Chombo cha mapambo cha kale kilichotelekezwa chauzwa kwa pauni milioni 1.5

Chanzo cha picha, DREWEATTS
Nyumba moja ya mnada nchini Uingereza imeuza chombo cha mapambo 'adimu sana' cha karne ya 18 ambacho kilikuwa kimetelekezwa kwa miongo kadhaa jikoni kwa pauni 1,449,000.
Chombo hicho, kilichopakwa rangi ya buluu na kupambwa kwa dhahabu na fedha, kilitengenezwa ili kupamba jumba la kifalme la Mfalme Xianlong wa China.
Makadirio ya awali ya chombo hicho cha kale, kilichopambwa kwa michoro ya popo na ndege wa Karak, kilianza kuuzwa kwa kati ya pauni 100,000 hadi 150,000.
Chombo hicho kilikuwa mali ya daktari wa upasuaji ambaye alirithi kutoka kwa mwanawe, ambaye hakutambua thamani yake halisi.

Chanzo cha picha, DREWEATTS
Ni mtaalam wa mambo ya kale ambaye aligundua thamani na historia ya kweli ya chombo hicho, ilisema nyumba ya mnada ya Drewits Auctioneers huko Berkshire.
Chombo hicho cha kale kiliuzwa kwa mnunuzi wa kigeni kupitia simu. Bei ya mnada ilikuwa £1,200,000, huku mzabuni akilipa £1,449,000, ikijumuisha malipo ya ziada yaliyolipwa na mnunuzi.
"Tumefurahishwa na matokeo haya bora ," alisema Mark Newsted, afisa katika jumba la mnada alisema. "Tumeona nia kubwa kutoka China, Hong Kong, Marekani na Uingereza, ambayo imesababisha ushindani wa zabuni."
Chombo hicho kina herufi sita "tofauti" za Mtawala Xianlong (1736 - 1795) kwa chini

Chanzo cha picha, DREWEATTS
"Colbati ya bluu mara nyingi inajulikana kwa kutoa rangi ya bluu ikieleaea matumizi ya vyombo vya bluu katika kutoa matambiko kwenye Madhabahu ya Kifalme ya China," nyumba ya mnada ya Drewits Auctions ilisema.
Aliongeza: "mara chache tunapata vyombo vya bluu vyenye maumbo ya mapambo yaliyopakwa rangi ya fedha, kutokana na ugumu wa kutumia chuma cha fedha katika kuchora maumbo haya."
Nyumba hii ya mnada ilipendekeza kwamba ndege wa Karak na popo wanaonyesha maisha marefu na ustawi.













