Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mshambuliaji wa Manchester United Paul Pogba asema timu yake inahitaji kufanya mabadiliko
Paul Pogba anasema Manchester United inahitaji "kubadilisha kitu fulani " baada ya kuchapwa bao 4-2 na Leicester, ikiwa ni mara ya pili wanashindwa katika mechi za Primia Ligi.
Manchester United wamechukua pointi moja kati ya pointi tisa ambazo walikuwa na uwezekano wa kuzipata, wakishuka hadi nafasi ya tano na hivyo kupoteza fursa ya uwezekano wa kupata taji.
Kumekuwa pia na michezo mingine ambapo walipata matokeo ambayo hayakutarajiwa katika msimu huu.
"Tumekuwa na aina hizi za mechi kwa muda mrefu na hatujawahi kupata tatizo. Tumekukubali kushindwa kirahisi na magoli ya kijinga ," Pogba aliiambia televisheni ya Sky Sports.
"Kama tunataka kushinda taji, hizi ndio mechi tunahitaji kushinda, hata kama ni ngumu sana.
"Tunafahamu kuwa mashabiki walitatusukuma na kutuwekea shinikizo na tunahitaji kuwa watu wazima zaidi, tucheze kwa uzoefu na majivuno-kwa njia nzuri-kwa kuchukua mpira na kucheza soka yetu.
"Tunahitaji kupata ufunguo kwa ajili ya mabadiliko haya kwasababu tulipaswa kushinda. Sijui kama ni mawazo ya wachezaji. Tunahitaji kubadili kitu fulani. Tunahitaji kutafuta mbinu za kiakili na kimkakati kushinda.Tunapaswa kuangalia kwa misingi ya kila mmoja wetu na kama timu kutatua hili."
Matokeo ya kukatisha tamaa ya hivi karibuni kwa Manchester United kulitia ukomo wa rekodi yao ya kutofungwa katika mechi 29 na miezi 20.
Timu hiyo ilishindwa kudhibiti kazi ya mchezo katikati ya uwanja na kukubali kushindwa kutokana na udhaifu wa safu yao ya ulinzi.
"Ni kama tuliwazawadia kusawazisha," alisema meneja wa United Ole Gunnar Solskjaer.
"Bao la pili lilikuwa lilitukatisha tamaa. Halafu likasawazishwa…na sekunde 10 baada ya kukubali kushindwa tena. Kwahiyo kumakinika katika nyakati kubwa, hilo ni jambo muhimu katika mechi ."
Goli la kwanza la Leicester lilitokana na mkwaju kutoka kwa Manchester United wenyewe kutoka kwenye eneo lao la penati.
Meneja wa Manchester United alionekana mwenye kupoteza muda wake wa kiufundi katika eneo lake huku Leicester, wakionekana kulisakata dimba ipasavyo na kuiyumbisha timu ambayo ilionekana kukosa mpangilio na uongozi, ikiwa na wasi wasi na kuonekana kukabiliwa na shinikizo mchana mzima.
Kama meneja Solskjaer atabeba lawama nyingi zaidi -lakini pia wachezaji maarufu waliomo ndani ya timu hii.