Majid Khan: Mfungwa aliyedhulumiwa kingono na madaktari wa CIA

Hayo yalitajwa kwenye ushuhuda wa kurasa 39 na Majid Khan, mwanachama wa al Qaeda aliyezuiliwa kwa karibu miongo miwili kwenye kambi ya jeshi la wanamaji wa Marekani huko Guantanamo.

Mwanaume huyo mzaliwa wa Saudi Arabia aliyekulia Pakistan Ijumaa alihukumiwa kifungo cha miaka 26 baada ya kukiri kulisaidia kundi la al Qaeda.

Lakini kama sehemu ya makubaliano, aliruhusiwa kusoma yaliyomkumba, ukiwa ndio ushuhuda wa kwanza kwa Umma kuhusu dhuluma dhidi ya mfungwa baada ya mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 mjini New York na huko Pentagon.

Khan, aliyekuwa anaishi Baltimore nchini Marekani kabla ya kuajiriwa na al Qaeda, aliiambia mahakama kuwa alifungwa minyororo kwa siku kadhaa, mara nyingi akining'inia bila chakula wala nguo, kwenye seli zenye giza na muziki uliochezwa kwa sauti, bila ya choo wala umeme.

Sikuwa na namna ya kwenda msalani, hata ndoo kwa hivyo nililazimika kujisaidia ndani ya seli.

Khan alisoma ushuhuda huo mbele ya majaji sita kutoka jeshi la Marekani ambao walijadiliana kwa chini ya saa tatu siku iliyofuata na kumhukumu miaka 26 kutokana na kukiri kwake Februari mwaka 2012.

Hata hivyo huku hiyo ni mfano tu kwa kuwa Khan na mawakili wake walifikia makubaliano ya siri na maafisa wa vyeo vya juu huko Pentagon ambapo anaweza kuachiliwa kati ya Februari 2022 na kabla ya Februari 2025.

Khan alikiri kufanya kazi kama msafirishaji wa al Qaeda na amekuwa kizuizini tangu akamatwe nchini Pakistan mwaka 2003.

Dhuluma

Kulingana na ushuhudu wake, dhuluma dhidi yake zilikuwa kubwa hadi akaanza kuwaambia waliokuwa wanamhojia kile walitaka kuskia, "ndio dhulukma hizo zipate kukoma."

"Lakini vile nilitoa ushirikino na kuwaambia ndivyo walivyonitesa zaidi," alisema.

Kwenye ushuhuda wake anadai kuwekwa kwenye mfereji wa maji ya barafu, vile alifungwa nyororo kwa siku kadhaa na kupokea vitisho kuhusu ulipizaji kisasi dhidi ya famalia yake nchini Marekani.

"Baada ya siku mbili za kuning'inia, kukosa usingizi na kukaa kwenye mazingira yenyebaridi kali, nilichanganyikiwa, Ninakumbuka nikiona ng'ombe, mjusi mkubwa," alisema.

Kulingana na ushuhuda wake ni dhuluma alizofanyiwa hasa kwenye sehemu za siri ndio zimemuacha mdhara makubwa kwake.

Khan alikulia Pakistan na kuhamia Marekani akiwa na umri wa miaka 16. Anasema alikuwa kijana mdogo aliyekuwa anaishi katika mazingira magumu wakati aliajiriwa na al Qaeda: Sasa akiwa na umri wa miaka 41 anadai analikana kundi la al Qaeda na ugaidi.

Majibu

Kufuatia hukumu yake Khan, maafisa saba ya vyeo vya juu waliokuwa kwenye mahakama ya jeshi walikana madai kuhusu mateso aliyoyataja.

Kwenye barua iliyotumwa kwa gazeti la New York Times ambapo asilimia kubwa ya majaji walitaka Khan ahurumiwe, jeshi lilitaja vitendo dhidi ya mfungwa huyo kama doa kwa Marekani.

Khana alikumbwa na dhuluma za kimwili na kisaikolojia kupita mipaka ya mbinu za mahojiano zinazoruhusiwa.

Maafisa hao pia walikosoa hataua ya Khan kuzuiwa bila mashtaka kwa miaka 9 na kunyimwa nafasi ya kuwa na wakili kwa miaka minne unusu ya kwanza.

"Vita dhidi ya ugaidi"

Septemba mwaka 2001 mashambulizi yalisababisha Marekani kuanzisha kampeni ndefu na ya gharama ya juu katika historia yake dhidi ya kile kilichotajwa kuwa vita dhidi ya ugaidi.

Oparesheni hizo za kimataifa zilizoungwa mkono na nchi washirika na NATO, hazikusababisha tu vita sehemu tofauti mashariki ya kati lakini pia kuwawinda viongozi wakuu na wanachama wa kile Marekani ilikitaja kuwa makundi ya kigaidi.

Tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000 viongozi wa makundi ya al Qaeda, Taliban na makundi mengine yenye siasa kali walianza kuonekana kwenye orodha ya waliosakwa zaidi duniani.

Tangu Januaei 2002, wafungwa wa kwanza walianza kuwasili Guantanamo na kwa taratibu gereza kwenye kambi ya jeshi mashariki mwa Cuba lilijaa baadhi ya wanaume waliotajwa kuwa hatari zaidi duniani.

Lakini haikuwa hiyo tu: Marekani ilianza kubuni vituo vya kuzuia kwenye nchi nyingi, ambapo wafungwa walihojiwa kupata habari kuhusu al Qaeda na mipango ya mashambulizi ya kigaidi.

Kati ya mbinu zilizotumika kuwahoji wafungwa, na namna fulani ya kuwafanya wahisi kufa maji, walifungiwa ndani ya visanduku vidogo, waliweka katika mazingira waliyotengwa, kunyimwa usingizi, chakula, kulazimishwa kukaa uchi na kudhuduliwa katika sehemu zao za siri.