Kwa nini tuko katika 'zama za visiwa vya bandia'

An aerial view of the Palm Jumeirah island in Dubai, UAE

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika historia, wanadamu wamejaribu kuunda ardhi kavu ndani ya maziwa, mito na bahari, ambayo wangeweza kuijaza. Lakini Karne ya 21 imeleta nia mpya - na labda mguso wa hisia - kwa juhudi hii.

Tunaishi katika "zama za visiwa", kulingana na mwanajiografia wa kijamii Alastair Bonnett wa Chuo Kikuu cha Newcastle, nchini Uingereza. "Visiwa vipya vinajengwa kwa wingi na kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa zamani."

Kizazi hiki kipya cha visiwa ni cha ujasiri, kikubwa zaidi - na kinaweza kuharibu zaidi - kuliko kitu chochote ambacho mababu zetu walijenga, anaandika Bonnett katika kitabu chake Elsewhere: Journey Into Our Age Of Islands.

Mwanajiografia huyo alizuru visiwa vilivyotengenezwa katika maeneo tofauti duniani, kuchunguza jinsi vilivyojengwa. Visiwa vya bandia vikubwa, vilivyoundwa kwa kumwaga mamilioni ya tani za mchanga ndani ya bahari. Viwanja vya "Frankenstein" vilivyofunikwa kwa zege, vilivyoundwa ili kuunganisha nguvu za kijeshi na kisiasa. Na mitambo mirefu ya mafuta yenye urefu wa mamia ya mita hadi chini ya bahari.

Ijapokuwa baadhi ya mijengo bandia imesombwa na maji , mchakato huo ulichukua mda. Mara nyingi, kuna viumbe wadogo chini ya maji yanayozunguka visiwa vilivyotengenezwa na mwanadamu. "Mara nyingi visiwa bandia ni maeneo yaliyokufa. Kujaribu kuwarejeshea uhai tena ni kazi ngumu," anaandika Bonnett. Katika maeneo kama vile Bahari ya China Kusini, "miamba iliyowahi kuwa safi na ambayo haijaguswa...imeharibiwa vibaya sana: imegawanywa kwa mraba na kukorogewa simiti".

Lakini hata hivyo, Bonnett alijikuta akivutiwa na ubunifu huu wa bandia, kujaribu na kuelewa jinsi visiwa hivyo zilivyojengwa, na kwa nini uamuzi wa kuzijenga ulifikiwa. Ikiwa zinakubalkai au la, zitasimulia vizazi vijavyo hadithi ya jinsi ubinadamu ulivyojiona katika miaka ya awali

Ili kuelewa jinsi umri wa visiwa unavyoonekana, angalia hizi piacha(hapo chini) upate mfano wa kuvutia zaidi na athari ya visiwa hivyo kote duniani - ukiangazia hali ilivyo katika Mataifa ya Ghuba, bahari ya Asia, na pwani ya Uingereza na Marekani.

Muonekano wa angani wa visiwa vya The World huko Dubai, UAE

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muonekano wa angani wa visiwa vya The World huko Dubai, UAE
A dredger pumps sand onto an artificial island in Dubai, UAE

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Meli katika Ghuba ya Uajemi ikisukuma tani za mchanga,ili kukuza kisiwa polepole
Muonekano wa kisiwa bandia kinachojulikana kama The Pearl kwenye ufuo wa Doha, Qatar

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kisiwa cha Pearl kilichotengenezwa na mwanadamu, huko Qatar, kina urefu wa karibu mita za mraba milioni 4 na kugharimu mabilioni ya ujenzi.
Kisiwa cha Swan huko Paris kilipiga picha kutoka Mnara wa Eiffel

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kisiwa cha Swan huko Paris kiliundwa mwanzoni mwa miaka ya 1800 ili kulinda madaraja ya jiji hilo
Muonekano wa angani wa Visiwa vya Venetian karibu na pwani ya Miami huko Florida, Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ilijengwa mwanzoni mwa Karne ya 20, mali hiyo kwenye Visiwa sita vya Venetian huko Miami iliuzwa wakati bado iko chini ya maji.
Picha ya setilaiti ya Kisiwa cha Palm na Kisiwa cha Hibiscus katika ufukwe wa Miami, Florida, Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Picha ya setilaiti ya Kisiwa cha Palm na Kisiwa cha Hibiscus katika ufukwe wa Miami, Florida, Marekani
Muonekano wa angani wa kisiwa cha Palm Jumeriya huko Dubai, UAE

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muonekano wa angani wa kisiwa cha Palm Jumeriya huko Dubai, UAE
Kisiwa cha Balboa huko California kilijengwa juu ya matope, na kwa miaka wakaazi walitatizika na miundombinu duni

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kisiwa cha Balboa huko California kilijengwa juu ya matope, na kwa miaka wakaazi walitatizika na miundombinu duni
Kisiwa cha Balboa sasa ni mojawapo ya masoko ya gharama kubwa ya mali isiyohamishika nchini Marekani, yenye watu 3,000.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kisiwa cha Balboa sasa ni mojawapo ya masoko ya gharama kubwa ya mali isiyohamishika nchini Marekani, yenye watu 3,000.
Picha ya angani ya mifumo miwili ya mafuta nje ya nchi, Cromarty Firth, Scotland, Uingereza

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Picha ya angani ya mifumo miwili ya mafuta nje ya nchi, Cromarty Firth, Scotland, Uingereza
Mitambo ya mafuta kwenye pwani ya Invergordon huko Scotland

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mitambo ya mafuta kwenye pwani ya Invergordon huko Scotland
A satellite image of Subi Reef, an artificial island being developed in the South China Sea.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mustakabali wa visiwa? Subi Reef ni kidokezo kimoja, sehemu ya mradi mkubwa wa Kichina wa kutengeneza visiwa katika Bahari ya China Kusini
Muonekano wa kisiwa bandia cha Qingdong-5 katika pwani ya Dongying katika mkoa wa Shandong mashariki mwa China

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Muonekano wa kisiwa bandia cha Qingdong-5 katika pwani ya Dongying katika mkoa wa Shandong mashariki mwa China