Ni Siku
ya 14 ya uvamizi kamili wa Urusi nchini Ukraine. Kwa hivyo, ikiwa unajiunga
nasi, hapa kuna muhtasari wa haraka kuhusu matukio makuu katika saa 12
zilizopita:
•
Kulikuwa na taarifa za ving'ora vya anga Jumatano asubuhi katika miji kadhaa ya
Ukraine, ukiwemo mji mkuu wa Kyiv
• Hatua
zote mbili za uhamishaji wa watu kutoka
mji wa kaskazini-mashariki wa Sumy - ambao kwa siku kadhaa umekuwa chini ya
mashambulizi makali ya Urusi - zilikamilika kwa mafanikio, Ukraine ilisema.
• Rais
wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitoa hotuba ambayo haijapata kifani kutoka
ofisi yake mjini Kyiv kwa wabunge wa Uingereza katika Baraza la Commons.
• Alimnukuu
Winston Churchill, akiionya Urusi kwamba
"tutapigana msituni, mashambani, ufukweni, mitaani"
• Rais
wa Marekani Joe Biden alitangaza kupiga marufuku kabisa Marekani kuagiza mafuta, gesi na makaa ya mawe nchini Urusi
• Umoja
wa Mataifa ulisema wakimbizi milioni mbili sasa wameikimbia Ukraine - katika
hali ambayo sasa ni mzozo wa wakimbizi unaokua kwa kasi zaidi barani Ulaya
tangu Vita vya Pili vya Dunia.
•
McDonald's, Starbucks na Coca-Cola ni kampuni za hivi punde zaidi za Magharibi
kusitisha kazi zao nchini Urusi
Urusi
yatangaza usitishaji mwingine wa mapigano kwa raia kuondoka mijini
Moscow
imetangaza usitishaji vita kwa muda ili
kuruhusu raia katika miji inayoshambuliwa kukimbia, kulingana na ripoti za
vyombo vya habari vya serikali ya Urusi.
Barabara
zitawekwa tena kwa Kyiv, Chernihev, Sumy, Kharkiv na Mariupol saa 10:00 kwa saa
za huko. Ni mara ya tatu ya usitishaji vita kutangazwa na Moscow.
Jana,
maafisa wa Ukraine walisema walifanikiwa kuwahamisha watu 5,000 kutoka Sumy -
uokoaji wa kwanza wa watu wengi uliofaulu.
Walakini,
jaribio kama hilo kwa wale wa Chernihiv lilishindwa kwa sababu Urusi iliendelea
kushambulia njia ya kutokea, Ukraine ilidai.
Ukraine: Mke wa Rais Olena Zelenska alaani mauaji ya watu
Mke wa Rais wa Ukraine Olena Zelenska ametoa taarifa ya kusikitishwa na uvamizi wa Urusi, akilaani "mauaji ya watu wengi" nchini humo.
Aliangazia zaidi vifo vya watoto, akitaja majina ya watoto watatu waliokufa katika mashambulizi ya mabomu.
Amesema Ukraine inataka amani lakini italinda mipaka yake na utambulisho wake.
Bibi Zelenska, 44, hajulikani aliko, na mumewe Rais Volodymyr Zelensky anasema familia yake inalengwa na vikosi vya Urusi.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi