Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fahamu faida za kiafya za kumkanda mtoto mchanga
Utamaduni wa kuwakanda watoto umekuwepo kwa karne kadhaa katika nchi mbali mbali mbali duniani hususani kusini mwa Asia. Sasa wanasayansi wanasema utamaduni huu huenda ukaokoa maisha ya watoto wengi.
Renu Saxena alirejea nyumbani kutoka hospitali na mtoto wake mchanga baada ya kujifungua salama. Lakini kilichomshangaza ni muonekano wa mtoto huyo. Alikua mdogo sana na ngozi yake ilikuwa nyepesi kiasi cha kuona mishipa inavyopita kwenye ngozi yake nyepesi.
Saxena alijifungua mapema kabla ya muda wake akiwa na ujauzito wa wiki 36, mtoto akiwa na uzani wa kilo mbili na gramu nne(2.4kg).
Familia ya Saxena ilimshauri awe anamkanda mtoto kila siku kwani itamsaidia kukua. Lakini madaktari walimshauri asubiri kidogo hadi uzani wa mtoto uongezeke kabla ya kumkanda.
Saxena alikubaliana nao na kusubiri kwa wiki mbili. Katika kipindi hicho mtoto aliongeza uzani wa gramu 100 na alikuwa akilala na kuamka kila baada ya muda mfupi.
Saxena alimwajiri muuguzi mstaafu ambaye pia ni mtaalamu wa kushughulikia watoto wachanga na kujifunza jinsi ya kumkanda mwanawe. Mambo yalianza kuwa mazuri, mtoto akaanza kulala vizuri na pia kuongeza uzani wa mwili.
Matokeo hayo ni ishara wazi kwamba kumkanda mtoto mdogo kuna manufaa makubwa. Asia Kusini hata watoto waliozaliwa kabla ya muda wao kutimia pia hukandwa.
Utafiti unaonesha kuwa mafuta yanayotumiwa kukanda yakitumiwa kwa usashihi yana uwezo wa kusaidia uzani wa mtoto kuongezeka, kuzuia magonjwa yanayosababishwa na bakteria na kupunguza vifo vya watoto wachanga kwa hadi asilimia 50.
Utafiti hata hivyo unapendekeza kuwa wazazi wanaotaka kufanya utaratibu huo, kwanza wapate ushauri kutoka kwa wataalamu kuhakikisha ni salama kwa mtoto wao.
Familia zinazoenzi utamaduni huu wa kale, pia zina mtazamo wao.
Saxena ambaye pia meneja wa zamani wa mauzo anatokea jimbo la Uttar Pradesh kaskazini mwa India, eneo ambalo linajulikana kwa utamaduni huu wa kumkanda mama na mtoto baada ya kujifungua.
Familia yake imekuwa ikifuata utaratibu huu kwa miaka na mikaka.
''Mama yangu kila wakati alikua akiniambia kwamba nilikuwa haraka sana baadaa ya kuzaliwa- Mimi nilikua mtoto wake wa tatu, anasema ukuaji wangu wa kasi ulichangia wa kukandwa kila siku aliporejea nyumbani kutoka hospitali'', anasema Saxena.
Muuguzi wa kuwatunza watoto wachanga alimfunza Saxena jinsi ya kutayarisha mafuta ya kukanda- kwa ubadilisha kati ya mafuta ya nazi na ya uto ambayo yanahitaji kuwa vuguvugu kabla ya kuanza kutumia -Mtoto anastahili kukandwa kwa walau kwa muda wa dakikia 30 na kisha kumuogesha mtoto kwa maji ya uvuguvugu.
''Tulianza kwa kumkanda taratibu maeneo ya tumbo hadi sehemu nyingine za mwili ikiwa ni pamoja na vidole vya miguu na kuendelea na utaratibu huo hadi kichwani'' anasema Saxena.
Watafiti wanasema kumkanda mtoto akiwa mchanga kuna manufaa ya kiafya ambayo yanaweza kumsaidia hata akiwa mtu mzima.
''Ngozi ni sehemu kubwa ya mwili wa binadamu ambayo mara nyingi umuhimu wake na afya yake hupuuzwa kwa ujumla.'' Anasema Gary Drmstadt, Profesa wa Tawi la tiba inayoshughulikia matibabu ya watoto wachanga na tiba endelevu katika Chuo Kikuu cha Stanford.
Mara ya kwanza alipozuru Bangladesh na India, Drmstadt aligundua kuwa kinamama hususani wale wazee walipendelea sana kuwakanda watoto wachanga. ''Nilishangaa sana nilipojua kwamba utamaduni huuu umekuwepo kwa karne kadhaa,ndipo nikaanza kutafiti zaidi,''anasema.
Na mnamo 2008, katika utafiti wa watoto 497 waliozaliwa kabla ya muda ambao walipokea masaji ya kila siku katika hospitali huko Bangladesh, Darmstadt na washirika wake walionesha kuwa zoezi hili la zamani linanaweza kuokoa maisha ya watoto.
"Tulibaini kuwa hatari ya maambukizi ilipungua kwa asilimia 40, huku hatari ya vifo ikipungua kwa kati ya asilimia 25 hadi 50. Matokeo ambayo ni muhimu sana," anasema.
Katika utafiti mwingine tofauti, watafiti hao pia waligundua kuwa masaji ya kawaida husaidia kujenga microbiome ya mtoto - aina ya bakteria inayopatikana kwenye ngozi na kwenye utumbo. Microbiome ina jukumu muhimu sana katika kuongeza kinga.
Faida za kumkanda mtoto
Wanasanyansi wanasema kuwa kukanda kunasisimua neva zinazounganisha ubongo na tumbo, hali inayosaidia umeng'enyaji mzuri wa chakula kwa mtoto na kupata virutubisho, hali inayosaidia watoto kuongezeka uzito.
Kumkanda mtoto tumboni kunampunguzia maumivu, hii ni muhimu hasa kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda wao kutimia kwa kuwa hutumia muda miezi wakiwa wapweke hospitali.
Kumkanda mtoto pia kunaboresha usingizi wake na kusaidia kutolewa kwa homoni ya oxytocin.
Kukanda mtoto kunakufanya ujifunze jinsi ya kuwasiliana na mtoto. Kunamfanya mtoto ajihisi yuko salama, mwenye kupendwa na kuheshimiwa, pia mzazi unajifunza tabia zake na kumuelewa vyema.
Mzazi utakuwa mwenye kujiamini, na tafiti zinasema hali hii itakufanya upunguze msongo wa mawazo baada ya kujifungua.