Ni zaidi ya
saa 24 tangu Rais wa Marekani Donald Trump atangaze kusitisha mapigano kwa wiki
mbili nchini Iran, jambo ambalo Israel, Iran na wapatanishi wa Pakistan walilithibitisha.
Lakini
tayari makubaliano ya amani yanaonyesha kuyumba.
Israel
imeanzisha wimbi kubwa la mashambulizi nchini Lebanon, na kuua watu wasiopungua
182.
Waziri Mkuu
wa Israel Benjamin Netanyahu ameelezea mashambulizi hayo kama "pigo kubwa
zaidi" kwa Hezbollah tangu kuanza kwa vita, akisema Israel itaanza tena
kupigana na Iran kukiwa na haja ya "kufanya hivyo".
Wakati huo
huo, Iran imesema ikiwa mashambulizi nchini Lebanon hayatakoma mara moja huenda
yakachochea "hatua kuchukuliwa".
Siku ya
Jumamosi, Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance atashiriki katika mazungumzo na
Iran mjini Islamabad, Pakistan.
Jambo la
msingi litakuwa usafiri wa meli katika Mlango-Bahari wa Hormuz, njia ya
baharini katika Ghuba ya Uajemi ambayo ni muhimu kwa usambazaji wa mafuta duniani.
Iran imesema
meli "zitalengwa na kuharibiwa" ikiwa zitapita bila ruhusa.
Spika wa
bunge la Iran pia anasema mambo matatu ya kusitisha mapigano kwenye mapendekezo
yenye masuala 10 "yamekiukwa waziwazi", huku Vance akisema kila mara
kuna "mapungufu" katika makubaliano kama hayo.
Hezbollah yasema imeshambulia kaskazini mwa Israel
Vile vile, Hezbollah imesema imerusha makombora kaskazini mwa Israeli.
Wanamgambo hao
wanaoungwa mkono na Iran wanasema ilikuwa ni kujibu ukiukwaji wa mapigano,
katika taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
Pia
wametishia kuendelea na mashambulizi hadi "uchokozi wa Israel na
Marekani" dhidi ya Lebanon utakapokoma.
Bado kuna kutokubaliana kuhusu kama nchi hiyo imejumuishwa katika usitishaji mapigano.