Wanaume wa Singapore ambao wako radhi kufungwa jela kwa ajili ya imani zao

Yeo Zheng Ye alikulia Singapore akijua kuwa siku moja atalazimika kwenda jela.

Kama mshirika wa kanisa la Jehovah's Witnesses, imani yake inamzuia kubeba silaha na kujiunga na vitu vyote vilivyokusudiwa kwa vita

Kwa hivyo alipotimiza miaka 20, alikataa kujiunga na mpango wa huduma kwa taifa, na kufungwa jela kwa miaka miwili na nusu.

Ijapokuwa Singapore haikuwa vitani, utumishi wa kijeshi ni lazima kwa raia wote wa kiume nchini na kizazi cha pili cha wakazi wa kudumu wanapofikisha miaka 18.

Tangu 1970, inakadiriwa kuwa washirika wa kanisa la Jehovah Witnesses wanafungwa jela kila mwaka, ingawa hakuna anayeingizwa kwenye rekodi ya kudumu ya uhalifu wa jinai.

Bw. Yeo alifungwa jela kwa karibu miaka mitatu, mwaka mmoja zaidi ya muda ambao ungechukua kupata mafunzo ya huduma kwa taifa.

Akiwa jela, angeliamka saa kumi na moja alfajiri kuosha vyoo na kupiga deki varanda ya urefu wa mita 200 ambayo mara nyingi inachafuliwa kwa viatu vyenye tope.

"Wafuasi wa Jehovah Witnesse's hawalazimishwi kufanya mazoezi na kubeba magunia ya mchanga kama wanavyofanya wafungwa wengine kila siku," alisema afisa wa zamani wa polisi ambaye hakutaka jina alke litajwe.

Bw. Yeo anasema ilimchukua - karibu mwaka mzima kuzoea mazingira ya jela.

"Nililia sana, kwa siku kadhaa. Nililia kabla niende jela, hasa nilipofahamu kwamba sitoweza kutoka wala kukutana na jamaa na marafiki zangu kwa miaka miwili na nusu ijayo," alisema.

Ndugu yake mkubwa aliyemtegemea kwa ushauri na ambaye pia ni mfuasi wa kanisa hilo alifungwa jela mwaka uliotangulia kwa kuwa yeye pia ni mfuasi wa kanisa.

"Nilidhani angalau nitamuona ndugu yangu,"alisema Bw. Yeo.

Familia ya waumini

Bwana Yeo na ndugu yake waliingizwa katika Imani hiyo walipokua watoto wadogo.

Baba yao alijiunga na kanisahilo baada ya kuhudumu kama mwanajeshi.

Baada ya kukamilisha mafunzo ya awali ya miaka miwili ,wanahitajika kufanya majukumu ya kikosi cha ziada kwa wiki kadhaa mara moja kwa mwaka. Mpango ambao unaendelea kwa miaka 10.

Kwa hivyo Baba yake Bw.Yeopia alifungwa jela kutokana na imani ya dini yake.

"Mama yangu sio mshirika wa kanisa, lakini alijua kuwa [kifungo gerezani] kinanikabili mimi na ndugu yangu kwa sababu baba yetu alikuwa amerejea kizuizini mara kadhaa, wakati mwingine hali hiyo ikitishia kazi yake," anasema Bw. Yeo.

Waajiri nchini humo wanatakiwa kisheria kuwaachia wafanya kazi wao kwa mafunzo ya kila mwaka ya uhifadhi.

Hata hivyo washirika wa kanisa la Jehovah's Witnesses ambao wanakataa kujiunga na mafunzo hayo wanafungwa jela kwa siku 40 zaidi, na wanapoteza ulinzi huo.

Jordan Chia, mwalimu wa somo la muziki wa Jehovah's Witness alihukumiwa kifungo cha miezi saba jela na kazi ngumu kwa kukataa kwenda kufanya majukumu ya ulinzi kwa mara ya pili.

"Ilikuwa ni changamoto kwa sababu sikuju nitakaa kizuizini muda gani. Niliwaambia waajiri wangu hawana lazima ya kuiweka kazini kama sipo," Bw Chia aliambia BBC.

"Lakini kwa bahati nzuri walifanya hivyo."

Kanisa na nchi

Maswali yanayohusu hitaji la kupeleka gerezani wanaokataa kujiunga na mpango wa utumishi kwa taifa yamewasilishwa katika Bunge la Singapore mara kadhaa.

Lakini mawaziri wamesisitiza umuhimu wa kuwa na adhabu kali ya utekelezaji wa sera hiyo wakisema kuwa "huduma kwa taifa ni kiungo muhimu kwa usalama wa nchi ndogo kama Singapore".

"Hakuna raia wa Singapore anastahili kuruhusiwa kutoa sababu yoyote ya kujiondoa katika juhudi za ulinzi wa kitaifa kwani kila Msingapore ananufaika na amani na usalama ambayo Huduma ya Kitaifa imesaidia kuimarisha, "Matthias Yao Chih aliliambia Bunge mnamo 1998 wakati alipokuwa Waziri wa Nchi kwa Ulinzi.

Sasa wanaishi na kufanya kazi katika magereza tofauti na wafungwa na wanapewa wiki kadhaa za likizo kila mwaka.

"Washirika wetu nchini Singapore wamekuwa wakielezea mamlaka hamu yao ya kutaka kuchangia ustawi wa jami," alisema masemaji wa chama cha Jehovah's Witnesses kanda ya Asia-Pacific

Bw.Yeo anasema aliwahi kuomba kuhudumu kataka kazi zingine za kiraia kama wazima moto ambayo hufanywa na watu waliopitia mafunzo ya huduma kwataifa.

Jamii ya kimataifa inaunga mkono watu kufanya huduma mbadala.

Mkataba wa Ulaya wa kutetea Haki za Binadamu unasema kwamba nchi zinapaswa kutoa huduma mbadala kwa raia ambao wanaamini ''matumizi ya nguvu yanaweza kukinzana na uhuru wa kuabudu su imani ya mtu ."

Bwana Yeo hata hivyo aliachiliwa huru mwezi Aprili, siku moja kabla ya Singapore kuweka amri ya kwanza ya kutotoka nje ili kudhibiti maambukizi ya Corona.