Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mpango wa Israel wa 'kutwaa' Mji wa Gaza ni njia bora ya kumaliza vita na kuwashinda Hamas, Netanyahu asema.
Mkutano wa dharura wa Umoja wa Mataifa umeitishwa kujadili mpango wa Netanyahu wa kupanua vita huko Gaza, huku Israeli ikipinga vikali ukosoaji wa kimataifa.
Muhtasari
- Rais Samia Suluhu Hassan: 'Spika Ndugai ni nguzo muhimu ya Taifa'
- Padri aachwa na 'jeraha kubwa la kichwa' baada ya kushambuliwa
- Kenya yavunja msururu wa ushindi wa Morocco katika michuano ya CHAN
- Mpango wa Israel wa 'kutwaa' Mji wa Gaza ni njia bora ya kumaliza vita na kuwashinda Hamas, Netanyahu ase
- CHAN 2024: Kenya ya funga 1-0 dhidi ya Morocco
- Je, Kenya 'itatoboa' dhidi ya Morocco kufuzu robo fainali ya CHAN 2024?
- Mohamed Salah ahoji Uefa kuhusu kifo cha 'Mpalestina Pele'
- Washirika wa Ukraine wa Ulaya wasema mazungumzo ya amani sharti yajumuishe serikali ya Kyv
- Takriban watu 500 walikamatwa katika maandamano ya London kupinga marufuku ya kundi linalounga mkono Palestina
- Miamba ya Mars iliyopatikana Niger inauzwa mamilioni New York – Niger yahoji
- "Tutakufuata": Waandamanaji Tel Aviv wamwambia Netanyahu kuhusu mpango wa kuidhibiti Gaza
Moja kwa moja
Na Dinah Gahamanyi
Rais Samia Suluhu Hassan: ‘Spika Ndugai ni nguzo muhimu ya Taifa’
Rais wa Jamuhuri ya Tanzania Samia Suluhu Hassan amemuomboleza aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania Job Yustino Ndugai kama kiongozi shupavu aliyeacha alama isiyofutika katika historia ya Taifa.
Akizungumza katika shughuli ya kuuaga mwili wa Ndugai leo kwenye majengo ya Bunge, jijini Dodoma, Rais Samia alisema kwamba,’ Tumempoteza kiungo muhimu wa Taifa, Kiongozi aliyeaminiwa ndani na nje ya nchi na aliyejituma bila kuchoka katika kutumikia wananchi na kulinda maslahi ya Taifa,” alisema Rais Samia.
Ndugai alifariki wiki iliyopita baada ya kuugua kwa muda mfupi. Mwili wake unatarajiwa kupelekwa Wilayani Kingwa kwa ajili ya taratibu za mazishi baada ya siku nzima ya shughuli ya kumuaga katika viwanja vya majengo ya Bunge.
Spika mstaafu Ndugai kabla ya kifo chake aliibuka mshindi katika kura za maoni, kuwania ubunge katika jimbo la Kongwa mkoani Dodoma katikati mwa Tanzania, zilizopigwa hivi karibuni.
Ndugai alihudumu katika nafasi ya Spika wa Bunge la Tanzania kwa miaka 6, kuanzia mwishoni mwa 2015 hadi alipojiuzulu Januari, 2022.
Kabla ya hapo alihudumu kama Naibu Spika kati ya Novemba, 2010 Na Novemba, 2015.
Pamoja na kuwa mahiri kwa kuzifahamu vema kanuni za Bunge, aliwahi kukosolewa kwa kutoa kauli tata ikiwemo kusema alikuwa na uwezo wa kumzuia mbunge yeyote asizungumze kabisa bungeni.
Pia aliwahi kukosolewa kwa kusema aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, John Magufuli angelazimishwa kuendelea kugombea urais baada ya kumalizika vipindi viwili vinavyoruhusiwa kikatiba ”atake asitake”.
Pia unaweza kusoma:
Padri aachwa na 'jeraha kubwa la kichwa' baada ya kushambuliwa
Kasisi mmoja anatibiwa hospitalini kutokana na "jeraha kubwa la kichwa" baada ya kupigwa na chupa huko Downpatrick Uingereza.
Fr. John Murray alishambuliwa katika Kanisa la St Patrick kabla ya Misa yapata saa siku ya Jumapili.
Polisi walisema mwanamume mmoja aliingia kanisani kwenye Barabara ya St Patrick na kumpiga kasisi huyo kichwani kabla ya kuondoka.
Downpatrick Family Of Parishs walisema: "Padre Murray kwa sasa anapokea matibabu. Tunakushukuru kwa maombi na kheri zako."
Naibu Inspekta wa eneo McBurney alisema: "Hili lilikuwa shambulio la kushangaza na la kikatili kabisa na limemwacha kasisi na jeraha kubwa la kichwa."
Huduma ya Ambulance ya Ireland Kaskazini ilituma ambulensi ya dharura kwa tukio ambalo lilimpeleka kasisi huyo katika Hospitali ya Royal Victoria huko Belfast.
Polisi walisema kasisi huyo alisalia katika "hali mbaya".
Mwanachama wa bunge la SDLP South Down Colin McGrath alilaani shambulio hilo.
"Hili ni shambulio la aibu dhidi ya kasisi mmoja mzee ambalo limemuacha katika hali mbaya hospitalini", alisema Bw McGrath.
“Kwa hili kutokea kanisani ni jambo la kuchukiza sana na nimezungumza na wanajamii wengi ambao wameshtuka na kusikitishwa na jambo hili kutokea.
Kenya yavunja msururu wa ushindi wa Morocco katika michuano ya CHAN
Kenya imeandikisha historia ya kuvunja msururu wa ushindi wa Morrocco uliokuwepo tangu 2016.
Kenya sasa ipo kidedea kwenye jedwali ya kundi A ikiwa na pointi 7 ikifuatwa na Morrocco na Pointi tatu kwa pamoja na DRC huku Angola ikiwa na pointi moja na Zambia ikivuta mkia.
Japo Harambee stars imecheza kwa zaidi ya dakika 47 wakiwa na wachezaji 10, Morrocco ilishindwa kupenya safu ya ulinzi ya Kenya kwa muda huo wote, huku vijana wa Macarthy wakilinda bao moja lililotiwa kimyani katika dakika ya 42.
Kipa wa Kenya Omondi ndiye mchazaji bora wa mechi kwa juhudi zake kuzuia Morrocco kufunga japo walikuwa na nafasi nzuri za kufunga katika awamu ya pili.
Kocha MaCarthy alipata kadi ya njano katika dakika ya kwanza ya kipindi cha pili, Refa aliwaadhibu baadhi ya wachezaji wa Morrocco pia kwa kuwachezea vibaya wachezaji wa Kenya.
Kenya sasa inakodolea macho kufuzu kwa robo fainali na kujiunga na Tanzania katika awamu hiyo inayofuata raundi ya makundi, kama timu ya pili kutoka Afrika Mashariki.
Unaweza pia kusoma:
Mpango wa Israel wa 'kutwaa' Mji wa Gaza ni njia bora ya kumaliza vita na kuwashinda Hamas, Netanyahu asema
Waziri mkuu wa Israel sasa anawaambia waandishi wa habari kuwa Israel "haina chaguo" ila "kumaliza kazi" na "kuwashinda" Hamas.
Anasema kuwa 70-75% ya Gaza iko chini ya udhibiti wa kijeshi wa Israeli, lakini anasema kuwa Hamas ina ngome mbili zilizobaki. Moja ni Gaza City, anasema, na "kambi kuu" ni nyingine.
Siku ya Ijumaa, baraza la mawaziri la usalama la Israel liliagiza IDF "kusambaratisha" ngome hizo mbili.
Anasema hii ndiyo "njia bora" ya kumaliza vita. Anaongeza kuwa Israel itawaruhusu raia kwenda katika maeneo yaliyotengwa salama ambapo watakuwa na chakula cha kutosha, usalama na matibabu.
Hakuna mtu wa gaza isingenusurika Israel ingetekeleza 'sera ya njaa'
Netanyahu anasema Israel itawawezesha raia kuondoka kwa usalama katika maeneo ya mapigano hadi maeneo salama yaliyotengwa.
Watapewa chakula, maji na matibabu "kama tulivyofanya hapo awali", waziri mkuu anasema, akiongeza lengo la Israeli ni kuepusha janga la kibinadamu.
Anasema kuwa "mamia ya malori yameingia Gaza".
Iwapo Israel ingetekeleza "sera ya njaa", anasema, "hakuna mtu katika Gaza ambaye angesalimika baada ya miaka miwili ya vita." Anaongeza kuwa Israel imetuma na kupiga mamilioni ya maandishi na simu kuwaambia raia waondokane na madhara.
Unaweza pia kusoma:
Habari za hivi punde, CHAN 2024: Kenya yafunga 1-0 dhidi ya Morocco
Kenya imefunga 1-0 dhidi ya Morocco katika mechi inayoendelea katika Uwanja wa Kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi. Bao hilo lililotikisa wavu kunako dakika ya 42 na mshambuliaji Ryan Ogem na kuwaacha mashabiki wakiutikisa uwanja huo kwa kelele za shangwe.
Kwa sasa mechi imeingia katika kipindi cha mapumziko, lakini Kenya itakuwa na wachezaji 10 kwa mara nyingine baada ya mchezaji Chrispin Irambo kupata kadi nyekundu kwa kumtendea madhambi mchezaji wa Morroco katika dakika ya 45.
Mkufunzi wa Kenya amelalmikia hatua hiyo ambayo anasema imetolewa kimamosa, wala refa alitoa uamuzi huo baada ya kuangazia upya hali ya mchezo kwa mfumo wa VAR.
Morrocco ilipewa mkwaju wa moja kwa moja - free kick ambayo mlindalango wa Kenya aliinyaka, huku zilisalia dakika chache za ziada katika kipindi cha kwanza.
Kenya inajipata katika hali hii kwa mara ya pili baada ya kuondolewa mchezaji Nabwire katika dakika ya 21 kwenye mechi dhidi ya Angola siku ya Alhamisi.
Baada ya dakika 45 za wamu ya kwanza, Kenya ipo kifua mbele dhidi ya Morrocco huku vijana wa Nyumbani wakijitahidi sana kuwazuia wapinzani wao kutowafunga.
Aidha Harambee stars ilijaribu kuvunja safu ya ulinzi ya Morrocco zaidi ya mara mbili kupata bao, ila imekuwa vigumu. Hatimaye vijana walipenya na kupata nafasi ya kuweka mpira nyuma ya wavu wa Morrocco katika dakika ya 42 , bao lililofungwa na mchezaji Ryan Ogem.
Mshambulizi Boniface Muchiri amekuwa kiungo muhimu cha kikosi cha mkufunzi benny Macarthy katika juhudi za Kenya kujaribu kuweka bao kwenye wavu wa Morrocco na kuwachangamsha mashabiki ambao wamejitokeza kuwapa motisha vijana wa nyumbani.
Morrocco ilipata mshtuko baada ya mchezaji wao kupata jeraha na kuondolewa uwanjani kwa dakika kadhaa kupata matibbau kabla ya kurejea uwanjani.
Morrocco imekuwa na nafasi nyingi za kuishambulia wavu wa Kenya ila vijana wa nyumbani walijitahidi kuwazuia.
Unaweza pia kusoma:
Je, Kenya 'itatoboa' dhidi ya Morocco kufuzu robo fainali ya CHAN 2024?
Vijana wa Mkufunzi Benny Macarthy wameshuka uwanjani kwa sasa katika mechi ngumu zaidi ya KUNDI A kati ya Kenya na Morrocco ambapo vijana wa nyumbani watakuwa na kibarua kigumu kuwazuia Morrocco kutowafunga mabao.
Kocha wa Kenya, MaCarthy amewaambia waadishi wa Habari wkamba japo mlima uliopo mbele yao ni mkubwa, watajaribu kuukweya wakiwategemea mashabiki ambao wamejaza uwanja wa Moi – Kasarani hadi pomoni kuwapa motisha ya kufaynya vyema katika mechi hii ya tatu Kenya.
Kenya ili pata pigo katika mechi yake dhidi ya Angola wakati ambapo mchezaji Nabwire alipopewa kadi nyekundu kwa kumtendea madhambi mchezaji wa Angola katika dakika ya 21 na kuilazimu kikosi hicho kucheza wakiwa watu kumi kwa zaizi ya dakika 65.
Morrocco kwa upande wao wamekuwa na wakati mzuri baada ya kuiadhibu Angola katika mechi ya ufunguzi na kujipatia pointi tatu.
Kenya itakuwa inaomba dua kwamba matokeo bora ya Tanzania yatakuwa nao katika mechi ya Jumapili hii.
Taifa Stars kwa sasa wanaongoza kundi B kwa pointi 9 huku wakiwa tayari ndani ya
robo fainali, wakisubiri kumaliza mechi zilizosalia katika raundi ya makundi.
Uganda pia ilijipa nafasi nzuri ya kufuzu kwa robo fainali ilipoicharaza Guinea mabao matatu kwa nunge katika mechi yao wiki iliyopita. Kwa sasa Uganda Cranes iko nambari mbili kwenye jedwali chini ya Algeria iliyo na pointi nne.
Unaweza pia kusoma:
Mohamed Salah ahoji Uefa kuhusu kifo cha 'Mpalestina Pele'
Mhambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah, ametoa maoni yake kuhusu heshima aliyopewa mchezaji wa Palestina Suleiman al-Obeid na shirikisho la soka la Ulaya -Uefa kwenye mitandao ya kijamii, ambalo limeshindwa kushughulikia hali iliyosababisha kifo chake.
Siku ya Alhamisi, Chama cha Soka cha Palestina (PFA) kilisema Obeid aliuawa katika shambulizi la Israel alipokuwa akisubiri msaada wa kibinadamu kusini mwa Ukanda wa Gaza siku moja kabla ya kifo chake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41, aliyepewa jina la utani la "Pele wa soka la Palestina" na PFA, alifunga zaidi ya mabao 100 katika maisha yake ya soka, yakiwemo mawili katika mechi 24 za kimataifa.
Katika taarifa iliyotumwa kwenye tovuti ya X siku ya Ijumaa, Uefa ilisema: "Kwaheri Suleiman al-Obeid, 'Pele wa Palestina'.
"M,chezaji mwenye vipawa ambaye alitoa matumaini kwa watoto wengi, hata wakati wa siku za giza."
Jana, nyota wa Misri Salah, 33, alijibu: "Je, unaweza kutuambia jinsi alivyokufa, wapi, na kwa nini?"
BBC Sport imewasiliana na Uefa kwa maoni.
Unaweza pia kusoma:
Washirika wa Ukraine wa Ulaya wasema mazungumzo ya amani sharti yajumuishe serikali ya Kyv
Washirika wa Ukraine kutoka Ulaya wamesimama nyuma ya kiongozi wa Kyiv katika juhudi mpya za kuiunga mkono Ukraine, wakisisitiza kwamba majadiliano ya aina yeyote kuhusu amani na Urusi ni sharti yamjumuishe Rais Zelensky.
Taarifa ya pamoja iliyotolewa na viongozi wa Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Poland na Tume ya bara Ulaya imewasilishwa kabla ya mkutano uliopangwa kufanyika kati ya Marais Donald Trump wa Marekani na Vladimir Putin wa Urusi katika jimbo la Alaska nchini Marekani siku ya Ijumaa ijayo.
Kwa mujibu wa afisa wa Ikulu ya White House, Rais Trump yuko tayari kufanya mkutano wa pamoja kati ya mataifa matatu husika utakaowahusisha Rais Zelensky wa Ukraine, lakini kwa sasa mipango iliyopo inamuangazia Rais Putin tu aliyetoa ombi la kufanya kikao na Rais Trump.
Rais wa Ukraine amesema mara kadhaa kwamba maamuzi bila ya uwepo wa Kyiv ni kama kufanya , ‘maamuzi yasiyokuwa na uzito wowote.’
Awali, Rais Trump alikuwa amependekeza kwamba angeanza kwa kukutana na Rais Putin pekee, akiwaeleza waandishi wa habari kuwa alipanga ‘kuanza na Urusi.’ Lakini rais huyo wa Marekani amesema pia kwamba anaamini kuwa ‘Tuna na fusra kubwa ya kuandaa kikao cha pamoja tukiwahusisha Marais Putin na Zelensky.’
Haijabainika wazi iwapo Rais Putin atakubali kushiriki kwenye kikao hicho . Amekataa kushiriki katika vikao vilivyopendekezwa awali mara kadhaa huku viongozi hao wawili wa mataifa jirani yanayozozana wakishindwa kukutana ana kwa ana tangu Urusi ilipoanza mashambulizi ya kivita dhidi ya Ukraine miaka mitatu iliyopita.
Akizungumza katika kikao cha waandhishi siku ya Ijumaa, Rais Trump pia amependekeza kwamba, ‘Mataifa husika huenda yakakabidhiana udhibiti wa maeneo kadhaa wanayoyakalia na kuyadhibiti kwa sasa,’ kwa ajili ya kufanikisha maafikiano kati ya Moscow Kyiv – hali ambayo ilimfanya Zelensky kutoa tamko kali.
Shirika la habari la Marekani CBS limesema kwamba Ikulu ya White House inajaribu kuwashawishi washirika wa Ukraine barani Ulaya kukubaliana kwamba Urusi iwe na udhibiti wa eneo zima la Donbas liliopo mashariki mwa Ukraine na kuendelea kukalia jimbo la Crimea.
Viongozi wa Ulaya katika taarifa yao, wamesema kwamba , ‘mipaka ya kimataifa kama ilivyowekwa kwenye ramani haipaswi kubadilishwa kwa nguvu.’
Unaweza pia kusoma:
Takriban watu 500 walikamatwa katika maandamano ya London kupinga marufuku ya kundi linalounga mkono Palestina
Watu 474 walikamatwa wakati wa maandamano ya kuunga mkono kundi lililopigwa marufuku la Palestine Action katika uwanja wa Bunge wa Westminster, polisi wa London wamesema.
Waandamanaji kwa wakati mmoja waliinua mabango ya kujitengenezea nyumbani yenye maandishi: "Ninapinga mauaji ya halaiki. Ninaunga mkono Hatua ya Palestina."
Mnamo Julai, Palestine Action lilitangazwa kuwa shirika la kigaidi chini ya Sheria ya Ugaidi ya 2000 , na kufanya uanachama ndani yake au kusaidia shughuli zake kuwa kosa la jinai linaloadhibiwa kwa hadi kifungo cha miaka 14 jela.
Polisi walisema mtu yeyote anayeonyesha mabango ya kuunga mkono Palestine Action "tayari amekamatwa au yuko katika harakati za kukamatwa."
Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha polisi wakitembea kati ya waandamanaji wakiwa wameketi chini, wakiwakaribia watu, kuzungumza nao, na kisha kuwaongoza.
Waandamanaji waliotambuliwa wakati wa mchakato wa kushughulikiwa waliachiliwa kwa dhamana kwa masharti kwamba wasishiriki katika maandamano zaidi ya kuunga mkono Hatua ya Palestina. Wale waliokataa kutoa taarifa za kibinafsi au ambao utambulisho wao haukuweza kuthibitishwa waliwekwa kizuizini.
Kulingana na polisi, kulikuwa na watu wapatao 500-600 kwenye uwanja huo, lakini sio wote walikuwa wameshikilia ishara, na baadhi yao walikuwa waandishi wa habari au walikuja kutazama tu.
Unaweza pia kusoma:
Mwamba wa Mars uliopatikana Niger unauzwa mamilioni New York – Niger yalalamika
"Aibu! Ni aibu!" Profesa Paul Sereno anasema kwa njia ya simu kutoka Chicago.
Hafanyi jitihada zozote za kuficha hasira yake kwamba kimondo adimu kutoka Mars kilichogunduliwa miaka miwili iliyopita katika taifa la Afrika Magharibi la Niger kiliishia kupigwa mnada mjini New York mwezi uliopita kwa mnunuzi ambaye hakutajwa jina.
Mtaalamu huyo wa elimu ya kale, ambaye ana uhusiano wa karibu na nchi, anaamini kwamba inapaswa kurejea Niger.
Sehemu hii ya ni ya kipande cha mwamba wa mamilioni ya miaka ya Sayari Nyekundu, kubwa zaidi kuwahi kupatikana Duniani, iliuzwa kwa $4.3m (£3.2m) huko Sotheby's
Lakini haijafahamika kama pesa zozote kati ya hizi zilienda Niger.
Vipande vya miamba hii ambavyo vimefika duniani kwa muda mrefu - baadhi huishia kuwa vitu vya kidini, vingine kama vitu vya maonyesho. Hivi karibuni , miamba ya aina hii mingi imekuwa kama mada ya utafiti wa kisayansi.
Biashara ya vimondo imelinganishwa na soko la sanaa, huku urembo na nadra kuathiri bei.
Soma zaidi:
"Tutakufuata": Waandamanaji Tel Aviv wamwambia Netanyahu kuhusu mpango wa kuidhibiti Gaza
Maelfu ya waandamanaji waliingia katika mitaa ya Tel Aviv Jumamosi jioni kupinga mpango wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa kuzidisha vita vya Gaza vilivyodumu kwa takriban miaka miwili, wakitaka kusitishwa mara moja kwa kampeni na kuachiliwa kwa mateka.
Waandamanaji walipeperusha mabango na kushikilia picha za mateka hao ambao bado wanashikiliwa huko Gaza, wakiitaka serikali kuwaachilia huru.
Idadi ya washiriki ilikadiriwa kuwa makumi kwa maelfu, wakati Jukwaa la Familia za Watekaji lilisema hadi watu 100,000 walishiriki katika maandamano hayo, kulingana na Agence France-Presse.
Shirika hilo pia limemnukuu Shahar Mor-Zehero, jamaa wa mateka waliouawa akisema, "Tutahitimisha kwa ujumbe wa moja kwa moja kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu: Ikiwa utavamia sehemu za Gaza na mateka wakauawa, tutawafuata katika viwanja vya miji, wakati wa kampeni za uchaguzi, na wakati wote na kila mahali."
Ingawa mamlaka haijatoa makadirio rasmi ya idadi ya washiriki, inaonekana kuwa kubwa zaidi kuliko umati wa watu walioshiriki katika maandamano ya awali ya kupinga vita.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel ilitangaza siku ya Ijumaa kwamba Baraza la Mawaziri la Usalama, ambalo ni kundi dogo la mawaziri wakuu, limeamua kuuteka mji wa Gaza, na kupanua wigo wa operesheni za kijeshi katika eneo lililoharibiwa la Palestina, licha ya upinzani mkubwa wa umma na onyo la kijeshi kwamba hatua hiyo inaweza kuwahatarisha mateka.
Unaweza pia kusoma:
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara ya Jumapili ya tarehe 10.08.2025