Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi safari za mbuga ya Maasai Mara zinavyoathiri maisha ya wanyapori Kenya
- Author, Vivienne Nunis
- Nafasi, BBC News, Kenya
Asubuhi na mapema katika hifadhi ya Maasai Mara ya Kenya - nyumbu wakila kwa utulivu, ndege wanajazana kwenye matawi ya mti wa acacia na pundamilia wengine wakitembeatembea karibu - ghafla simu ya redio inaingia.
Mwongozaji wetu akiendesha gari kwa mwendo wa kasi katika maeneo tambarare baada ya kuambiwa "ndugu wanne" maarufu wako kwenye matembezi.
Duma hawa madume wanajulikana kufanya kazi pamoja na ufanisi mkubwa - ingawa, pamoja na nyumbu wengi katika maeneo ya karibu, ni ngumu kufikiria kifungua kinywa kitakuwa changamoto kubwa.
Kwetu sio mbio tu za gari ya magurudumu manne tu kwenye nyasi kavu kushuhudia mauaji . Magari mengine yasiyopungua 27 yanazunguka kundi la pundamilia na nyumbu wakisubiri onesho.
Duma wanne mwishowe wanapopata mawindo yao kumwangusha nyumbu mmoja chini, karibu nusu ya magari huzunguka ili kuwatazama. Kila gari hubeba kikundi cha watalii, kamera mkononi, wakipiga picha za taya za duma shingoni mwa nyumbu na kurekodi kilio cha mwisho cha huzuni cha mnyama huyo.
Mauaji ndio watalii wengi huja kuona. Ukatili wa ufalme wa wanyama ulivyotekelezwa.
Wachache wangeweza kusema walikuja kuona makundi ya watalii wengine, wakitoza malipo kwa mwandamo unaofuata, au kwamba walifurahia mazingira ya namna magari ya Land Rover yaliyokuwa yameegeshwa ; lakini kwa wengi ndivyo safari ya kwenda Mara imekuwa.
Mwezi uliopita, serikali ya Kaunti ya Narok ilitoa tena sheria na miongozo ambayo inapaswa kuzingatiwa wakati wa kuchukua watalii kwenye maeneo ya hifadhi
Inakuja baada ya kundi la wageni na kambi yao kupigwa marufuku kutembelea Mara mwezi Julai, baada ya video iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii kuonesha mtu akipiga picha ya mtoto wa chui kwenye akiwa amekaa kwenye gari lake mlango ukiwa wazi.
Kanuni hizo zinasema magari lazima yawe angalau umbali wa mita 25 (futi 82) mbali na spishi za paka na madereva hawapaswi kuweka mzunguko wa magari karibu na wanyama, ambao wanahitaji kuweza kutathmini mazingira kwa hatari inayoweza kutokea.
'Safari ya Ferrari'
Kunapaswa pia kuwa na kiasi cha magari matano wakati wowote - lakini hili kwa kawaida hupuuzwa.
Kukamatwa ukivunja sheria kunaweza kukusababishia faini papo hapo, kuondolewa mara moja kutoka Mara au marufuku ya ziara za baadaye.
Lakini kutekeleza sheria katika eneo la kilomita za mraba 1,500 sio rahisi na John Ole Tira, mwenyekiti wa Chama cha Miongozo ya Mara - kikundi cha hiari na washiriki 175 - anasema pia kuna shida ya kukidhi matarajio ya watalii.
"Wanapolipa pesa, wateja wengi, ikiwa hawakuona simba au tembo - 'Big Five' - wanafikiria hawakuona chochote."
"Big five" - simba, tembo, nyati, faru na chui - ni neno ambalo awali lilibuniwa na wawindaji wa wanyama walio wagumu sana kuua.
Phoebe Mottram, mhifadhi wa Uingereza anayeishi Afrika Kusini ambaye alikuwa akifanya kazi kama mwongoza safari, anasema ingawa sasa inahusu kutazama wanyama na sio kuwapiga risasi wanyama, wazo la Big five linabaki kuwa tatizo.
"Linapokuja kwenye soko," anasema.
"Wageni wanataka kuona kile wanachoambiwa wanapaswa kuona, na waongozaji wengi huishi kwa kupata posho, kwa sababu mishahara yao haitoshi.
"Kwa hivyo mwongozaji atakayewapat Big Five, hupata posho bora ."
Yeye na mwenzi wake Lawrence Steyn, mwongozaji mwingine wa zamani, hivi karibuni walizindua jukwaa mtandaoni ambalo linalenga kuwaunganisha watalii na kambi na miongozo ya safari ya kimaadili, inayoitwa Thatch na Earth.
"Una jukumu pale unapoweka pesa zako," anasema Bw Steyn.
Wakati kujibu simu za redio za kuona wanyama ni sehemu ya kazi, miongozo inapaswa kuwaelimisha wateja juu ya kuthamini mazingira kwa ujumla.
"Tunaiita safari ya Ferrari," anasema. "Ni msemo wa Afrika Kusini kwa watu ambao huenda haraka sana kutoka kwa nyati kwenda kwa tembo hadi kwa faru na kisha wanarudi nyumbani na kuiita hiyo siku nzuri."
'Serengeti ni bora zaidi'
Romina Facci, ambaye anaendesha tovuti ya 'Exploring Africa', anaonya kwamba ikiwa waongozaji wataendelea kushinikiza wanyama kwa kujazana,inaweza kuwa vigumu kuwapata.
"Ikiwa wanyama wanahisi kuwa na mafadhaiko, wanaweza kuamua kuondoka ," anasema.
Wengine wanaweza hata kuchagua kuzuia uhamiaji wa kila mwaka kutoka Serengeti kwenda Mara - moja ya vivutio vikubwa vya wanyamapori barani Afrika, wakati wanyama zaidi ya milioni wanahamia kutafuta malisho mapya.
"Katika misimu mingine, wakati mvua kubwa, wanyama wengine wa jamii swala huamua kukaa Tanzania na hawavuki Mto Mara kwenda Kenya kwa sababu hawahitaji: wanapendelea kukaa katika mazingira yenye utulivu zaidi. "
Utafiti wa mwaka 2018 ulionesha kuwa duma wanaoishi katika sehemu za Maasai Mara na msongamano mkubwa wa magari ya watalii walilea watoto wachache kuliko wale wa maeneo ya watalii wachache - hali inayotia wasiwasi kwa spishi iliyo na wanyama karibu 7,000 tu waliosalia porini.
Sensa ya kwanza kabisa ya wanyamapori nchini Kenya, iliyofanyika mapema mwaka huu, iligundua kuwa wakati idadi ya wanyama walio hatarini kupotea, kama faru mweusi na tembo, wengine, spishi ya swala, adimu wana hatari ya kutoweka Kenya.
Jerome Gaugris, mtaalam wa ikolojia ambaye anatoa ushauri wa mazingira nchini Afrika Kusini, anasema huwaelimisha waongozaji na watalii.
Anasema mipaka ya gari ambayo imekuwa mazoea ya kawaida katika mbuga za wanyama za Afrika Kusini kwa miaka inapaswa kutekelezwa nchini Kenya, ingawa anakubali ni ngumu kufanya hivyo kwenye ardhi ya umma ambapo waongozaji tofauti, waendeshaji na wakala hufanya kazi.
"Tunaruhusu gari nne wakati wakati wowote," anasema André Burger ambaye anaendesha Hifadhi ya Wanyama ya Welgevonden nchini Afrika Kusini.