Transfer Deadline Day: Tarehe ya mwisho ya usajili Uingereza na Uropa ni lini?

Klabu za Ligi Kuu ya Primia zimetumia karibu £ 1bn katika dirisha la uhamisho ambalo lilibadilika na kuvutia zaidi wakati Manchester United ilipokubali makubaliano ya kushangaza ya kumsajili tena Cristiano Ronaldo kabla ya tarehe ya

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno alikuwa akionekana kuwa tayari kujiunga na wapinzani wao Manchester City, lakini mabadiliko makubwa ya matukio Ijumaa iliyopita yalisababisha Ronaldo kushawishika kurudi Old Trafford baada ya kuondoka kilabu hiyo miaka 12 iliyopita.

Pia kilichovutia wakati wa usajili, Ole Gunnar Solskjaer hatimaye alimaliza dau la pauni milioni 73 kwa Jadon Sancho kutoka Borussia Dortmund, pamoja na uhamisho wa pauni milioni 34 kwa mshindi wa Kombe la Dunia la Ufaransa Raphael Varane kutoka Real Madrid.

Mabingwa wa Ligi ya Primia, City huenda walimkosa Ronaldo, lakini wakavunja rekodi ya Uingereza juu ya mchezaji mmoja kwa kumsajili kiungo wa kati Jack Grealish kutoka Aston Villa kwa pauni milioni 100.

Vilabu za Ligi Kuu ya Primia zimetumia pauni milioni 962 katika uhamisho wa wachezaji hadi sasa, ikimaanisha kwamba kutakuwa na haja ya kuongeza kiwango kikubwa tu cha fedha kufikia kile kilichotumika mwaka katika kipindi cha dirisha la usajili cha Pauni bilioni 1.3.

Mabingwa wa Ulaya Chelsea pia walimsajili tena mshambuliaji Romelu Lukaku kutoka kwa mabingwa wa Serie A Inter Milan kwa dau kubwa la pauni milioni 97.5, makubaliano ya kima cha juu zaidi wakati wa kipindi cha dirisha la usajili.

Arsenal wametumia karibu pauni milioni 140 kwa kuongeza kikosi nguvu ikiwemo pauni milioni 50 kwenda kwa Brighton kwa ajili ya mlinzi wa kimataifa wa England Ben White, pauni milioni 30 kwa kiungo wa kati wa Real Madrid Martin Odegaard na pauni milioni 24 kwa mlinda mlango Aaron Ramsdale kutoka Sheffield United.

Gunners pia wamepunguza pauni 200,000 kwa wiki katika mshahara huku winga Mbrazil Willian kandarasi yake ikikatizwa katika makubaliano ya pande zote mbili kuwezesha kurejea kwa kilabu cha kwanza cha Corinthians.

Liverpool ilichochea kifungu cha kumruhusu kuondoka kwa pauni milioni 36 kwa mlinzi Ibrahima Konate kutoka RB Leipzig, wakati Villa ilitumia pesa za Grealish kwa ununuzi wa mshambuliaji Danny Ings, kiungo wa kati Emiliano Buendia na winga Leon Bailey.

Dirisha la uhamisho tayari limeweka kumbukumbu kwa Lionel Messi akifanya jambo lililodhaniwa kwamba haliwezekani kwa kuondoka Barcelona na kujiunga na Paris St-Germain baada ya mkataba wake kumalizika Nou Camp.

Mkataba huo peke yake ungeweza kuibuka na ushindi katika usajili kwa timu hiyo ya Ligue 1, lakini pia ilivutiwa na kipa wa Italia Gianluigi Donnarumma, mlinzi wa Uhispania Sergio Ramos na mchezaji wa kimataifa Mholanzi Georginio Wijnaldum ... wote kwa uhamisho wa bure.

Je tarehe ya mwisho ya usajili mwaka huu ni lini?

Dirisha la uhamisho kwa Ligi Kuu ya Primia, Ligi ya Soka ya Uingereza na Uskochi yaani Scotland linafungwa Jumanne, Agosti 31, saa 23:00 BST.

Na mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 zinaanza siku mbili baadaye kwa hivyo, huenda wachezaji wasikutane na wenzao wapya waliosajiliwa hadi wiki inayofuata watakaporudi kwenye vilabu vyao.

Vipi kuhusu Ulaya?

Dirisha la uhamisho wa ligi kuu barani Ulaya pia linafungwa Jumanne.

Huko Ujerumani linafungwa saa 17:00 BST, wakati Uhispania, Italia na Ufaransa linafungwa saa 00:00 BST.

Je! Itakuwa siku yenye shughuli nyingi?

Mchezaji mmoja ambaye hatakuwa anahamia kwengineko ni nahodha wa England Harry Kane, ambaye alikuwa akihusishwa sana na kuhamia Manchester City, lakini badala yake aliahidi kubaki Tottenham.

Hata hivyo, makubaliano ya kiwango cha juu na ghali zaidi ya kipindi hiki cha dirisha la usajili huenda bado yakajitokeza kwasababu Real Madrid inataka kumsaka mshindi wa Kombe la Dunia raia wa Ufaransa Kylian Mbappe kutoka PSG baada ya kutoa kandarasi ya pili ya pauni milioni 146.

Klabu hiyo ya Ufaransa inaripotiwa kujaribu kufanya juhudi zake zote dakika ya mwisho kumsaini Erling Braut Haaland kutoka Dortmund kama mbadala wa Mbappe.

Kulikuwa na usajili wa siku 12 tu za siku za mwisho za Ligi Kuu ya Primia mwaka jana - idadi ndogo zaidi katika miaka ya hivi karibuni - sasa je, tutashuhudia mikataba zaidi ikikamilishwa wakati huu?

Chelsea inayotafuta kuchukua mataji inaweza kuwa kilabu cha Ligi ya Primia yenye shughuli nyingi siku ya Jumanne na uwezekano wa kusajili au kuondoka kwa wachezaji.

Blues wanaonekana kama watahitajika kulipa kifungu cha kuruhusiwa kuondoka cha pauni milioni 68 ili kumsajili Jules Kounde wa Ufaransa kutoka Sevilla huku Borussia Dortmund wakionekana kuwa na nia ya kusajili winga Callum Hudson-Odoi.

Mshambuliaji wa Everton Moise Kean anaweza kuchukua nafasi ya Ronaldo katika klabu ya Juventus, wakati Toffees inaweza kumleta mshambuliaji wa zamani wa Newcastle Salomon Rondon kwa mkopo - na mchezaji wao wa kimataifa wa Colombia James Rodriguez anaweza kurudi kwa kilabu cha zamani cha Porto kwa mkopo.

West Ham inaendelea kuhusishwa na uhamisho wa kudumu kwa mshambuliaji wa Manchester United Jesse Lingard, ambaye alifurahia mafanikio ya uhamisho wa mkopo msimu uliopita.

Leicester wanafanya mazungumzo na RB Leipzig juu ya makubaliano ya kudumu kwa Ademola Lookman, wakati Wolves wana nia ya kumchukua Sven Botman kutoka Lille.