Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini tuko katika 'zama za visiwa vya bandia'
Katika historia, wanadamu wamejaribu kuunda ardhi kavu ndani ya maziwa, mito na bahari, ambayo wangeweza kuijaza. Lakini Karne ya 21 imeleta nia mpya - na labda mguso wa hisia - kwa juhudi hii.
Tunaishi katika "zama za visiwa", kulingana na mwanajiografia wa kijamii Alastair Bonnett wa Chuo Kikuu cha Newcastle, nchini Uingereza. "Visiwa vipya vinajengwa kwa wingi na kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa zamani."
Kizazi hiki kipya cha visiwa ni cha ujasiri, kikubwa zaidi - na kinaweza kuharibu zaidi - kuliko kitu chochote ambacho mababu zetu walijenga, anaandika Bonnett katika kitabu chake Elsewhere: Journey Into Our Age Of Islands.
Mwanajiografia huyo alizuru visiwa vilivyotengenezwa katika maeneo tofauti duniani, kuchunguza jinsi vilivyojengwa. Visiwa vya bandia vikubwa, vilivyoundwa kwa kumwaga mamilioni ya tani za mchanga ndani ya bahari. Viwanja vya "Frankenstein" vilivyofunikwa kwa zege, vilivyoundwa ili kuunganisha nguvu za kijeshi na kisiasa. Na mitambo mirefu ya mafuta yenye urefu wa mamia ya mita hadi chini ya bahari.
Ijapokuwa baadhi ya mijengo bandia imesombwa na maji , mchakato huo ulichukua mda. Mara nyingi, kuna viumbe wadogo chini ya maji yanayozunguka visiwa vilivyotengenezwa na mwanadamu. "Mara nyingi visiwa bandia ni maeneo yaliyokufa. Kujaribu kuwarejeshea uhai tena ni kazi ngumu," anaandika Bonnett. Katika maeneo kama vile Bahari ya China Kusini, "miamba iliyowahi kuwa safi na ambayo haijaguswa...imeharibiwa vibaya sana: imegawanywa kwa mraba na kukorogewa simiti".
Lakini hata hivyo, Bonnett alijikuta akivutiwa na ubunifu huu wa bandia, kujaribu na kuelewa jinsi visiwa hivyo zilivyojengwa, na kwa nini uamuzi wa kuzijenga ulifikiwa. Ikiwa zinakubalkai au la, zitasimulia vizazi vijavyo hadithi ya jinsi ubinadamu ulivyojiona katika miaka ya awali
Ili kuelewa jinsi umri wa visiwa unavyoonekana, angalia hizi piacha(hapo chini) upate mfano wa kuvutia zaidi na athari ya visiwa hivyo kote duniani - ukiangazia hali ilivyo katika Mataifa ya Ghuba, bahari ya Asia, na pwani ya Uingereza na Marekani.