Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Israel yashambulia kaskazini mwa Gaza huku zaidi ya 80 wakiuawa - Hamas

Israel inasema inakagua ripoti za majeruhi lakini ilishutumu maafisa wa Hamas kwa kushirikisha takwimu "zilizotiliwa chumvi".

Muhtasari

  • Wanajeshi watatu wameuawa katika shambulizi la Israel - Jeshi la Lebanon
  • 'Hakuna mahali salama Gaza' - afisa wa Umoja wa Mataifa
  • Nyota wa Inter Miami Messi kucheza katika kombe la dunia la Fifa
  • Umoja wa Mataifa yataka njia zaidi za kuingia Gaza kufunguliwa
  • Jeshi la Israel lashambulia makao makuu ya ujajusi ya Hezbollah - IDF
  • Kenya: Sherehe za Mashujaa bila Naibu Rais
  • Mfalme Charles aanza ziara yake ya Australia kwa kuhudhuria misa kanisani
  • Watu saba wauwa baada ya pantoni kujaa kupita kiasi kwenye sherehe
  • Mfalme Charles aanza ziara yake ya Australia kwa kuhudhuria misa kanisani
  • Watu saba wauwa baada ya pantoni kujaa kupita kiasi kwenye sherehe
  • Watu 73 wauawa katika shambulizi la Israel kaskazini mwa Gaza - mamlaka

Moja kwa moja

Na Asha Juma

  1. Golikipa wa West Ham, 15, afariki baada ya kuugua saratani

    Golikipa wa shule ya michezo ya West Ham amefariki akiwa na umri wa miaka 15 baada ya kuugua saratani.

    Oscar Fairs kutoka Benfleet, Essex, aligundulika kuwa na aina ya uvimbe usio wa kawaida kwenye ubongo wenye ukubwa wa 7cm (2.8in) unaofahamika kama ependynoma, mwezi Agosti 2023.

    Alifanyiwa upasuaji mara saba, raundi moja ya matibabu ya mionzi yanayofahamika kama chemotheraphy na radiotherapy, lakini aliambiwa kuwa kitu pekee anachoweza kufanya ni kupata matibabu ya kupunguza maumivu na msongo wa mawazo unaotokana na kuugua maradhi makubwa.

    Mkurugenzi wa klabu hiyo ya michezo Mark Noble amesema kuwa “alikuwa na maisha mazuri kwa siku za baadaye, na inasikitisha sana kuwa ameondoka kwa familia na marafiki zake katika umri mdogo.”

    Salam za pole kutoka kwa vilabu vingi na wachezaji wengi wa mpira zimekuwa zikitolewa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwemo kipa wa Real Madrid Thibaut Courtois na nyota wa Liverpool aliyestaafu, Jamie Carragher.

    Ukurasa wa kusaidia familia kukusanya £100,000 kwaajili ya gharama za matibabu nchini Ufaransa umefunguliwa.

    Kulingana na familia yake, Wachezaji wa timu ya West Ham wamechangia £27,000, huku mwenyekiti wao David Sullivan akichangia £10,000 na mchezaji wa Arsenal na mchezaji wa zamani wa West Ham Declan Rice wakitoa £5,000.

    Ratiba zote za shule hiyo ya michezo za mwishoni mwa wiki zimeahirishwa ikiwa kama ishara ya heshima kwa marehemu.

  2. Marekani yasema uhusiano wake na Korea Kusini ni kama ‘chuma’

    Balozi wa Marekani nchini Korea Kusini ameandika kwenye ukurasa wake wa X kuwa amekutana na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo, baada ya hatua ya kumuondoa madarakani Rais Yoon.

    Philip Goldberg amesema “Kama kawaida, Marekani inaunga mkono Jamhuri ya Korea na hatua ya kidemokrasia na kikatiba ipo pamoja na raia wake.”

    “Waziri wa mambo ya nje Cho na mimi tumehakikisha kuwa uhusiano wetu utaendelea kuwa imara kama chuma. Ahadi zetu kuhusiana na amani kwenye rasi ya eneo hili zipo thabiti.”

    Korea Kusini ni mshirika muhimu wa Marekani katika eneo la Asia – nchi hizo mbili zinashirikiana kwa karibu sana hususan, kwenye masuala yanayo husiana na Korea Kaskazini.

    Pia unaweza kusoma:

  3. Mlipuko wa bomu waua watu watatu na kujeruhi wengi kwenye tamasha Thailand

    Takriban watu watatu wameuawa na wengi kujeruhiwa baada ya bomu kurushwa kwenye kundi la watu waliokusanyika katika tamasha nchini Thailand.

    Shambulio hilo lilitokea muda mfupi kabla ya saa sita usiku saa za eneo hilo, siku ya Ijumaa, katika tamasha la Red Cross Doi Loyfa, linalofanyika kila mwaka kwenye wilaya ya Umphang, Kaskazini mwa jimbo la Tak.

    Watuhumiwa wawili wanashikiliwa, lakini kulingana na vyombo vya habari nchini humo na shirika la habari la AP wakinukuu kile ambacho polisi wa Thai wamekisema, ni kuwa, hakuna mashtaka yoyote yaliyotolewa hadi sasa.

    Polisi wanasema karibu watu 48 wamejeruhiwa, ambao sita kati yao wamejeruhiwa vibaya sana.

    Polisi walipewa taarifa majira ya 23:30PM usiku saa za Thailand siku ya Ijumaa.

    Timu ya uokoaji ya Umphang imesema kuwa bomu lilirushwa na kutua mbele ya jukwaa lililokuwepo nje ambapo wahudhuriaji wa tamasha hilo walikuwa wakicheza densi.

    Waziri mkuu Paetongtarn Shinawatra ametoa salamu za pole kwa familia za wale walioathirika na tukio hilo kupitia mtandao wa kijamii wa X.

    Pia aliongeza kwa kusema ameagiza polisi na mashirika ya kiusalama kuchunguza chanzo cha mlipuko huo na kuwasaidia wale walioathirika na tukio hilo. Pia ameagiza kuwepo kwa idadi kubwa ya polisi kwenye matukio yote ya matamasha.

    Ripoti kadhaa zinaashiria kuwa mlipuko huo ulisababishwa na bomu lililotengenezwa nyumbani kwa kutumia vifaa ambavyo ni rahisi kupatikana.

    Pia unaweza kusoma:

  4. Mahakama ya katiba Korea Kusini yatarajia kukutana siku ya Jumatatu

    Vyombo vya Habari nchini Korea Kusini vimeripoti kuwa, Mahakama ya Kikatiba inatarajia kukutana siku ya Jumatatu kuzungumzia ratiba ya kusikilizwa kwa kesi ya kumuondoa Yoon madarakani.

    Mahakama pia itapanga tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo hadharani, licha ya kuwa haijulikani ikiwa Yoon mwenyewe atahudhuria.

    Kiongozi wa chama cha Yoon amekubali matokeo ya kura ya kumuondoa madarakani

    Kiongozi wa chama cha Yoon cha People’s Power, Han Dong-hoon, anasema anakubali matokeo ya leo na anayachukulia kwa umakini sana.

    Kabla ya wabunge kupiga kura ya kutaka kumuondoa Yoon madarakani, Han alijaribu kumuomba rais kufikiria kujiuzulu.

    Han amewaambia waandishi wa habari bungeni muda si mrefu kuwa, chama cha People’s Power “kitarekebisha makosa yaliyotokea na kulinda katiba na demokrasia.”

    Pia unaweza kusoma:

  5. Ghasia nchini Georgia zaongezeka huku aliyekuwa mchezaji soka akitarajiwa kuwa rais

    Mchezaji wa mpira wa miguu wa zamani kutoka timu ya mpira ya Manchester City, anatarajiwa kuapishwa kuwa rais siku ya Jumamosi na bunge la Georgia, lenye mgawanyiko mkubwa, baada ya siku 16 za maandamano yanayounga mkono umoja wa ulaya, EU, ambayo yamegubika miji ya nchi hiyo.

    Mikheil Kavelashvili, 53, ni mbunge wa zamani kutoka chama cha Georgian Dream ambacho kimeshutumiwa kwa kuwa na misimamo mikali na ndiye mgombea pekee wa nafasi hiyo.

    Waandamanaji walianza kukusanyika nje ya bunge Jumamosi asubuhi.

    Vyama vikuu vinne vya upinzani vimemkataa Kavelashvili na kususia bunge, wakisisitiza kuwa uchaguzi uliofanyika mwezi Oktoba 2024, ulikuwa wa hila.

    Rais anayeondoka madarakani ambaye anashirikiana kwa karibu na mataifa ya Magharibi, Salome Zourabichvili, ameshutumu kitendo cha Kavelashvili kuibuka mshindi na kudai kuwa kulikuwa na udanganyifu, na kusisitiza kuwa yeye ndiye anayeshikilia nafasi pekee ya Georgia inayofuata kanuni za demokrasia.

    Maandamano dhidi ya chama cha Georgian Dream yalianza mara tu baada ya uchaguzi wa Oktoba, lakini yaliibuka tena mnamo Novemba 28 wakati serikali ilipotangaza kuwa inasimamisha mazungumzo ya kujiunga na umoja wa ulaya, EU, hadi mwaka 2028.

    Pia unaweza kusoma:

  6. Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu ya leo. Kwaheri.

  7. Hezbollah yarusha mabomu ya roketi kuelekea kambi ya jeshi la Israel ya Filon

    Hezbollah inasema imeshambulia na mabomu kambi ya jeshi la Israel katika eneo la Rosh Pina, Kaskazini mwa Israel.

    Katika taarifa yake kupitia mtandao wa Telegram kundi hilo limesema, limerusha silaha aina ya roketi salvo katika kambi ya kijeshi kwenye majira ya 12:30 saa za Israel (10:30 BST).

    Shambulizi hilo linajiri baada ya vikosi vya ulinzi vya Israel (IDF) kusema awali kuwa ving’ora vililia katika eneo la juu la Galilaya na wakati huohuo silaha 30 za anga zilivuka zikitokea Lebanon.

    Baadhi ya silaha hizo zilikabiliwa na vikosi vya anga vya Israel huku zingine zikianguka chini.

    Soma pia:

  8. 'Ilihisi kama tetemeko la ardhi,' anasema mkazi wa kaskazini mwa Gaza

    Mtu anayeishi kaskazini mwa Gaza ameelezea wakati mashambulizi ya Israel yalipokumba kitongoji chake huko Beit Lahia kama walihisi "kama tetemeko la ardhi".

    "Tulikimbilia nje baada ya kusikia mayowe ya wanawake na watoto na tukagundua kuwa majirani zetu walikuwa wakilengwa na msururu wa mabomu," anasema Ahmed Al Hajeen.

    Hajeen amesema kitongoji hicho ni makazi ya "raia na familia zilizolazimika kuhama makazi yao", wengi ambao walikimbia "maeneo hatarishi" na walidhani wangekuwa salama huko.

    Anasema watu kadhaa ambao walikuwa wameuawa walitolewa kutoka chini ya vifusi, lakini wengi walikuwa "bado wamenasa".

    Soma zaidi:

  9. Wanajeshi watatu wameuawa katika shambulizi la Israel - Jeshi la Lebanon

    Jeshi la Lebanon linasema kuwa wanajeshi watatu wameuawa baada ya gari la kijeshi kushambuliwa na mashambulizi ya anga ya Israel huko Nabatieh, kusini mwa Lebanon.

    Shambulio hilo lilitokea kwenye barabara ya Ain Ebel-Hanin, inayounganisha kijiji cha mpakani cha Ain Ebel na mji wa karibu wa Hanin.

    Israel bado haijatoa maoni.

    Jeshi la Lebanon kihistoria limejiepusha na mapigano ya mpakani kati ya Israel na Hezbollah, lakini idadi kubwa ya wanajeshi wake wameuawa katika mashambulizi ya Israel tangu mapigano kati ya Israel na Hezbollah yalipoongezeka mwezi uliopita.

    IDF inasema makombora 160 yalirushwa kuelekea Israel kutoka Lebanon

    Wakati huo huo, Jeshi la Israel linasema takriban makombora 160 yamerushwa kutoka Lebanon hadi saa 15:00 saa za eneo.

    Hii ni pamoja na roketi 70, ambazo baadhi yake zilinaswa, ambazo Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema hapo awali zilirushwa Israel mwendo wa saa 11:00 kwa saa za eneo.

    Soma zaidi:

  10. 'Hakuna mahali salama Gaza' - afisa wa Umoja wa Mataifa

    Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa wa Mchakato wa Amani ya Mashariki ya Kati anasema "hakuna mahali salama Gaza".

    Katika taarifa, Tor Wennesland anaongeza "jinamizi huko Gaza linazidi kuongezeka" na vita katika eneo hilo "lazima vikome sasa".

    Kwenye shambulizi la jana usiku huko Beit Lahia, wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema kuwa takriban watu 87 waliuawa huku Wennesland ikisema hilo limefuatia wiki za "operesheni zilizoimarishwa".

    Idadi ya waliofariki Gaza yaongezeka hadi 42,603 - wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas

    Taarifa za hivi karibuni kutoka wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema watu 84 wameuawa na wengine 158 kujeruhiwa katika muda wa saa 24 zilizopita.

    Takriban Wapalestina 42,603 ​​wameuawa na wengine 99,795 kujeruhiwa, tangu Israel ilipoanza mashambulizi yake ya kijeshi huko Gaza, tarehe 7 Oktoba mwaka jana, kulingana na wizara ya afya.

    Tarehe 7 Oktoba, shambulio lililoongozwa na Hamas dhidi ya Israel lilisababisha takriban watu 1,200 kuuawa na 251 kuchukuliwa mateka.

    Takriban mateka 100 bado wanazuiliwa huko Gaza.

    Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema mapema wiki hii kwamba mapigano yataendelea hadi mateka waliosalia warejeshwe nyumbani.

    Soma zaidi:

  11. Nyota wa Inter Miami Messi kucheza katika kombe la dunia la Fifa

    Timu ya Inter Miami imechaguliwa kucheza katika michezo ya kombe la dunia la FIFA 2025.

    Mashindano hayo yanayojumuisha timu 32 yatafanyika nchini Marekani mwaka 2025 kuanzia Juni 15 hadi Julai 3.

    Hii ni pamoja na timu 12 kutoka Ulaya, sita kutoka Amerika ya Kusini, 12 kutoka Asia, Afrika na Amerika ya Kaskazini na nafasi mbili za mwisho zikienda kwa klabu moja kutoka Oceania na nyingine Marekani ambayo ni mwenyeji wa mashindano hayo.

    Inter Miami, ambayo nusu inamilikiwa na David Beckham, wametunukiwa nafasi hiyo baada ya klabu hiyo kushinda Ngao ya Wafuasi wa MLS - ambayo imepewa kwa klabu hiyo katika MLS na msimu bora wa michezo hiyo.

    Tangazo hilo lilikuja baada ya Lionel Messi kufunga magoli matatu na kuisaidia Inter Miami kuvunja rekodi ya pointi za msimu wa kawaida za MLS.

    Mechi zitachezwa katika viwanja nane nchini Marekani - ikiwa ni pamoja na Uwanja wa Hard Rock wa Inter Miami - huku fainali ikifanyika kwenye Uwanja wa MetLife huko New Jersey.

    Uamuzi wa Fifa wa kupanua shindano hilo umekosolewa na vilabu na wachezaji, hususan baada ya UEFA kupanua hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Ligi ya Europa kwa kujumuisha mechi mbili zaidi.

    Droo kamili ya Kombe la Dunia la Vilabu itafanywa mwezi Desemba 2024.

    Pia unaweza kusoma:

  12. Umoja wa Mataifa yataka njia zaidi za kuingia Gaza kufunguliwa

    Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kutaka njia zaidi za misaada kufunguliwa kuelekea Gaza, ukisema kuwa hauwezi kuendesha shughuli zake za kutoa misaada ya kibinadamu "kwa kiwango kinachohitajika".

    "Hatuwezi kuendesha operesheni za kutoa misaada ya kibinadamu kwa kiwango kinachohitajika tukiwa na sehemu chache tu za kuvuka mpaka zilizo mbovu na zisizowezwa kufikika vizuri," inasema Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) katika eneo la Palestina linalomilikiwa kimabavu.

    “Msaada unakuwa umetolewa pale tu unapowafikia watu wanaouhitaji, wanapouhitaji.”

    Awali Israel imesema kuwa inalenga maeneo ya Hamas katika eneo la kaskazini na sio kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia.

    Kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas, takriban watu 87 wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel, kaskazini mwa Gaza.

    Wizara hiyo ya afya pia imesema takriban watu 87 wameuawa na zaidi ya watu 40 wamejeruhiwa katika shambulizi la Israel ndani ya Beit Lahia.

    Katika taarifa za hivi karibuni, wizara hiyo imeongeza kuwa kuna idadi kubwa ya waathiriwa ambao bado wapo chini ya vifusi, na wafanyakazi wa kutoa huduma ya afya hawawezi kuwafikia.

    Mamlaka zinazoendeshwa na Hamas jana usiku zilisema takriban watu 73 wameuawa katika shambulio hilo. Israel ilisema inakagua ripoti za waliofariki lakini inaamini kuwa takwimu zilizochapishwa na mamlaka ya Hamas "zimetiwa chumvi" na hazilingani na taarifa zinazoshikiliwa na jeshi lake.

    Soma pia:

  13. Jeshi la Israel lashambulia makao makuu ya ujajusi ya Hezbollah - IDF

    Jeshi la Israel limesema limefanya shambulizi kwenye makao makuu ya kijasusi ya Hezbollah katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.

    "Mapema asubuhi ya leo, IAF (kikosi cha anga cha Israel) kilifanya shambulizi kwenye kituo kikuu cha kijasusi cha Hezbollah na eneo la kutengeneza silaha lililokuwa chini ya ardhi huko Beirut," jeshi lilisema katika taarifa yake.

    Pia limeongeza kuwa hatua kadhaa zilichukuliwa ili "kupunguza uwezekano wa kuuawa kwa raia", ikiwemo "kutoa onyo mapema kwa wakaazi".

    Jeshi la Israel linasema kikosi chake cha anga kimemuua Al-Haj Abbas Salama, ambaye wanasema ni kamanda mkuu wa Hezbollah katika mstari wa mbele wa vita kwenye eneo la kusini, pamoja na Rada Abbas Awada na Ahmad Ali Hussein.

    Jeshi hilo pia linasema Awada alikuwa mtaalamu mkuu wa mawasiliano wa Hezbollah na Hussein aliwahi kuwa mkuu wa kitengo cha kutengeneza silaha.

    Kufikia sasa Hezbollah haijasema chochote kuhusu mashambulizi hayo.

    Picha za hivi karibuni kutoka pembezoni mwa mji kusini mwa Beirut, zimekuwa zikionesha moshi ukiendelea kufuka kwenye majengo ya makaazi ya watu baada ya shambulizi la anga la Israel katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.

    Soma pia:

  14. Kenya: Sherehe za Mashujaa bila Naibu Rais

    Rais William Ruto wa Kenya ameongoza sherehe za Mashujaa za Oktoba 20, 2024 katika kaunti ya Kwale.

    Hata hivyo, sherehe hizo zilikuwa tofauti kidogo kwasababu hakukuwa na naibu rais kama ilivyozoeleka.

    Hili lilitokana na kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa Naibu wake Rigathi Gachagua huku mahakama ikizuia uteuzi wa mrithi wake Profesa Kithure Kindiki.

    Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi ndiye aliyemualika Rais kuhutubia nchi.

    Miongoni mwa waliokuwepo kwenye sherehe hizo ni pamoja na Naibu Rais Mteule Kithure Kindiki.

    Rais amezungumzia mengi katika hotuba yake ikiwa ni pamoja na kugusia changamoto katika uhamaji kutoka mfumo wa Afya wa Jamii wa NHIF hadi SHA.

    “Ninatoa wito kwa Wakenya wote kuwa na imani na subira kidogo. Katika kipindi cha wiki chache, SHA itakuwa ikituhudumia ipasavyo na kutimiza ndoto ya Huduma ya Afya kwa Wote,” Rais alisema.

    Wakenya takriban 142 watatunukiwa tuzo za shujaa.

    Soma zaidi:

  15. Mfalme Charles aanza ziara yake ya Australia kwa kuhudhuria misa kanisani

    Mfalme Charles na Malkia Camilla waliungana na waumini wa kanisa mjini Sydney katika misa ya Jumapili, kwenye siku yao ya kwanza ya shughuli watakazozifanya katika ziara yao nchini Australia.

    Hii ni safari ya kwanza ya mfalme kutembelea Australia tangu awe kiongozi wa nchi hiyo mwezi Septemba 2022 na ni moja ya safari kubwa alizozifanya mfalme tangu aanze matibabu ya saratani mwezi Februari 2024.

    Ziara yao ya siku sita katika nchi hiyo ya Jumuiya ya Madola itahusisha kukutana na viongozi wa kisiasa na jumuiya, na kusherehekea watu wa taifa hilo, utamaduni na historia.

    Walijumuika na waumini wa Kanisa la Anglikana la St Thomas' kaskazini mwa Sydney kwa ajili ya misa, iliyoongozwa na askofu mkuu wa jiji hilo, Kanishka Raffel.

    Wanandoa hao wa kifalme walikutana na umati wa watu waliokuwa na shauku kubwa kuwaona, ambao wengi wao walipanga foleni tangu asubuhi na baadaye kuruhusiwa kuingia kwenye ua wa kanisa ili kuzungumza na wanandoa wa kifalme baada ya ibada.

    Kwa wengi ilikuwa ni kutoa salamu na nafasi ya kuwapa maua au kuchukua picha pamoja.

    Mfalme pia alikabidhi bunge la jimbo la New South Wales saa ya mchanga ya kioo katika kusherehekea kumbukumbu ya miaka 200 ya baraza lake la juu.

    Pia alitoa hotuba kwa wageni, ambapo alizungumzia "furaha yake kuu" ya kutembelea Australia kwa mara ya kwanza kama Mfalme, "na kuamsha upya upendo wa nchi hii na watu wake ambao nimeuthamini kwa muda mrefu".

    Picha ya Mfalme na Malkia Camilla ilitolewa siku ya Jumamosi, ambayo pia ni siku ya mapumziko kwa wanandoa hao, ikiwaonyesha baada ya kuwasili siku ya Ijumaa katika makaazi rasmi ya gavana mkuu wa Australia ambaye pia ni muwakilishi wa mfalme nchini humo yanayofahamika kama Admiralty House.

    Pia unaweza kusoma:

  16. Watu saba wauwa baada ya pantoni kujaa kupita kiasi kwenye sherehe

    Mamlaka za jimbo la Georgia nchini Marekani zinasema takriban watu saba wamefariki baada ya sehemu ya pantoni kuvunjika katika Kisiwa cha Sapelo ndani ya jimbo hilo siku ya Jumamosi.

    Idara ya maliasili ya Georgia, ambayo inasimamia gati, ilisema angalau watu 20 walitumbukia kwenye maji pale ubao wa kuingilia kwenye meli ulipoporomoka.

    Tukio hilo lilitokea takriban saa 16:30PM saa za Georgia (20:30PM GMT) kwenye gati inayofahamika kama Marsh Landing baada ya umati wa watu kukusanyika kwaajili ya sherehe ya kitamaduni.

    Watu wengi wamepelekwa hospitalini huku shughuli za utafutaji na uokoaji zikiendelea.

    Rais wa Marekani Joe Biden amesema yeye na mke wake wanasikitishwa kuhusu watu waliofariki na “wanawaombea wale waliojeruhiwa na mtu yoyote ambaye bado hajapatikana.”

    Kulingana na taarifa katika eneo hilo, Bado haijafahamika ni nini kilisababisha ajali hiyo kwenye njia iliyounganishwa kati ya ubao wa kuingilia kwenye pantoni na gati kwa upande wa nchi kavu.

    Pia unaweza kusoma:

  17. Watu 73 wauawa katika shambulizi la Israel kaskazini mwa Gaza - mamlaka

    Mashambulizi ya Israel yamesababisha vifo vya takriban watu 73 wakiwemo wanawake na watoto katika mji wa Beit Lahia kaskazini mwa Gaza, mamlaka inayoongozwa na Hamas imesema.

    Makumi ya wengine wamejeruhiwa na wengi bado wamenasa chini ya vifusi baada ya shambulio hilo la Jumamosi usiku, maafisa waliongeza.

    Israel ilisema inakagua ripoti za waliopoteza maisha lakini ikaongeza kuwa takwimu zilizochapishwa na mamlaka ya Hamas "zimetiliwa chumvi" na hazilingani na taarifa za jeshi lake.

    Mapigano pia yanaendelea kuripotiwa kusini mwa Lebanon na kusini mwa Beirut Jumapili asubuhi, ambapo moshi ulionekana ukipanda juu ya jiji hilo.

    Israel ilisema jeshi lake la anga lilishambulia "takriban maeneo 175 ya magaidi" huko Gaza na Lebanon katika siku iliyopita.

    Ofisi ya vyombo vya habari vya serikali inayoongozwa na Hamas ilisema shambulio la bomu huko Beit Lahia Jumamosi usiku lilikumba maeneo ya makazi "yaliyokuwa na watu wengi", na kwamba watu 73 wameuawa - idadi ambayo pia iliripotiwa na shirika la ulinzi wa raia wa Gaza.

    BBC haiwezi kuthibitisha takwimu hizo kwa uhuru.

    Kulingana na shirika la habari la Palestina Wafa, jumba zima la makazi liliharibiwa katika shambulizi hilo.

    Juhudi za uokoaji huko Beit Lahia kwa sasa zimetatizika kutokana na mawasiliano na huduma za intaneti kukatizwa katika eneo hilo, maafisa wa afya wa Gaza waliongeza.

    Mashambulizi ya hivi karibuni yamefanyika saa chache baada ya ripoti za milio ya risasi kutoka kwa wanajeshi wa Israel katika hospitali ya Indonesia mjini humo.

    Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) liliiambia BBC kwamba lilikuwa limeshambulia "eneo lengwa la ugaidi la Hamas" na "linafanya kila linalowezekana ili kuepuka kusababisha madhara kwa raia".

    Israel ilianza mashambulizi mapya ya kijeshi kaskazini mwa Gaza mwanzoni mwa mwezi Oktoba, ikisema inajaribu kuwazuia Hamas kujikusanya katika eneo hilo.

    Soma zaidi:

  18. Bila shaka hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 20/10/2024