Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Paul Pogba kuondoka Manchester United kwa uhamisho huru
Paul Pogba ataondoka Manchester United kwa uhamisho huru , mkataba wake utakapokwisha mwishoni mwa Juni, klabu hiyo imethibitisha.
Pogba, 29, alivunja rekodi ya dunia kwa dau la pauni milioni 89 alipojiunga tena na klabu hiyo akitokea Juventus mwaka 2016.
Alicheza mechi 27 katika msimu wa mwisho wa majeruhi katika kipindi chake cha pili.
"Ulikuwa mwisho wenye utulivu kwa United ambao ulileta nyakati nyingi nzuri kwa kila mtu," klabu cha Old Trafford ilisema katika taarifa.
"Magoli mengi mazuri, pasi za mabao na ustadi.
"Kwa kijana aliyejiunga na akademi akiwa na umri wa miaka 16 na kufanya zaidi ya mechi 200 za United na kubeba Kombe la Vijana, pamoja na mataji mawili ya ubingwa(Silverware) , ni jambo linalopaswa kupongezwa na kushangiliwa."
Pogba alijiunga na United kwa mara ya kwanza akitokea klabu ya Le Havre ya Ufaransa mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 16 na alikuwa sehemu ya timu ya vijana iliyoshinda Kombe la Vijana mwaka 2011.
Alicheza mechi saba pekee za wakubwa kabla ya mkataba wake kuisha Julai 2012 na akaondoka na kujiunga na Juventus.
Pogba alishinda tuzo nane kuu mjini Turin, ikiwa ni pamoja na mataji manne mfululizo ya Serie A, kabla ya kurejea tena Old Trafford kwa kuvunja rekodi.
Alishinda Kombe la EFL na Ligi ya Europa katika msimu wake wa kwanza katika klabu hiyo lakini walithibitisha mataji pekee ambayo angenyakua katika kipindi chake cha pili.
Kutoelewana na aliyekuwa meneja wa wakati huo Jose Mourinho kulimfanya apoteze unahodha mwaka wa 2018 na majeraha yaliyoathiri uchezaji wake.
Pogba alifunga mabao 39 katika mechi 233 katika muda wake wote wa kuitumikia klabu hiyo lakini mechi yake ya mwisho ya nyumbani dhidi ya Norwich City mwezi Aprili ilimshuhudia akidhihakiwa na wafuasi wake wakati alipobadilishwa.
'Kielelezo cha mawazo ya hovyo ya United'
Kwa maelezo yote katika taarifa yao, ukweli ni kwamba Manchester United ililipa pesa mara mbili kwa ajili ya Paul Pogba - ili kumpata kutoka Le Harve na kisha alipovunja rekodi ya dunia ya wakati huo kwa kuwagharimu £89m kumnunua kutoka Juventus.
Na hakuna wakati wowote Pogba ametoa kiwango cha juu cha uchezaji ambacho United ilihitaji kutoka kwake.
Kumekuwa na mambo mengi ya kusisimua, hasa mchango wake wa mabao mawili katika ushindi wa 3-2 baada kurejea Manchester City mnamo 2018 na pasi zake nne za mabao dhidi ya Leeds United siku ya ufunguzi wa msimu.
Lakini alikuwa wa muda mfupi sana ikilinganishwa na matokeo ya wachezaji kama Kevin de Bruyne huko Manchester City na hata Fabinho huko Liverpool, ushawishi wa Pogba ulikuwa wa matukio.
Ilionekana kana kwamba United walitumia pesa zote hizo kumnunua Pogba mara ya pili bila mpango wa jinsi ya kupata kilicho bora kutoka kwake. Ilimaanisha kwamba tabia yake ya nje ya uwanja ilianza kuvuma.
Alitofautiana vibaya na Jose Mourinho, ambaye alimvua unahodha kwa kukerwa kuondoka Old Trafford, na hakulipa imani ambayo Ole Gunnar Solskjaer aliendelea kuonyesha kwake.
Pogba popote atakapokwenda - na Juventus haijasitishwa kumsajili tena - inawezekana atakuwa na ushawishi mkubwa.