Mashindano ya makombora ya Korea Kaskazini na Kusini … Kwanini nchi hizi mbili zinashindana kuongeza silaha ?

Dunia imekuwa ikishuhudia Pyongyang mpango wa nyuklia na makombora ya masafa mkubwa kuwahi kushuhudiwa kamwe . Korea Kaskazini pia imekuwa ikikabiliwa na vikwazo .

Lakini Korea Kusini inatazamia kuongeza zaidi mpango wake wa makombora baada ya kuondolewa kwa vikwazo vya muda mrefu dhidi ya Seoul mwezi Mei mwaka huu.

Hatua ya korea Kusini ya kuongeza silaha zake za makombora kukabiliana na Korea Kaskazini kunaibua maswali kuhusu malengo ya mpango wa nyuklia wan chi hiyo. Pia ina uungaji mkono wa ndani ya nchi ya Korea Kusini.

Nchi hizi mbili zinapanua mpango wake wa silaha huku zikionesha utashi wa kufanya mazungumzo. Hatahivyo, juhudi za kila upande za kuongeza makombora zimekwamisha mazungumzo baina ya nchi mbili.

Tarehe 11 na 12 Septemba, vyombo vya habari vya Korea Kaskazini viliripoti kwamba Chuo cha sayansi ya ulinzi cha Korea Kaskazini kilifanya jaribio la aina mpya ya makombora ya masafa marefu yanayojiongoza kulenga eneo.

Makala ilisema kuwa makombora hayo mapya yameundwa kwa umbo la yai, nnamba nane, yana uwezo wa kupaa angani kwa takriban masaa mawili.

Vyombo vya habari vilitaja uwezo wa makombora ya kulenga maeneo yaliyo umbali wa kilomita 1500.

Siku mbili baada ya tangazo hilo Korea Kaskazini pia ilizindua kombora jinginge lililotengenezwa kwa vyuma vya treni.

Jeshi la Korea Kaskazini limeyaelezea makombora hayo kama makombora ya ballistic umbali wa kilomita 800 kabla ya kutua. Makombora ta Ballistic husafiri hadi kilomita 800 kabla ya kutua katika Bahari ya Mashariki(East Sea).

Septemba 28 Korea Kaskazini ilizindua kombora jipya la Hasong-8 hypersonic. Nchi hiyo inasema kombora jipya ni moja ya makomboira yake ''Matano muhimu''

Awali Pyongyang lifanya majaribio kadhaa ya silaha baina ya Mei 2019 na Machi 2021

Gwaride la Oktoba lilikuwa na maonyesho ya silaha nyingi mpya

Wataalamu wa Marekani wamezungumza na BBC kuhusu athari za vita vya Korea Kaskazini

KIwa upande mwingine Korea Kaskazini inazindua makombora mapya , huku Korea Kusini pia ikizindua polepole silaha zinazotengenezwa ndani ya nchi hiyo.

Septemba 15, Rais Moon Jae-in alisimamia jaribio la kombora la masafa la ballistic lililotengenezwa kutokana na manoari ya ndani ya nchi.

Inaonekana Hyun Moo alilipatia jina la 4-4.

Linadhaniwa kufanana na kombora la masafa mafupi la zamani la Hyun Moo 2B aina ya ballistic (SLBM).

Makombora hayo yalizinduliwa kutoka kwenye manuari yenye uzito wa tani 3,000 inayofahamika kama Dawson Ahn Chang Ho.

Zilikuwa ni manoari tatu za kwanza kutengenezwa ndani ya nchi. Hisi zina uwezo wa kupiga hadi umbali wa kilomita 500.

Makombora ya masafa mafupi ya ballistic na manoari sio mafanikio pekee ya Korea Kusini . Korea Kusini pia ilizindua "Kombora la masafa marefu linaloweza kupiga ardhini kutroka angani" tarehe 15 septemba.

Katika siku hoyo hiyo Wizara ya ulinzi ya Seoul ilifichua kombora la aina ya supersonic linaloweza kujiongoza kupiga eneo, likiwa ni kombora lenye nguvu zaidi la ballistic.

Aina mpya ya roketi inayotarajiwa kuzinduliwa katika anga za mbali ifikapo mwaka 2024 pia imefanyiwa majaribio.

Nani mwenye nguvu?

Nguvu na udhaifu wa jeshi la Korea mbili ni tofauti. Hii inaonyesha maendeleo ya nchi zenyewe baada ya Vita vya Korea.

Kulingana na wavuti wa uchambuzi wa kijeshi, Korea Kaskazini imewekwa katika nafasi ya 28 na Korea Kusini iko nafasi ya sitini katika orodha ya vikosi vya kijeshi vya mataifa 140 yaliyochambuliwa na taasisi ya global firepower.

Korea Kaskazini ni nchi ya nne kwa kuwa na idadi kubwa ya wanajeshi duniani , ikiwa na jumla ya wanajeshi milioni 1.3, huku Korea Kusini ikiwa na wanajeshi 600,000.

Korea Kaskazini imeanza juhudi za kuboresha zana zake za kijeshi kwa kutengeneza silaha mpya . Lakini tisho la nyuklia la nchi hiyo ni nguvu kwa nchi hii.

Katika miaka ya nyuma, Korea Kaskazini pia ilionyesha nia katika kutengeneza mpango wa silaha, lakini shinikizo kutoka Marekani lilipelekea kusainiwa kwa mkataba unaozuwia utengenezwaji wa silaha za nyuklia katika mwaka 1975, na kuweka sharti kwamba mpango wa nyuklia uwe ni maslahi ya amani tu.

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Seoul mwaka 2020 ulibaini kuwa asilimia 46,9 ya raia wan chi hiyo wanaunga mkono silaha za nyuklia, huku 21.8 wakipinga silaha hizo.

Je namba za simu za dharura zitafanya kazi tena?

Dada yake Kim Jong Un Kim Yoo Jong amekuwa akikosolewa kwa kuhoji uwezo wa Korea Kusini wa silaha.

Seoul, kwa upande mwingine, inaendelea kuongeza hifadhi yake ya silaha.

Tarehe 21 Septemba, Moon alitoa wito wa kumalizika kwa Vita vya Korea, huku Kim Yo-jong ikionekana kuishiwa nguvu. Vita vya Korea vilimalizika kwa makubaliano ya usitishaji mapigano mwaka 1953 kati ya nchi hizo mbili.

Alisema kuwa pendekezo la kumaliza vita vya Korea lilikuwa na kupongezwa na kuionya Korea Kashazini kubadili msimamo wake kama hili lingewezekana.

Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini ameelezea wasi wasi wake kuhusu pendekezo la Moon.

Alionya kuwa nchi zoter mbili zitatumbukia katika mashindano ya silaha yasiyomalizika.

Seoul inatarajiwa kufanya mazungumzo kabla ya muhula wa Bw Moon kumalizika mwaka ujao baada ya pendekezo la Kim Jong Un kurejesha mawasiliano ya simu yaliyokuwa yameharibika baina ya Korea hizi mbili.

Huku nchi hizi mbili zikipanua uwezo wa makombora yake na mipango ya anga za mbali, kuna haja ya kuwepo kwa uwiano baina ya mazungumzo na vichocheo vya vita.