Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vita vya Ukraine: Pentagon yatoa orodha kamili ya silaha zilizotolewa na Marekani kwa Ukraine
Pentagon imetoa orodha kamili ya silaha ambazo Marekani imezitoa kwa Ukraine
Rais wa Marekani Joe Biden amesaini waraka unaoelezea msaada wa kijeshi wa dola bilioni 40 kwa Ukraine. Waraka huo unasema kuwa dola bilioni 23.4 zitatengwa kwa ajili ya msaada wa kijeshi, na fedha nyingine zilizobakia zitatolewa kwa ajili ya misaada ya kibinadamu na kiuchumi.
Ifuatayo ni orodha ya silaha ambazo zitatolewa:
- Mwanajeshi wa Ukraine alifanya majaribio ya mifumo ya kuzuwia makombora
- Mifumo zaidi ya 1400 ya kuzuwia makombora ya anga
- Silaha zaidi ya 5500 za mifumo ya kuzuia makombora aina ya Javelin
- Mifumo mingine zaidi ya 14000 ya kudhibiti makombora ya anga
- Mifumo zaidi ya 700 ya kuongoza ndege zisizo na rubani.
- Pamoja na mifumo ya makombora 90,155 ya howitzers (silaha zinazopiga masafa marefu) na zaidi ya mizinga ya makombora 200,000.
- Magari ya mkakati yapatayo 72 yanayobeba makombora zaidi ya 155 aina ya howitzers
- Helikopta aina ya 16 Mi-17
- Mamia ya vifaru vyenye kasi kubwa vinavyoweza kusafiri kila mahali vinapohitajika vinavyofahamika kama SUVs 200 M113 ambavyo vinaweza kuwasafirisha wanajeshi na kuwakinga na mashambulizi;
- Zaidi ya bunduki ndogo 7000
- Zana za kujikinga na mashambulizi 75,000 pamoja na kofia (helmets)
- Mifumo ya 121 Phoenix Ghost Tactical, magari anga yanayofyatua makombora yanayoongozwa bila abiria ndani yake.
- Mifumo ya makombora ya anga aina ya Puma , inayoongoza manoari za kivita za walinzi w mwambao,
- Mifumo 17 kukabiliana na mifumo ya upelelezi ya anga.
- Silaha aina ya M18A1 Claymore inayoongozwa kwa kwa mtambo
- Kifaa cha kulipua na kuangamiza cha C-4 kwa ajili ya kuondoa vizuizi ili kuweza kupata mawasiliano yaliyolengwa
- Vifaa vinavyowezesha kuona usiku, kamera za kuona na kuchukua picha za masafa ya mbali, Na huduma za picha za setilaiti
- Vifaa vya kujikinga na kuzuia madhara ya kiafya ya vilipuzi
- Vifaa vya kikemikali, kibaiolojia, kifaa cha kujikinga na silaha za nyuklia ; vifaa vya tiba, vikiwemo vya huduma ya kwanza; Kifaa cha kufungua vifaa vya kielekroniki
Unaweza pia kusoma:
Pentagon tayari imekwishatangaza takriban milioni dola milioni 332 za msaada mpya wa kijeshi kwa Ukraine.
Tangu kuanza kwa vita vipya, Zelensky amekuwa akiwaomba viongozi wa mataifa ya magharibi kuongeza misaada, akisema kuwa anaweza kulishinda jeshi la Urusi iwapo jeshi lake litapewa ndege na magari mengine ya kijeshi.
Mwezi Aprili, Marekani ilithibitisha kwa mara ya kwanza kwamba ilitoa msaada wa makombora ya howitzers na mifumo ya upelelezei kwa Ukraine.
Balozi wa Urusi nchini Marekani anasema Moscow ilituma ujumbe wa kidiplomasia kwa kuitaka Marekani iache kutuma silaha kwa Ukraine.