Wanafunzi wa Nigeria wanaokusanya shahada kuendelea kuishi Ulaya

Modupe Osunkoya

Chanzo cha picha, MODupe Osunkoya

Baada ya maombi yake ya kazi zaidi ya 200 kutofanikiwa kupitia kwenye mtandao wa LinkedIn pekee, mwanafunzi wa Nigeria Modupe Osunkoya alijua kuwa muda wake ulikuwa unaisha wa kuongeza kipindi chake cha kuishi nchini Ubelgiji.

Huku kibali chake cha mwanafunzi kuishi Ubelgiji kikiwa kimebakiza miezi mitatu tu muda wake uishe, alikuwa amebakia na chaguo la kupata kazi au kuondoka nchini humo.

Lakini kulikuwa na chaguo jingine-kujisajili kwa stashahada ya tatu ya uzamili tangu aondoke Nigeria mwaka 2017.

"Sikujiona nikisomea shahada ya udaktari -PhD lakini kama nitakwenda nyumbani sasa, hakuna kazi inayonisubiri," aliiambia BBC mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 28.

ukosefu wa hali ya juu wa ajira- mmoja kati ya vijana watatu bila kazi-na hali ya maisha ya umasikini huwafanya Wanigeria wengi wenye elimu zaidi huamua kujaribu bahati zao za kazi ughaibuni kuliko kurejea nyumbani.

Kwa hiyo mwaka jana Bi Osunkoya alijiunga kwa ajili ya kusomea stashahada ya uzamivu -PHD nchini Estonia ambayo anaisoma sambamba na Shahada ya Uzamili nchini Ubelgiji.

Aliishia Estonia, baada ya kutopata kazi au stashahada ya uzamivu nchini Ubelgiji.

"Masomo ni njia ya ku mwisho, na kama Mungu akisema mwishowe nitaishia kupata makazi ya kudumu , kwanini nisiishi?" alisema.

Shahada yake ya uzamivu kuhusu Miji ya siku zijazo katika Chuo kikuu cha teknolojia cha Tallinn ilikuwa ya manufaa. Mwisho wa miaka minne ya utafiti anaweza kuomba kuwa mkazi wa kudumu wa Estonia.

Anapanga kuhamia katika taifa hilo la Ulaya masharikikwa ajili ya kozi, ambayo sawa na zile za Ubelgiji, hufundishwa kwa lugha ya Kiingereza.

Women, with two of them in pink skirts and black tops

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wahitimu wa Chuo kikuu wamekuwa wakipata ugumu wa kupata kazi nchini Nigeria

Bi Osunkoya ni mmoja tu kati ya wanafunzi wa Nigeria kutoka katika famili ambazo sio sehemu ya wasomi matajiri zaidi wanaosomea ughaibuni.

Mwaka jana , takriban Wanigeria 100,000 walisafiri ng'ambo kwa ajili ya masomo, kulingana na shirika la ICEF , linalofuatilia wanafunzi wa kimataifa.

Wengi wana matumaini ya kuwa wakazi wa kudumu katika nchi zinazowapokea, na kuchukua hatua moja kwa wakati mmoja kufikia lengo lao.

Kujifunza kuhusu Afrika-nchini Ubelgiji

Bonuola, (ambaye hakutaka jina lake la pili lifichuliwe) mwanafunzi mwingine Mnigeria aliyepo nchini Ubelgiji anasema: "Watu humaliza shahada ya uzamili, wanarudi kwa ajili ya stashahada ya uzamili ambayo ni chini ya kiwango chao cha elimu, hala wanasomea Astashahada za garama ya chini, yote kwa lengo la kuendelea kuwa kubakia nchini kisheria ."

Lich ya kupata shahada ya uchumi nchini Nigeria, aliamua kuanzia mwanzo alipowasili nchini Ubelgiji, akamaliza kozi ya miaka mitatu ya utawala- ili kuongeza muda wake -halafu akaendelea kufanya shahada ya uzamili katika utawala

Bado hajakata tamaa ya uwezekano wa kusomea shahada ya pili ya uzamili na shahada ya uzamivu iwapo hataweza kupya kazi itakayofungua njia ya kupata kibali cha kudumu cha kuishi Ubelgiji.

"Mimi ni Muafrika ninayesoma kuhusu Afrika nchini Ubelgiji na inaniudhi sana ," alisema mwanafunzi wa tatu , Ifeoma, (sio jina lake halisi) ambaye kwa sasa anasomea shahada ya pili ya uzamili tangu alipowasili nchini humo mwaka 2019.

"Siichukulii kwa umakini, ni kupoteza muda tu huku nikifikiria la kufanya ,"aliongeza.

An African man sculpture is displayed at the Museum of Central Africa (RMCA) in Tervuren in the suburbs of Brussels on October 9, 2013.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Ubelgiji ina historia tata kama koloni la Afrika

Ada ya masomo kuwa ya chini hadi euro 1,000 ($1,200; £850) kwa mwaka na kiwango cha chini cha garama ya mwanafunzi kuishi nchini Ubelgiji ni ya chini, ikilinganishwa na mataifa mengine ya Ulaya, vimeifganya nchi hiyo kuwavutia Wanigeria wengi wanaotoka katika familia zenye kipato cha wastani.

"Garama ya maisha ni ya chini-unaweza kupata makazi kwa euro 300 kwa mwezi ," sanasema Bi Osunkoya.

Sawa na wengine, aliondoka nyumbani akiwa na pesa za kulipa ada ya muhula mmoja na pesa z kumuwezesha kuishi kwa wiki kadhaa. Alijilipia elimu yake kwa kufanya kazi hadi saa 20 kwa wiki, kwani alikuwa anaruhusiwa kufanya hivyo , na kulipwa hadi euro 1,000 kwa mwezi.

Lakini wanafunzi kutoka familia zenye uwezo wa kifedha hupendelea kusomeakatika nchi zinazozungumza kiingereza kama vile Canada,Uingereza na marekani, ambako kuna wanafunzi wa Nigeria zaidi 13,000.

Canada inapendelewa zaidi ya Uingereza

Idadi ya wanafunzi wa Nigeria ya kwenda nchini Uingereza imepungua - kutoka wnafunzi 18,020 katika mwaka 2013/14 hadi wanafunzi 10,540 katika mwaka 2017/18, kiwango hiki kikiwa ni sawa na 41% . kulingana shirika la ICEF.

Sababu moja ya hili ilikuwa ni kuondolewa kwa kibali(visa)ambayo inawaruhusu wanafunzi wa kigeni kufanya kazi kwa miaka miwili baada ya kumaliza masomo.

Hilo pamoja na ada nafuu, mchakato rahisi wa upatikanaji rahisi wa kibali Tnjia ya wazi ya kupata stashahada ya uzalimi na kibali cha makazi ya kudumu vimewavutia wanafunzi wengi zaidi.

Students outside the gate of University of Lagos

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Baadhi ya wanafunzi nchini Nigeria kabla ya kuhamia ng'ambo kwa masomo yao

Sawa na wanafunzi wenye wa kigeni, wanafunzi wa Nigeria hulipa zaidi ya mara tatu ya ada inayolipwa na wanafunzi wa Uingereza au wale wanaotoka katika nchi za Muungano wa Ulaya.

Lakini inakuwa vigumu kwa Wanigeria kupata kazi za ofisini nchini Nigeria, na hata nchi kama Ubelgiji ambako lugha ya kiingereza haitumiwi.

Kifulama, Kifaransa na kijerumani ndio lugha rasmi na wengi miongoni mwa waajiri wanataka wahitimu wanaoweza kuzungumza walau lugha mbili.

Sawa na wanafunzi wengine wa Nigeria, Bi Osunkoya anazungumza vyema lugha ya Kiingereza pekee, ingawa anaelewa kifulama kidogo.

"Hata kama una kibali cha kusoma zaidi utakuwa unaushindani wa kazi na wenyeji ambao wanazungumza lugha bora zaidi kuliko wewe ,"anasema.

Baadhi ya wanafunzi pia wanalalamikia ubaguzi wa rangi, huku wengine wakisema wamekuwa na elimu ya upindukia na bado hawana uzoefu.

Wiki iliyopita, Ubelgiji ilibadili sheria yake ya uhamiaji ili kuwaruhusu wanafunzi kuishi kwa walau mwaka mmoja kwa kutumia kibali cha muda ili kutafuta kazi.

Lakini Bonuola anasema hatachagua hilo, kwasababu wakati mmoja aliwahi kujisajili , wakati huu hataweza kurejea shuleni kwa shahada zaidi kama hatapata kazi.

"Ilikuwa ni kama kujipata umenaswa katikati ya mwamba na eneo gumu ," alisema.