Mzozo wa Ukraine: Kwanini Biden ameamua kutopeleka jeshi Ukraine

Joe Biden alihutubia taifa akichukua tahadhari ya kutoweka hatarini maisha ya wanajeshi wa taifa hilo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Joe Biden alihutubia taifa akichukua tahadhari ya kutoweka hatarini maisha ya wanajeshi wa taifa hilo

Rais Wa Marekani Joe Biden ametumia mtaji mkubwa wa kidiplomasia katika kukabiliana na uchokozi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

Utawala wake bila kusita ulitangaza onyo juu ya uvamizi wa Urusi - ambao ulionekana kuwa sahihi.

Lakini Bwana Biden pia ameweka wazi kwamba Wamarekani hawako tayari kupigana, ingawa Warusi wao wako tayari. Zaidi ya hayo, ameamuru kutuma vikosi nchini Ukraine kuwaokoa raia wa Marekani, ikiwa itafika kwa hilo. Na kwa kweli ameondoa wanajeshi ambao walikuwa wakihudumu nchini humo kama washauri wa kijeshi na wachunguzi.

Kwa nini amechora mstari huu mwekundu katika mgogoro huu ulio ndani ya sera za kigeni za urais wake?

Hakuna maslahi ya usalama wa taifa

Kwanza kabisa, hakuna suala la kitisho cha usalama, kwa sababu Ukraine sio nchi jirani na Marekani. Hili haliko. Wala hii si kambi ya kijeshi ya Marekani. Haina akiba ya mafuta ya kimkakati, na sio mshirika mkubwa wa biashara.

Lakini kutokuwepo kwa maslahi ya kitaifa siku za nyuma hakujawazuia marais wa zamani kumwaga damu kwa niaba ya wengine. Mwaka 1995, Bill Clinton aliingilia kati kijeshi katika vita vilivyochangia kuanguka kwa Yugoslavia. Na mwaka 2011 Barack Obama alifanya vivyo hivyo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Libya, kwa kuegema misingi ya kibinadamu na haki za binadamu.

Wanajeshi wa marekani nchini Bosnia 1995

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanajeshi wa marekani nchini Bosnia 1995

Mwaka 1990 George H W Bush alihalalisha muungano wake wa kimataifa kuifurusha Iraq kutoka Kuwait kama mtetezi wa utawala wa sheria dhidi ya utawala wa msituni. Maafisa wa ngazi ya juu wa usalama wa taifa wa Biden wametumia lugha kama hiyo wakati wakielezea tishio la Urusi kwa misingi ya kimataifa ya amani na usalama. Lakini wamekuwa wakihubiri mapambano ya kiuchumi kwa njia ya vikwazo vikali kama jibu, sio operesheni za kijeshi.

Biden hatumii jeshi kuingilia mgogoro

Ni silica a muda mrefu. Aliunga mkono hatua za kijeshi za Marekani katika miaka ya 1990 ili kukabiliana na migogoro ya kikabila huko Balkan. Na alipiga kura kuunga mkono uvamizi wa Marekani nchini Iraq mwaka 2003. Lakini tangu wakati huo amekuwa na wasiwasi zaidi wa kutumia nguvu za kijeshi za Marekani.

Alipinga hatua ya Obama kuingilia kati mgogoro wa Libya pamoja na kuongeza wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan. Anatetea kwa uthabiti amri yake ya kuondoa vikosi vya Marekani kutoka Afghanistan mwaka jana licha ya machafuko yaliyoambatana nayo na janga la kibinadamu lililoachwa.

Na mwanadiplomasia wake wa ngazi ya juu Antony Blinken - "Whisperer" ambaye amebuni sera ya kigeni ya rais huyo kwa miaka 20 aliyofanya kazi nae - amefafanua kuwa usalama wa taifa utakuwa ni zaidi ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, kupambana na magonjwa ya kimataifa na kushindana na China kuliko kuingilia kijeshi.

Wamarekani hawataki vita pia

Kura ya maoni ya AP-NORC imeonyesha kwamba asilimia 72% walisema Marekani inapaswa kujihusisha kwa kiasi kidogo kwenye mzozo wa Urusi-Ukraine, au isijihusishe kabisa.

Wanacholenga ni masuala ya kiuchumi, hasa hasa kupanda kwa bei za bidhaa, kitu ambacho Biden anapaswa kukumbuka wakati huu uchaguzi wa katikati ya muhula unakaribia kufanyika.

Seneta mwingine wa sera za kigeni, kutoka chama cha Republican, Marco Rubio, amesema vita kati ya mataifa hayo mawili makubwa ya nyuklia duniani haitakuwa nzuri kwa mtu yeyote.

Hatari ya vita ya mataifa yenye nguvu kubwa

Biden hataki kuchochea "vita vya dunia" kwa kuhatarisha mapambano ya moja kwa moja kati ya wanajeshi wa Marekani na Urusi nchini Ukraine na amekuwa wazi kuhusu hilo.

"Sio kama tunakabiliana na kundi la kigaidi," rais Biden aliiambia NBC mapema mwezi huu. "Tunakabiliana na moja ya majeshi makubwa zaidi duniani. Ni hali ngumu sana, na mambo yanaweza kwenda haraka."

Hakuna uwajibikaji wa mkataba

Hakuna majukumu ya mkataba ya kuilazimisha Marekani kuchukua hatua yoyote ya hatari. Shambulio dhidi ya nchi yoyote ya NATO ni shambulio dhidi ya wote - ahadi ya msingi ya Kifungu cha 5 ambayo inaunganisha wanachama wote kulindana.

Lakini Ukraine sio mwanachama wa NATO, jambo ambalo limetajwa na Blinken kuelezea kwa nini Wamarekani hawatapigana kinyume na maadili ambayo wamekuwa wakiyahubiri.

Kuna dhana fulani hapa, kwamba mzozo unaoendelea unahusu madai ya Putin ya kutaka Ukraine kamwe isiruhusiwe kujiunga na muungano wa kijeshi, na NATO kuyakataa madai hayo.

Profesa wa Harvard na mwandishi wa sera za kigeni, Stephen Walt amedai kukataliwa kwa maelewano na Marekani na nchi nyingine za NATO haina maana kwa sababu hakuna utayari wa kuweka nguvu yoyote ya kijeshi nyuma yake.

Je, malengo yatafanikiwa?

Rais Biden amekuwa akituma wanajeshi Ulaya na kuwarejesha wale ambao tayari wapo, kuimarisha washirika wa NATO ambao wanapakana na Ukraine na Urusi.

Hii imedaiwa na utawala kama juhudi za kuwahakikishia jamhuri za zamani za Soviet wasiwasi juu ya lengo pana la Putin la kushinikiza NATO kuondoa vikosi kutoka kwenye meneo yake ya mashariki.

Bei ya mafuta imepanda

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bei ya mafuta imepanda

Lakini uvamizi wa Ukraine wiki hii umeongeza wasiwasi juu ya matarajio ya mgogoro mkubwa - ama shambulio la bahati mbaya au makusudi la Urusi.

Mwishowe kutaongezeka kwa kiasi kikubwa, na kusababisha Ibara ya 5 kujitolea kwa pamoja chini ya NATO. Lakini ama inaweza kuwaleta majeshi ya Marekani katika vita.

"Ikiwa ataingia katika nchi za NATO," Bwana Biden amesema, "tutahusika."