Akihutubia taifa siku ya Ijumaa kutoka Ikulu, alibainisha
kuwa deni la umma linaendelea kuwa sehemu kubwa ya ushiriki na mazungumzo
nchini Kenya.
"Leo nimeteua kikosi kazi huru cha kufanya ukaguzi wa
kina juu ya deni la umma na kuripoti kwetu katika miezi mitatu ijayo,"
alisema.
Rais Ruto
amesema idadi ya washauri serikalini itapunguzwa kwa asilimia 50.
"Idadi ya
washauri katika serikali itapunguzwa kwa asilimia 50 ndani ya utumishi wa umma
kwa haraka," alisema.
Rais wa
Kenya William Rito amesema bajeti zilizokuwa
zimetengewa ofisi ya Mke wa Rais na Naibu Mke wa Rais, na Mke wa Waziri Kiongozi zimeondolewa.
Amesema pia kwamba kwamba mpango
wa kuwaajiri maafisa wakuu wa utawala umesitishwa na idade ya washauri wa
serikali imepunguzwa kwa 50%, huku akithangaza kukatwa kwa 50% ya bajeti ya
ukarabati wa majengo ya serikali.
Baada ya malalamiko kuhusu ziara
za viongozi wa kiserikali na bunge nje ya nchi kutoka kwa umma wa Wakenya, Rais
Ruto ametangaza kuwaziara zisizo muhimu za viongozi zimesitishwa.
Katika hotuba hiyo Bw Ruto ametangaza kuwa
utoaji wa michango ya pesa za misaada kwa
viongozi wa serikali al maarufu Harambee umesimamishwa na badala yake serikali
itaweka mfumo wa utoaji wa misaada hiyo.
Amesema mabadiliko haya yanalenga kuboresha
huduma za serikali kwa umma na kuhakikisha wananchi wanapata huduma kamili
wanazohitaji kutoka kwa serikali.
Haya
yanajiri huku Rais William Ruto akitoa mwaliko wa
mazungumzo yaliyopewa jina la "Engage" mtandaoni kupitia X Space kati
yake na vijana, wengi wao "Gen Z," ambao wamekuwa wakiandamana
kupinga nyongeza ya ushuru tangu tarehe 18 Juni.
Maandamano hayo ambayo yamegeuka na kuwa maandamano ya kuipinga serikali
kutokana na masuala ambayo hayajashughulikiwa, yamesababisha vifo vya zaidi ya
watu 40, huku mamia wakijeruhiwa au kukamatwa.