Tetesi za soka Ulaya Jumanne tarehe 31.08.2021: Kounde,Emerson,Mbappe, Bellerin, Kounde, Hudson-Odoi, Tagliafico, Edouard

Sevilla wamekataa ofa ya "kutoridhisha" ya Chelsea kwa beki wa Ufaransa Jules Kounde.

Klabu ya Uhispania imesimama kidete juu ya ada inayohitajika kwa Kounde, ikisisitiza kwamba hataruhusiwa kujiunga na Blues kwa chini ya euro milioni 80.

Mkurugenzi wa michezo wa Sevilla Monchi, alithibitisha Katika mkutano na waandishi wa habari ofa hiyo ilikuwa imekataliwa kwa kijana huyo wa miaka 22.

Tottenham wanatarajia kumsajili mlinzi wa Brazil Emerson Royal kutoka Barcelona baada ya kukubali malipo ya Euro 30m (Pauni 25.8m).

Mchezaji huyo wa miaka 22 huko Betis kwa vipindi viwili, akifunga mabao matano katika michuano 79.

Emerson, aliyejiunga na Barca kutoka Atletico Mineiro ya Brazil mnamo 2019, alishiriki kwenye kampeni ya Brazil ya fainali ya kombe la Copa America msimu huu wa joto

Anatarajiwa kushindana kuipata nafasi ya beki wa kulia huko Spurs na Japhet Tanganga na Matt Doherty.

Viongozi hao wa Ligi Kuu wanataka kumuachilia beki wa pembeni Serge Aurier.

Emerson alicheza dakika nyingi kuliko mchezaji yeyote wa Betis msimu uliopita walipomaliza katika nafasi ya sita kwenye La Liga na kufuzu kwa Ligi ya Europa.

Ameshinda mataji manne na Brazil tangu aanze mechi yake ya kwanza mnamo 2019.

Real Madrid imejiondoa katika mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kutoka Paris St-Germain kwasababu vilabu haviwezi kukubali ada.(RMC Sport - in French)

Hata hivyo, klabu hiyo ya Uhispania inatarajia kuipiku PSG katika mbio za kumsajili kiungo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 18 Eduardo Camavinga kutoka Rennes. (Canal+ via Get French Football News)

Manchester City hawatarajii yeyote zaidi ama kuingia au kuondoka kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa baada ya kumfungia kipa wa Brazil Ederson, 28, kwa mkataba mpya. Kiungo wa Ureno Bernardo Silva, 27, alikuwa ndiye gumzo katika ofa kutoka AC Milan, lakini hakufurahishwa na hatua hiyo. (Times - subscription required)

Barcelona watajaribu kumsajili beki wa kulia wa Arsenal na Uhispania Hector Bellerin, 26, ikiwa mlinzi wa Brazil Emerson Royal, 22, ataondoka Nou Camp na kujiunga na Tottenham. (Mundo Deportivo - in Spanish)

West Ham wamefikia makubaliano ya maneno na Ajax kumsaini beki wa kushoto Nicolas Tagliafico, ingawa kukamilisha makubaliano hayo kabla ya tarehe ya mwisho uhamisho , Jumanne itakuwa vigumu na mchezaji huyo wa miaka 28 ambaye sasa hivi yuko katika jukumu la kimataifa na Argentina. (Telegraaf - in Dutch)

Hata hivyo, kuna wasiwasi wa Hammers kuendeleza mpango wa kutafuta makubaliano na Tagliafico licha ya beki huyo kutolewa kwa klabu hiyo na mawakala wengi. (Athletic)

Chelsea wamemuambia ajenti wa beki wa kati wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde watafanya jaribio la mwisho kumsajili mchezaji huyo wa miaka 22. (ABC Sevilla, via Sport Witness)

Leicester City wameonyesha nia kwa winga wa Chelsea na England Callum Hudson-Odoi, 20, ambaye pia amehusishwa na Borussia Dortmund. (football.london)

Blues pia wanataka kumchukua kiungo wa Atletico Madrid raia wa Uhispania Saul Niguez, 26, kwa mkopo lakini mabingwa wa La Liga wanataka kujumuisha kifungu ambacho kitaifanya kuwa mkataba wa kudumu kwa £ 34m. (Goal)

Burnley wapo kwenye mazungumzo ya kumleta mlinzi wa Swansea City na Wales Connor Roberts, 25, Turf Moor. (WalesOnline)

Mshambuliaji wa Wolves Adama Traore, 25, amemuajiri wakala Jorge Mendes kumsaidia kupata uhamisho Tottenham. Mchezaji huyo wa Uhispania anataka kuungana tena na kocha wake wa zamani Nuno Espirito Santo. (Footballer Insider)

Wolves wamewasilisha dau la pauni milioni 8.6 kumsajili mlinzi wa Marseille na Croatia Duje Caleta-Car lakini timu hiyo ya Ligue 1 inataka pauni milioni 12.9 kabla ya kumruhusu mchezaji huyo wa miaka 24 aondoke. (Foot01 - in French)

Juventus wameamua kutotafuta mkataba kwa kiungo wa kati wa Barcelona na Bosnia-Herzegovina Miralem Pjanic, 31, huku kilabu cha Serie A kikikaribia kumsajili Mholanzi Mohamed Ihattaren mwenye umri wa miaka 19 kutoka PSV Eindhoven. Pjanic, ambaye alikaa Juventus kwa miaka minne kabla ya kujiunga na Barca mnamo mwaka 2020, ni mmoja wa wachezaji kadhaa ambao kilabu hicho cha Kikatalani wanajaribu kumuuza kabla ya tarehe ya mwisho ya Jumanne. (Goal)

Brentford imetoa ofa ya pauni milioni 13 kwa beki wa Gremio, Mbrazil Vanderson, 20, ambaye pia amevutia AC Milan msimu huu. (Goal)

Kiungo wa kati wa Chelsea Tino Anjorin anakaribia kujiunga na Lokomotiv Moscow katika mkataba wa mkopo ambao unajumuisha chaguo la pauni milioni 17 kumnunua Mwingereza mwenye umri wa miaka 19. (Goal)