Davemaoite: Madini ambayo hayajawahi kuonekana ndani ya almasi

Chanzo cha picha, Aaron Celestian/NHMLA
Watafiti wa madini ya almasi nchini Botswana walikata tamaa miongo mitatu iliyopita wakati waligundua madini ya kijani kibichi yaliyokuwa na alama nyuesi ndani yake.
Hawakuona thamani kubwa kwenye madini haya hivyo waliyauza kwa mtaalamu mmoja wa madini nchini Marekani ambapo yamehifadhiwa tangu mwaka 1987.
Utatifi wao ulisubiri hadi kundi moja la wataalamu kugundua kitu cha kushangaza jinsi wanavyoleza kwenye chapisho la wiki iliyopita la jarida la sayansi.
Jiwe hilo halikuwa almasi yenyewe, lakini alama zilizokuwa ndani yake zililifanya lisiwe kamilifu. Lilikuwa na kitu kinachojulikana kama devemaoite.
Ni madini ambayo hayajawai kuonekana moja kwa moja na wanasayansi na yanapatikana sehemu zenye msukumo mkubwa kama zile zilizo mbali ndani ya ardhi ya dunia.
Lakini kwa kuwa yalikuwa ndani ya almasi yalipata uwezo wa kufika juu ya ardhi.
Kuyapata madini haya "inatuonyesha mengi kuhusu kubadilika kwa dunia," alisema mwana jiolojia Oliver Tschauner ambaye aliongoza utafiti katika chuo cha Nevada huko Las Vegas.
Ugunduzi usiotarajiwa
Davemaoite ni madini yaliyopewa jina la mwana jiolojia raia wa China Ho-Kwang "Dave" Mao lakini kawaida hujulikana kama calcium silicate perovskite.
Hadi sasa wanasayansi wamefanikiwa kuyaiga kwenye mahabara kwa sababu huwa yanatengenezwa chini ya msukumo wa juu na joto.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ikiwa madini haya yatawekwa kwenye msukumo wa chini yatatengana kwa hivyo wanasayansi walifikiri kuwa wasingeweza kufanikiwa kuyaona na kupata sampuli.
Lanini kutokana na kwamba yalikuwa ndani ya almasi ambayo pia ni madini yatokanayo na msukumo mkubwa kwenye mkaa, waliweza kuyaona hata kama ni kwa muda mfupi.
Wakitumia X-ray Tschauner na wenzake waliyagundua kwenye jiwe la kijani kibichi lililopatikana nchini Botswana miaka ya 1980.
Tschauner anasema jiwe hilo liliundwa takriban umbali wa kilomita 660 ardhini na msukumo kama wa mara 1000 kuliko ule wa anga kwa dunia.
Sekunde ya maisha
Davemaoite ni sehemu ndogo ya kile kilicho ndani ya ardhi ya dunia kwa mfano asilimia 5 hadi 7 kulingana na wataalamu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati inakutana na madini kama uranium na thorium unakuwa sehemu ya mchakato unaochangia kuwepo joto mbali ndani ya ardhi.
Kuvunjwa kwa almasi, wanasayansi walikuwa na sekunde moja tu ya kuchunguza davemaoita, kwa sababu baada ya hapo iligeuka na kuwa kioo.
Walichogundua kinawawezesha wanasayansi kuelewa kinachondelea ndani ya ardhi ya dunia na kwa njia gani madini huundwa katika mazingira hayo.
"Kwa wafanya biashara wa vito na wanunuzi wa almasi ukubwa, rangi na ubora ni mambo makuu lakini alama hizo nyeusi zinazowakasirisha wafanyabiashara wa vito, ni zawadi kwetu," alisema Tshauner alipokuwa akitangaza ugunduzi huo.












