Hesabu hii mpya itachangia kupatikana kwa ndege ya MH370 iliyotoweka na watu 239 mwaka 2014?

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Kutoweka kwa ndege ya shirika la ndege la Malaysia iliyokuwa imewabeba abiria 239 na wahudumu ni moja ya mafumbo makubwa zaidi ya usafiri wa anga duniani.
Lakini mhandisi wa anga wa Uingereza ambaye ametumia zaidi ya mwaka mmoja akishughulikia janga hili, anaamini amegundua mahala ndege hiyo ilipoanguka.
Richard Godfrey anafikiri kuwa ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilianguka kwenye bahari ya Hindi kilomita 2,000 magharibi mwa Perth, Australia.
Ndege hiyio ilitoweka kutoka mitambo ya radar ikiwa safarini Machi 2014.
Godfrey aliiambia BBC kuwa ana matumaini "tunaweza kuwaelaza jamaa na kuujulisha umma na sekta ya safari za angani ni kipi haswa kilifanyikia ndege ya MH370 na jinsi ya kuzuia majanga kama hayo siku za usoni."
Alijumuisha data tofauti ziilzokuwa zimehifadhiwa sehemu tofauti kujaribu kuzioanisha na eneo jipya kusini mwa bahari ya Hinidi.
"Hakuna mtu alikuwa na jawabu kabla ya kujumlisha data kutoka setilaiti, data za Boeing, data za bahari na mabaki yaliyokuwa yakielea," alisema.
Godfrey alisema kuwa kazi zimeendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja na tumefanya majaribio kadhaa kwa wazo hili jipya na kuwa na uhakika wa kulitumia kwa MH370.
Eneo kamili tulilogundua kwa kutumia hesabu za data ni karibu digrii 33 kusini na digrii 95 mashariki katika bahari ya Hindi.
Shughuli mbili za utafutaji wa MH370 zimefanyika bahari ya Hindi bila kuzaa matunda.
Shughuli hizi za kutafuta zimegharimu mamilioni ya dola huku jamaa wakisisitiza kuwa wapendwa wao wapatikane, gharama ni kubwa sana.
"Ushahidi unaoonekana"
Grace Nathan alipoteza mama yake Anne, katika ajali hiyo
Umekuwa ni wakati mgumu sana, hakujakuwa na mwisho, tunaonekana kuzunguka tu na kugonga ukuta mmoja hadi mwingine.

Chanzo cha picha, RICHARD GODFREY
"Tumekuwa tukisubiri kitu kipya kwa muda mrefu"
Nathan wakili anayeishi mjini Kuala Lumpur anataka data hiyo mpya ifanyiwe majaribio na wataalamu wa safari za anga ambao wanaweza kuelewa sayansi ya eneo la ajali na kuonyesha kuwa nadharia hiyo ni ya ukweli.
"Tunakaribisha matokea yote mapya, hususan iwapo yanatokana na ushahidi unaoonekana. Katika kisa hiki, unatokana na ushidi unaoonekana. Kuna mambo yanayoweza kufanyiwa hesabu na hayatokani tu na picha za Google au vitu ambavyo haviwezi kuthibitishwa," alisema.
Shughuli za awali za kuitafuta MH370 zimekuwa ngumu kutokana na ukubwa wa eneo la kutafuta. Godfrey anaashiria kuwa wametafuta eneo la hadi ukubwa wa kilomita 120,000 na hawatafuti sindano kwenye nyasi, lakini kitu kidogo sana kwenye nyasi, ni vigumu sana kufanya hivyo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kina cha mita 4,000
Pendekezo jipya na mhandisi ni maili 40 mduara, eneo ndogoo zaidi kuliko yaliyotafutwa awali.
Mabaki hayo yanaweza kuwa kwenyee mwamba au kwenye sakafu ya bahari," alisema.
"Na utahitaji kusaka eneo hilo mara tatu au nne kabla ya kuanza kukusanya vitu.
"Mabaki hayo yanaweza kuwa kina cha umbali wa hadi mita 4,000," aliongeza
Zaidi ya vipande 30 kutoka ndege hiyo vimesombwa kwenda fukwe za pwani ya nchi za Afrika na visiwa vya bahari ya Hindi.

Chanzo cha picha, Reuters
Mwaka 2009 Godfrey alikuwa asafiri kwa ndege ya shirika a ndege la Ufaransa ya 447 kutoka Rio de Janeiro hadi Paris lakini kutokanna na mipango ya kazi alilazimika kubaki Brazil.
Ndege hiyo haikuwasili ilikokusudia kufika na ilipotea katika habari ya Atlantic. Tangu wakati huo alianza kufanya utafiti kuhusu ndege zilizopotea baharini na kupatikana kwao.
Godfrey ni mwanachama kwa kundi huru la MH370 na ni mhandisi aliye na ujuzi wa kuunda mifumo ya kutua na ile otomatiki ya ndege.
Ushahidi thabiti
"Tunataka kuwa eno la kusini mwa bahari wakati wa msimu wa joto, ambao ni sasa. Kwa hivyo shughuli za kutafuta zinaweza kuanza tena katika kipindi cha miezi 12 kwa sababu huwezi kukusanya raslimali na kuziweka pamoja kwa muda mfupi.
Ni wakati China ichukue jukumu la kuwatafuta waathiriwa wao. Au kampuni za binafsi zinawez kutafuta, zikifadhiliwa na kampuni za bima," anasema.
Kulikuwa na raia 122 wa China kwenye ndege hiyo ya MH370 iliyoondoka Kuala Lumpur lakini haikufika ilikotakiwa kufika, Beijing.

Chanzo cha picha, ANNE NATHAN
Kutoweka huko kumeibua nadharia tofauti kuhusu kile kilichofanyika.
Moja ya nadharia ni kwamba ndege hiyi ilitekwa na rubani ambapo rubani alichukua usukani na kuzima mitambo ya rada kabla ya kugeuka kwenda ghuba ya Thailand na kueleka magharibi.
Kuhusika kwa bodi ya usafiri ya Australia katika shughuli za kuitafuta ndege hiyo zilifkia kikomo Oktoba mwaka 2017.
Uamuzi wowote wa kuanza tena shughulu za kutafuta ndege ni suala la serikali ya Malaysia ambayo ndo nchi ndege hiyo ilisajiliwa.












