Marekani yawaonya raia wake kuhusu kusafiri kwenda Nigeria kwa sababu za usalama

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Marekani imewataka raia wake kufikiria upya kuhusu kusafiri kwenda Nigeria, ikitaja hatari kama vile ugaidi, machafuko ya kiraia na utekaji nyara.
Tahadhari ya usafiri ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani iliyotolewa Jumatano iliongeza kuwa majimbo fulani ya Nigeria ambayo yana hatari kubwa yamewekwa chini ya tahadhari kali zaidi linaloshauri kutoenda kabisa katika maeneo hayo.
Washington pia imeidhinisha kuondoka kwa wafanyakazi wake “wasio wa dharura” pamoja na familia zao kutoka ubalozi wa Marekani mjini Abuja, kufuatia kile inachokiita “kuzorota kwa hali ya usalama” kote nchini.
Tahadhari hiyo inatolewa wakati kukiwa na ongezeko jipya la mashambulizi katika baadhi ya maeneo ya nchi, licha ya ushirikiano unaokua wa kiusalama kati ya mataifa hayo mawili.
Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Washington imekuwa ikishirikiana na Abuja katika kupambana na ugaidi, usalama wa baharini, kubadilishana taarifa za kijasusi na mafunzo ya kijeshi.
Ushirikiano wa hivi karibuni umejumuisha msaada wa ufuatiliaji na uchunguzi wa anga, pamoja na matumizi ya ndege na helikopta zilizotolewa na Marekani na kutumiwa na vikosi vya Nigeria dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu na makundi yenye silaha.
Uamuzi wa kupunguza wafanyakazi wa ubalozi unaonesha pengo lililopo kati ya ushirikiano wa kimkakati wa kijeshi na hali halisi ya ukosefu wa usalama wa kila siku unaowakabili raia katika maeneo mengi ya nchi.
Katika tahadhari hiyo ya usafiri, raia wa Marekani walionywa kuwa mashambulizi yanaweza kutokea bila onyo katika maeneo ya umma ikiwemo masoko, hoteli, maeneo ya ibada, shule na vituo vya usafiri.
Unaweza kusoma;













