Urusi na Ukraine: Sweden yagundua eneo jingine linalovuja la bomba la gesi la Nord Stream
Uswidi imegundua uvujaji mpya katika bomba kubwa la chini ya maji linalobeba gesi asilia ya Urusi kwenda EU. Huu ni uvujaji wa nne uliogunduliwa wiki hii.
"Uvujaji huu haukujulikana tangu mwanzo. [Mapovu ya gesi] hayakuonekana kwenye rada kwa sababu ni mdogo [kuliko uvujaji mwingine]. Walinzi wa Pwani waliugundua walipokuwa wakichunguza eneo hilo kwa meli na ndege," - linanukuu uchapishaji huo.
Mwanzoni mwa juma, Denmark na Uswidi ziliripoti kuvuja kwa gesi kwenye mabomba ya gesi ya Nord Stream 1 na 2.
Ulaya inaamini kuwa ni hujuma, Urusi imefutilia mbali madai kwamba inalipua mabomba yake yenyewe, na Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi ilisema milipuko hiyo ilitokea katika "kanda zinazodhibitiwa na ujasusi wa Marekani."









