Uhalifu wa kivita ni nini na je Putin anaweza kushtakiwa kwa uvamizi wa Ukraine?

Chanzo cha picha, Reuters
Picha za miili ya raia katika mitaa ya Bucha zimesababisha kulaaniwa kimataifa huku Urusi na vikosi vyake ikishutuma kwamba inafanya uhalifu wa kivita.
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu tayari imeanza kuchunguza iwapo uhalifu wa kivita unafanyika na Ukraine pia imeunda timu ya kukusanya ushahidi.
Uhalifu wa kivita ni nini?
Raia hawawezi kushambiliwa makusudi - au miundo mbinu ambayo ni muhimu kwa maisha.
Baadhi ya silaha zimepigwa marufuku kwa sababu zinasababisha mateso ya kiholela au ya kutisha- kama vile mabomu ya ardhini dhidi ya wafanyikazi na silaha za kemikali au za kibaolojia.
Wagonjwa na waliojeruhiwa lazima wahudumiwe -ikiwa ni pamoja na maaskari waliojeruhiwa, ambao wana haki kama wafungwa wa kivita.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJA:Urusi inajaribu kuficha uhalifu wa kivita - Zelensky
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Sheria zingine zinazuia mateso na mauaji ya halaiki- jaribio la makusudi la kuangamiza kundi maalum la watu.
Makosa makubwa wakati wa vita kama vile mauaji, ubakaji au mateso makubwa ya kikundi, yanajulikana kama "uhalifu dhidi ya ubinadamu".
Kumekuwa madai gani ya uhalifu wa kivita Ukraine?
Ukraine ilisema shambulizi la anga la Urusi dhidi ya wodi za uzazi na watoto huko Mariupol ni uhalifu wa kivita. Watu watatu akiwemo mtoto waliuawa na wafanyakazi 17 na wagonjwa walijeruhiwa.
Pia kumekuwa na ripoti kwamba wanajeshi wa Urusi wamewalenga raia wa Ukraine wanaotoroka.
Kuna ushahidi unaoongezeka kwamba mabomu ya vishada - silaha ambazo zinajitenga na kuwa mabomu mengi - yamepiga maeneo ya raia wa Kharkiv.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ukraine ambazo zimetia saini kupiga marufuku matumizi yao duniani kote, lakini matukio haya bado yanaweza kuchukuliwa kuwa uhalifu wa kivita.
Wizara ya Ulinzi ya Uingereza inasema Urusi imetumia vilipuzi vya thermobaric, ambavyo hutengeneza ombwe kubwa kwa kunyonya oksijeni. Vilipuzi hivi vya kuharibu havijapigwa marufuku - lakini matumizi yake ya kimakusudi karibu na raia yatavunja sheria za vita.
Wataalamu wengi wanahoji uvamizi wenyewe ni uhalifu chini ya dhana ya vita vikali - zaidi juu ya hiyo hapa chini.
Je, washukiwa wa uhalifu wa kivita wanafuatiliwaje?
Kila nchi ina wajibu wa kuchunguza tuhuma za uhalifu wa kivita.
Baadhi ya mataifa yanafanya zaidi ya mengine.
Nchini Uingereza, afisa polisi wa ngazi ya juu wamejitolea kusaidia kukusanya ushahidi wa uwezekano wa uhalifu wa kivita nchini Ukraine.

Chanzo cha picha, AFP
Je, watuhumiwa wa uhalifu wa kivita wanawezaje kufunguliwa mashtaka?
Kumekuwa na mfululizo wa mahakama za mara kuamua kesi moja kwa moja tangu Vita vya Pili vya Dunia - ikiwa ni pamoja na mahakama ya uhalifu wa kivita uliofanywa baada ya kuvunjika kwa Yugoslavia.
Chombo pia kiliundwa kuwashtaki baadhi ya waliohusika na mauaji ya halaiki ya Rwanda, ambapo Wahutu wenye msimamo mkali waliwaua watu 800,000 katika muda wa siku 100 mwaka 1994.
Leo hii, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai (ICC) na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) zina majukumu ya kuzingatia sheria za vita.
Mahakama ya Kimataifa ya Haki
ICJ inaamua mizozo kati ya mataifa, lakini haiwezi kuwashtaki watu binafsi. Ukraine imeawasilisha kesi dhidi ya Urusi kuhusu uvamizi huo.
Ikiwa ICJ itatoa uamuzi dhidi ya Urusi, jukumu la kutekeleza hukumu hiyo litakuwa la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC).
Lakini Urusi - moja ya wanachama watano wa kudumu wa UNSC - inaweza kupinga pendekezo lolote la kuichukulia hatua.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai(ICC)
ICC inachunguza na kuwashtaki wahalifu wa kivita ambao hawako mbele ya mahakama za mataifa mahususi.
Ni mrithi wa kisasa na wa kudumu wa Nuremberg, ambayo iliwashtaki viongozi muhimu zaidi wa Nazi waliokuwa kizuizini mnamo 1945.
Nuremberg ilisisitiza kanuni kwamba mataifa yanaweza kukubali kuunda mahakama maalum ya kudumisha sheria za kimataifa.
Je, ICC inaweza kuchnguza uhalifu nchini Ukraine?
Mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, wakili wa Uingereza Karim Khan QC, anasema kuna msingi wa kuridhisha kwamba uhalifu wa kivita umetekelezwa nchini Ukraine - na ina idhini ya mataifa 39 kuchunguza.
Wachunguzi wataangazia madai ya zamani na ya sasa - kuanzia mwaka 2013, kabla ya Urusi kunyakua Crimea kutoka Ukraine.
Iwapo kuna ushahidi dhidi ya watu binafsi, mwendesha mashtaka atawaomba majaji wa ICC kutoa hati za kuwakamata ili kuwafikisha mahakamani - ambayo itafanyika The Hague.
Hapa ndipo mapungufu ya kiutendaji juu ya mamlaka ya mahakama yanapoonekana.
Mahakama haina jeshi lake la polisi. Inategemea mataifa kuwakamata washukiwa.
Lakini Urusi si mwanachama wa mahakama hiyo - ilijiondoa mwaka wa 2016. Rais Putin hatampeleka mshukiwa yeyote.
Ikiwa mshukiwa ataenda nchi nyingine, anaweza kukamatwa - lakini hilo linatiliwa shaka kama linaweza kufanyika.
Je, Rais Putin au viongozi wengine wanaweza kufunguliwa mashtaka?

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni rahisi sana kuwatwika mzigo wa uhalifu wa kivita maskari wanaofanya hivyo, kuliko viongozi waliowaamuru wapige risasi.
Lakini ICC pia inaweza kushtaki kosa la "kuendesha vita vikali".
Huu ni uhalifu wa uvamizi au mzozo usio na sababu, zaidi ya hatua za kijeshi zinazokubalika katika kujilinda.
Tatizo liko hapa: Profesa Philippe Sands QC, mtaalam wa sheria za kimataifa katika Chuo Kikuu cha London, anasema ICC haiwezi kuwashtaki viongozi wa Urusi kwa kosa hili kwa sababu nchi hiyo si mwanachama wa mahakama hiyo.
Kinadharia, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaweza kuomba ICC kuchunguza kosa hili. Lakini tena, Urusi inaweza kupinga hili kama mmoja wa wanachama watano wa kudumu wa baraza hilo.
Kwa hivyo kuna njia nyingine yoyote ya kuwashtaki watu binafsi?
Ufanisi wa ICC - na jinsi sheria ya kimataifa inavyofanya kazi - inategemea sio tu mikataba, lakini pia utasi wa kisiasa na diplomasia.
Na Prof Sands na wataalam wengine wengi wanahoji kuwa kama Nuremberg, suluhisho lipo kwa mara nyingine tena katika diplomasia na makubaliano ya kimataifa.
Anatoa wito kwa viongozi duniani kuunda mahakama maalum ilikshtaki Urusi kwa kuvamia Ukraine.














