Je kufanya kazi zamu usiku kunaathiri vipi afya yako? Hivi ndivyo moyo wako unavyoathirika

ikiwa umewahi kufanya kazi kwa kubadilisha mifumo ya zamu, unajua kwamba zamu za usiku zinaweza kukuacha ukiwa na uchovu, lakini je unajua kwamba uchovu huo pia unaweza kuwa mbaya kwa moyo wako?

If you have ever worked in a job with changing shift patterns, you know that nightshifts can leave you groggy and lethargic, but did you know that they can also be bad for the heart?

Utafiti mpya umeonyesha kwa nini hasa - na yote yanahusiana na 'saa za kibiolojia' za ubongo na moyo.

Hizi zinaweza kubadilishwa kwa kubadilisha mifumo ya mabadiliko, na kufanya moyo kuwa katika hatari ya kutofanya kazi vizuri.

Na hiyo inaweza kuwa mbaya sana kwa afya yako.

Saa za kibaiolijia ambazo hazijasawazishwa

Utafiti huo uliofanywa na Maabara ya MRC ya Biolojia huko Cambridge uliangazia saa ya ndani katika kila seli ya moyo ambayo hubadilisha usawa wa kemikali wa seli siku nzima.

Mwili wako unahitaji moyo wako kufanya kazi kwa bidii wakati unafanya kazi - hufanya hivi kwa kufanya moyo kupiga haraka.

"Jinsi moyo unavyopiga huamuliwa na mambo mawili: ishara kutoka kwa ubongo na viwango vya sodiamu na potasiamu ndani ya kila seli ya moyo, ambayo huchochea mapigo ya moyo," Dk John O'Neill, aliyeongoza utafiti huo, aliiambia BBC.

"Katika watu walio na afya njema seli hizi zinawianishwa na saa za kibailojia," alisema.

Lakini utafiti mpya uligundua kuwa tunapobadilisha zamu, ubongo hubadilika haraka sana, lakini saa za mwili ambazo tunazo katika kila seli ya moyo hubaki nyuma.

"Una siku chache ambapo ishara kutoka kwa ubongo hazilingani na kile ambacho moyo unatazamia," Dk O'Neill aliongeza. "Na hiyo ndio tunafikiria inawafanya wafanyikazi wanaobadilisha zamu kuwa hatarini zaidi wakati mpito kati ya zamu ya mchana na usiku.''

Hii huongeza hatari ya magonjwa mbalimbali ya moyo, hasa wakati wa mpito kati ya zamu ya mchana na usiku, ingawa ni lazima ieleweke kwamba kazi ya zamu itakuwa moja tu ya sababu nyingi za hatari katika kuendeleza matatizo ya moyo, ikiwa ni pamoja na umri, jinsia, historia ya familia na chakula.

Hatari za kiafya

"Kuna idadi ya matukio mabaya ya moyo," alisema Dk O'Neill. "Kinachotisha zaidi kinafahamika kama 'kifo cha ghafla cha moyo' ambapo moyo huchanganyikiwa na kuacha kufanya kazi kwa muda. Nahlai hii isipotibiwa mapema inaweza kusababisha kifo."

Kwa bahati nzuri, hali hii ni nadra sana, lakini kazi ya zamu imeonekana kuongeza hatari sio tu ya shida za moyo, lakini pia shida ya mmeng'enyo wa chakula, shida ya mhemko na huongeza hatari ya saratani kwa ujumla ikilinganishwa na watu wanaofanya kazi zamu za mchana pekee.

Hatari hii imetambuliwa na baadahi ya serikali - nchini Denmark, kwa mfano,wale ambao wamefanya kazi zamu za usiku kwa zaidi ya miaka 20 na kupata saratani wana haki ya kulipwa.

Ili kuwa na afya njema, saa zetu zote za kibaolojia zinahitaji kusawazishwa.

Ili kufanya hivyo kwa ufanisi, ni bora kuwa na utaratibu wa kila siku unaohusisha kulala wakati wa usiku na kula na kufanya kazi wakati wa mchana, lakini kwa mamilioni ya wafanyakazi hii haliwezekani.

Hata hivyo, wataalamu wa usingizi wanasema tunaweza kuchukua hatua mbalimbali za kivitendo ili kusaidia kupunguza madhara yanayotokana na kufanya kazi usiku.

Kukabiliana

"Kama wanadamu, ni rahisi kwetu kuchelewesha saa za mwili wetu, na vile vile saa kuu katika ubongo," anasema Dkt Renata Riha, Mshauri wa Tiba ya Usingizi na Kupumua katika Chuo Kikuu cha Edinburgh.

Anasema ratiba ya kazi inapaswa kuanza na zamu za mchana, kisha zamu za kutoka usiku, na mwishowe zamu za kukesha.

Ni vyema kufanya mizunguko mirefu ya zamu za usiku kwa angalau wiki mbili kwani huipa mwili wetu muda wa kuzoea.

"Inachukua takriban wiki moja kwa saa zote kuhama - saa kuu inayohusika na utoaji wa melatonin (homoni ya usingizi), ikifuatiwa na saa katika viungo vingine vyote vya mwili," Dk Riha anasema.

Pia anapendekeza kulala kidogo kwa dakika 20 hadi 30 wakati wa zamu ya usiku.

Kwa wastani mtu mzima anahitaji saa saba hadi nane za usingizi, lakini usingizi wote sio sawa.

Kulala wakati wa mchana sio sawa na usiku kutokana na tofauti za nyakati, na kunaweza kunyima mwili mapumziko yanayohitajika.

Dk Riha anasema wafanyakazi wa usiku wanapaswa kujaribu kwenda kulala mara tu wanaporudi nyumbani.

"Jaribu kalala katika mazingira yenye utulivu na chumba baridi kisicho cha mwangaza. Unaweza kutumia barakoa ya macho ikiwa huna mapazia au kitu cha kuzuia mwanga wa jua,"anasema.

"Ikiwa chumba chako kina joto, fikiria kuhusu njia za kukipoeza, kutokana na kutumia mto uliopozwa au feni. Kupunguza halijoto kunaudanganya mwili wako kufikiria kuwa ni wakati wa kulala."

Kuhadaa mwili wako

Mazoezi na chakula chenye liche bora pia kinaweza kusaidia ,cha msingi ni muda wa kufanya hivyo.

Kula na kufanya mazoezi kunaathiri moja kwa moja saa na mfumo wa mwili kupitia mabadiliko katika insulini ya homoni na joto la mwili, mtawaliwa.

Tunaweza kuhadaa miili yetu kukubali nyakati mpya kwa kujiweka kwenye mwanga na kupata 'kifungua kinywa' cha kisa sawa kabla ya kuanza zamu yetu ya usiku, na kisha kuepuka chakula na mwanga 'wakati wa usiku' mpya.

"Hakuna dawa amabayo tunaweza kurumia (kwa sasat)ambayo inaweza kubadili saa yako ya kibaiolojia, lakini ikiwa unahama kutoka zamu ya mchana kwenda zamu ya usiku, unahitaji tu kubadilisha utaratibu wako wote wa kila siku wakati wa mchana kabla ya zamu yako ya kwanza ya usiku, na ushikamane na utaratibu uliobadilishwa," anasema Dk O'Neill.

"Hii itakusaidia kukabiliana haraka zaidi na kuepuka madhara mengi yasiyofaa."