Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tazama: Kijana akamatwa baada ya kumrushia Mfalme Charles mayai
Mwandamanaji alizuiliwa na polisi wakati umati wa watu ulikusanyika kwenye eneo la Micklegate, mlango wa kitamaduni wa kifalme wa jiji, kuwasalimu wanandoa hao.
Alisikika akipiga kelele "nchi hii ilijengwa kwa damu ya watumwa" huku akizuiliwa.
Polisi wa Yorkshire Kaskazini walisema mwanamume, 23, alikamatwa kwa tuhuma za kosa la amri ya umma na akabaki kizuizini.
Watu katika umati walianza kuimba "Mungu mwokoe Mfalme" na "aibu juu yako" kwa mandamanaji.Mwanamume mmoja amekamatwa baada ya mayai kurushwa kwa Mfalme na Malkia Consort wakati wa ziara ya York.
Tukio hilo lilitokea siku ya pili ya ziara rasmi ya kifalme huko Yorkshire, wakati ambapo Mfalme na Malkia Consort walisafiri hadi Doncaster.
Wanandoa hao wa kifalme walikuwa wakikaribishwa na viongozi wa jiji la York wakati mayai kadhaa yalipotupiwa huku muandamanaji akiwazomea wawili hao.
Charles aliendelea kupeana mikono na watu mashuhuri akiwemo Bwana Meya huku mayai yakiruka kuelekea kwake, akatulia kwa muda kidogo kuangalia maganda yaliyopasuka chini.
Mayai yaliwakosa Mfalme na Malkia Consort na wakatolewa.
Maafisa kadhaa walionekana wakimzuia mtu chini nyuma ya uzio wa muda uliowekwa kwa ajili ya ziara ya Mfalme.