Kenya, huku miji mikuu ikiripoti kuwa na foleni ndefu kwenye vituo vichache vya mafuta ambavyo vina bidhaa hiyo.
Kuna sababu zinazokinzana kwa nini uhaba huo unashuhudiwa.
Rais Uhuru Kenyatta anasema ni kutokana na mzozo wa kimataifa uliosababishwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Kampuni ya kitaifa ya kuhifadhi mafuta - Kenya Pipeline - inasema kuna kiasi cha kutosha na mdhibiti EPRA ikionya kampuni yoyote inayoficha mafuta hayo kwamba itapokonywa leseni .
Wachambuzi wanasema ruzuku iliyocheleweshwa iliyoahidiwa na serikali kwa wauzaji mafuta ili kuwaokoa watumiaji kutokana na athari za msukosuko wa ulimwengu kunasababisha uhaba huo.
Mauaji ya Bucha yawashtua viongozi na kuzua wito wa vikwazo vikali zaidi

Chanzo cha picha, EPA
Kama tunavyozidi kuripoti, kumekuwa na wito wa kuiwekea Urusi vikwazo vipya na vikali zaidi kutokana na mauaji yanayoonekana ya idadi kubwa ya raia katika mji wa Bucha, karibu na Kyiv.
Ukraine imeshutumu wanajeshi wa Urusi kwa "mauaji ya kimakusudi" baada ya miili ya watu wasiopungua 20 waliovalia nguo za kiraia kupatikana mitaani katika mji huo.
Mamia ya maiti zinasemekana kupatikana katika miji ya nje ya mji wa Kyiv kufuatia kuondoka kwa wanajeshi wa Urusi katika eneo hilo, kwa mujibu wa maafisa wa Ukraine. Urusi inakanusha mauaji yoyote.
Haya ndiyo maoni ya hivi punde:
• Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa wito wa kuwekewa vikwazo zaidi vinavyolenga mauzo ya makaa ya mawe na mafuta ya Russia - akiviambia vyombo vya habari vya Ufaransa "kuna ushahidi wa wazi uhalifu wa kivita"
•Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Christine Lambrecht anasema Umoja wa Ulaya lazima sasa ujadili kupiga marufuku uagizaji wa gesi ya Urusi - jambo ambalo viongozi wamesita kufanya hadi sasa licha ya kuhimizwa na Ukraine kwa sababu ya athari ambayo ingekuwa kwa watumiaji wa Ulaya.
• Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameeleza picha za maiti kuwa ni "pigo tumboni"
• Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alilaani kile alichokiita "mashambulizi ya yenye ukatili". Ripoti zinaonyesha kuwa Uingereza inaweza kutangaza vikwazo vipya wiki hii
• Wakati huo huo rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel alisema vikwazo na uungwaji mkono zaidi wa Umoja wa Ulaya "ziko njiani"
Unaweza pia kusoma
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
Louis van Gaal: Maneja wa zamani wa Man Utd afichua ana saratani ya tezi dume

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal anasema anapokea matibabu ya saratani ya tezi dume.
Mholanzi huyo ambaye kwa sasa anaiongoza timu ya taifa ya Uholanzi, alitoa tangazo hilo kwenye kipindi cha televisheni cha Uholanzi Humberto siku ya Jumapili.
Van Gaal, 70, alisema ameficha habari hizo kutoka kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko ya hivi majuzi ya kimataifa.
"Sikutaka kuwaambia wachezaji wangu kwa sababu ingeweza kuathiri uchezaji wao," aliongeza.
Van Gaal yuko katika kipindi chake cha tatu kama kocha mkuu wa Uholanzi, akiwa ameiongoza hadi nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia la 2014 na sasa kwenye fainali za 2022 huko Qatar.
Aliongeza: “Katika kila kipindi nikiwa meneja wa timu ya Taifa nililazimika kuondoka usiku kwenda hospitali bila wachezaji kujua mpaka sasa, huku nikidhani ni mzima wa afya, lakini.. sipo. "
Katika kipindi cha miaka miwili akiwa Manchester United, Van Gaal aliiongoza kufanikiwa Kombe la FA mnamo 2016 kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho.
Pia ameshinda mataji ya ligi akiwa na Barcelona, Bayern Munich, AZ Alkmaar na Ajax, ambapo aliiongoza timu hiyo ya Uholanzi kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa mwaka 1995.
Mapigano yazuka kati ya vikosi vya Ethiopia na wapiganaji karibu na mpaka wa Kenya

Chanzo cha picha, Getty Images
Mapigano yameripotiwa kati ya watu wenye silaha na vikosi vya usalama vya Ethiopia katika mji wa Moyale kusini mwa Ethiopia karibu na mpaka wa nchi hiyo na nchi jirani ya Kenya.
Afisa wa eneo hilo ameambia BBC kwamba mapigano hayo yalitokea kati ya Jumamosi jioni na Jumapili asubuhi.
Afisa huyo amesema watu hao waliokuwa na silaha walikuwa wanachama wa kundi la waasi la Oromo Liberation Army (OLA) lakini ameshindwa kufichua iwapo kulikuwa chanzo cha mapigano hayo .
Tukio hilo ni dalili nyingine ya kudorora kwa usalama katika maeneo ya kusini na magharibi mwa nchi.
Makubaliano ya kibinadamu yaliyokubaliwa kati ya serikali na vikosi vya Tigray yamezua matumaini ya azimio la vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miezi kumi na saba huko kaskazini. Lakini katika eneo lenye watu wengi zaidi nchini la Oromia mapigano yameendelea kuripotiwa kati ya vikosi vya serikali- ambavyo ni pamoja na jeshi na polisi wa mkoa- na OLA.
Siku ya Jumamosi afisa mkuu wa kijeshi, Kanali Girma Ayele alisema vikosi vya usalama vilikuwa vinachukua hatua dhidi ya OLA katika kile alichokiita "operesheni iliyoratibiwa."
OLA kwa upande wao wanasema wanashinda vita. Odaa Tarbii, msemaji wa kundi hilo, amedai katika ujumbe wa Twitter siku ya Jumatatu kwamba vikosi vya serikali vimewaua waasi wengi katika eneo linaloitwa Malka Lammii kusini mwa Oromia.
Kuna wasiwasi kwamba ukosefu wa utulivu katika maeneo mengi unaweza kuzidisha machafuko ya kibinadamu kote nchini. Kulingana na Umoja wa Mataifa mchanganyiko wa ukame, migogoro na milipuko ya magonjwa inaweza kuwalazimisha zaidi ya Waethiopia milioni 20 kuhitaji msaada wa kibinadamu mwaka huu.
Wapinzani wa Sudan Kusini wakubaliana juu ya uongozi wa pamoja wa jeshi

Chanzo cha picha, AFP
Wapinzani wa Sudan Kusini wametia saini makubaliano ya kuunda kamandi ya jeshi la pamoja , nguzo muhimu ya makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwaka 2018.
Mkataba huo ulitiwa saini siku ya Jumapili katika mji mkuu, Juba, kufuatia upatanishi wa nchi jirani ya Sudan.
Mvutano kati ya Rais Salva Kiir na Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar hivi karibuni ulisababisha mapigano kati ya vikosi vyao.
Makubaliano hayo yanaweka masharti ya kuwajumuisha makamanda wa upinzani katika vikosi vya jeshi.
Mrengo wa Rais Kiir utakuwa na uwakilishi wa 60% katika nyadhifa muhimu katika jeshi, polisi na vikosi vya usalama. SPLM-IO ya Bw Machar na makundi mengine ya upinzani yatachukua asilimia 40 iliyobaki.
Upinzani utawasilisha orodha ya makamanda wao ndani ya kipindi cha wiki moja.Itafuatiwa na kuhitimu kwa vikosi vya umoja na kutumwa kwao - ambayo haipaswi kuzidi muda wa miezi miwili, kulingana na mpango huo."Watu wa Sudan Kusini wanatamani amani na amani inahusu usalama na leo tumepiga hatua kubwa katika hilo.
Tumekubaliana kwamba tutasonga mbele,” akasema Meja Jenerali Martin Abucha, aliyewakilisha mrengo wa Bw Machar.
“Ninataka kutoa wito kwa wenzangu kutoka pande nyingine kwamba ni muhimu kunyamazisha milio ya bunduki ili Sudan Kusini ifanikiwe.
Kusiwe na mapigano, kusiwe na mashambulizi,” aliongeza.Kambi ya kikanda, Mamlaka ya Kiserikali ya Maendeleo (Igad), imesifu mpango huo kama "mafanikio makubwa".
Angélique Kidjo na Black Coffee washinda tuzo za Grammy

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwimbaji wa Benin Angélique Kidjo na DJ Black Coffee wa Afrika Kusini wameshinda tuzo katika Grammys mwaka huu.
Kidjo alishinda albamu bora ya mwaka ya muziki wa dunia kwa ajili ya albamu yake ya Mother Nature. Iliwashirikisha wanamuziki wa Nigeria Burna Boy, Yemi Alade na Mr Eazi.
Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 61 aliwashinda Wanigeria Wizkid, Femi Kuti na Mghana Rocky Dawuni katika tuzo hiyo.
Huu ulikuwa ushindi wake wa tano wa Grammy baada ya kushinda kitengo hicho mnamo 2014, 2015, na 2019.
Katika hotuba yake ya kukubali tuzo alitoa pongezi kwa wasanii wa kizazi kipya barani Afrika ambao alisema watatamba katika sanaa ya muziki ulimwenguni.
Black Coffee wa Afrika Kusini alishinda albamu bora ya muziki wa densi/kielektroniki. Alishinda tuzo ya albamu yake ya Subconsciously.
Ilikuwa ni tuzo yake ya kwanza kabisa ya Grammy.
Alikubali tuzo hiyo pamoja na mwanawe mkubwa, Esona.
"Nataka kumshukuru Mungu kwa zawadi ya muziki na kuweza kuishiriki na ulimwengu na kuponya roho na kusaidia watu kupitia chochote wanachopitia maishani," alisema.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Picha za setilaiti zaonyesha mtaro wa futi 45 kwenye eneo la kaburi huko Bucha ,Ukraine

Chanzo cha picha, Maxar Technologies/Reuters
Picha za satelaiti kutoka Bucha zinaonyesha mtaro wa futi 45 kwenye eneo ambapo kaburi la watu wengi limetambuliwa, kampuni ya data ya satelaiti ya Marekani inasema.
Picha zilizonaswa Machi 31 na kutolewa na Maxar Technologies zinaonyesha kile kinachoonekana kuwa mtaro ndani ya eneo lenye Kanisa la Mtakatifu Andrew na Pyervozvannoho All Saints .
Kampuni hiyo ilisema dalili za uchimbaji zinaweza kuonekana kwenye picha zilizochukuliwa mapema Machi 10.
BBC haikuweza kuthibitisha picha hizo mara moja, ingawa timu kutoka CNN iliripoti kuona miili kwenye kaburi la pamoja kwenye eneo hilo.
Unaweza pia kusoma
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
Viongozi wa kimataifa walaani mauaji 'ya kikatili' ya Bucha

Chanzo cha picha, Getty Images
Nini cha hivi punde?
Ikiwa unajiunga nasi tu, au unahitaji muhtasari, haya ndiyo mapya tuliyo nayo kuhusu madai ya mauaji ya raia yaliyofanywa na vikosi vya Urusi katika mji wa Bucha nchini Ukraine
Mauaji ya Bucha
• Kumekuwa na madai ya mauaji ya kiholela huku wanajeshi wa Urusi wakitoroka kutoka maeneo muhimu ya uwanja wa vita karibu na mji mkuu wa Kyiv.
•Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine ameshutumu wanajeshi wa Urusi kwa "mauaji ya kimakusudi" katika mji wa Bucha, karibu na Kyiv.
• Picha kutoka jiji zinaonyesha uharibifu mkubwa na miili iliyotapakaa mitaani
•Mwandishi wa BBC Jeremy Bowen anaripoti kwamba wanajeshi wa Ukraine walipata takriban watu 20 waliouawa, baadhi wakiwa wamefungwa mikono nyuma ya migongo yao, walipokuwa wakiingia mjini.
• Waendesha mashtaka wa Ukraine wanasema wamepata miili 410 katika miji kadhaa karibu na Kyiv
Shutuma kali
• Viongozi wa dunia wamelaani mauaji hayo
•Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alisema mauaji hayo "bado ni ushahidi zaidi" kwamba Urusi ilikuwa ikifanya uhalifu wa kivita nchini Ukraine, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akielezea matukio hayo kama "pigo "
• Makamu chansela wa Ujerumani aliyataja mauaji hayo kuwa "uhalifu mbaya wa kivita" na rais wa Ufaransa alisema picha kutoka Bucha "hazivumiliki"
Urusi inajibu
• Katika taarifa, wizara ya ulinzi ya Urusi ilikanusha kwamba raia yeyote alijeruhiwa na vikosi vya Urusi huko Bucha
• Wanaita picha kutoka mji kuwa "Utunzi mwingine wa serikali ya Kyiv kwa vyombo vya habari vya Magharibi"
Unaweza pia kusoma
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo Jumatatu tarehe 4 Aprili 2022
