Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwanini Marekani taifa lenye uwezo mkubwa zaidi duniani limeshindwa kuangamiza Taliban Aghanistan?
Baada ya Marekani kurejea Afghanistan, juhudi zimekuwa zikifanyika kutafuta jawabu la swali hili kubwa: Kwanini nchi yenye nguvu duniani, yenye jeshi la kisasa, teknolojia za kisasa na jeshi la kisasa la anga, haiwezi kuiangamiza Taliban?
Wasomi na wadadisi wa Marakani wana wasiwasi kuhusu kwanini Marekani inashindwa vita vya kisasa.
Swali hili ni muhimu: Je Ushiriki wa Marekani nchini Afghanistan utakoma baada ya kuondoka kwa vikosi vya nchi hiyo Jumanne hii, hasa China na Urusi zitakapoendelea kutengeneza mashirikiano na Taliban?
Katika kuitetea Marekani, baadhi wanasema kwamba Marekani imekuwa na mafanikio makubwa nchini Afghanistan na Iraq.
"Jeshi la Marekani lilimpata na kumuua Osama bin Laden, likaisambaratisha al-Qaida, likawaua ama kuwakamata viongozi wa juu wa," anasema Profesa Tom Cassidy wa chuo kikuu cha Chicago.
Miundo mbinu ilitengenezwa Afghanistan, watoto wa kike walipata fursa ya kupata elimu mashuleni. Magaidi hatari kama Islamic State (IS) walisambaratishwa nchini Iraq, na ikahitimisha utawala wa madikteta kama Saddam Hussein na kanali Gaddafi huko Libya. Je haya ni mafanikio madogo?"
Vita vitano vikubwa vya Marekani baada ya mwaka 1945
Watu wengi Marekani wanaodhani kwamba Marekani imeshindwa kuondoa mzizi wa ugaidi katika nchi za Afghanistan, Syria, Iraq na Yemen. Ushindi wa kundi la Taliban na kurejea kwao madarakani ni ushahidi tosha ya kuefli kwa Marekani.
Kihistoria mpaka kufikia mwaka 1945, Marekani ilikuwa imeshinda vitakaribu vyote vikubwa ilivyoshiriki, lakini tangu mwaka 1945, Mafanikio ya Marekani yamekuwa madogo kwenye vita.
Tangu mwaka 1945, Marekani imepigana vita vitano vikubwa - Korea, Vietnam, vita ya Gulf, Iraq na Afghanistan, na vita vingine vidogo vidogo kama kule Somalia, Yemen na Libya.
Ukiacha vita ya Gulf mwaka 1991, ambayo unaweza kuhesabu Marekani ilishinda, vita vingine vyote Marekani imekuwa ikhangaika.
Carter Malkasian amefanya kazi miaka mingi kwenye utawala wa Marekani huko Afghanistan, utaona haya ukirejea kile alichoandika 'The American War in Afghanistan-a History' na kuchapishwa Julai mosi.
Kwa nini Marekani inashindwa vita?
Kitabu hiki kimeandika, vita kabla ya mwaka 1945 vilikuwa ni baina ya nchi nan chi, Marekani ilikuwa inashinda mar azote vita vya aina hii.
"Lakini imeshindwa vita vyote vya kisasa ambapo wapiganaji wanakuwa ni waasi, wasio na nguvu kijeshi lakini ni watu wa kujitoa."
Kushindwa huku ni tofauti kidogo, namna ambavyo wapiganaji wa Marekani wameondoka Benghazi, Somalia, Saigon na sasa Kabul katika namna isiyo na msaada, inafanya kushindwa huko kwa Marekani ni kwa aibu.
Ssa kwanii Marekani inashindwa vita? Watalaam wanasema zipo sababu nyingi za kwanini ni muhimu kufahamu utamaduni wa wenyeji.
"Mapigano kama Afghanistan, Iraq, Syria na Libya yalikuwa zaidi ni vita vya wenyewe kwa wenyewe,"anasema profesa Dominic Tierney, mtaalam wa sera kutoka chuo cha Swarthmore College, alipozungumza na BBC India. Nguvu haikupi uhakika wa kushinda vita vya aina hii, hasa inapotokea nchi kama Marekani haifahamu kuhusu utamaduni wan a kujikuta inakabiliana na adui ambaye ana uelewa mkubwa na amejitoa sana."
Kuhusu vita vya Iraq Tierney anasema "Tulidhani tungeweza kuisaidia Iraqi, lakini hatukuweza, tulikuwa wajinga na wenye kiburi na tunawajibika kwa madhira waliyopata watu, ambayo hayakuwa mazuri kwa kila upande," aliandika katika chapisho hilo
Profesa Aftab Kamal Pasha, mtaalam wa masuala ya Asia ya magharibi katika chuo kikuu cha Jawaharlal Nehru University, nay eye anaonyesha kuwa utamaduni unaiangusha marekani.
Katika mazungumzo yake na BBC Hindi, anasema, "Wamarekani hawajui utamaduni wan chi zingine na hawataki kuelewa.
Marekani imejifunza nini kutokana na kushindwa huku kwenye vita?
Uongozi wa Marekani hakujifunza katika vita ya Saegon, Vietnam. Ikaendsha shughuli za kijeshi Somalia mwaka 1993 na kufanya makosa yale yale.
Kitendo cha miili ya askari wa Marekani kuburutwa katika mitaa ya mji wa Mogadishu kilinaaniwa doniani kote. Wamarekani walikasirishwa sana na kitendo hicho. Wengi walihuzunishwa. Hiyo ikawa kama mwanzo mpya wa Marekani katika shughuli za kijeshi barani Afrika.
Oktba 1993, vikosi vya Marekani vikashambulia mji mkuu wa Somali Mogadishu, kwa lengo la kumkamata mbabe wa kivita Somali, Jenerali Mohamed Farah Adid, na washirika wake,lakini jeshi la Marekani lilikabiliwa na upinzani mkali.
Helkopta bili ziliangushwa, waajeshi 18 wa marekani na wawili wa Umoja wa mataifa waliuawa.
Profesa Aftab Kamal Pasha, kutoka chuo kikuu cha Jawaharlal Nehru, anasema "Kujenga nchi, demokrasia, haki za binadamu na elimu kwa wanawake ni visingizio tu huko Afghanistan na Iraq suala kubwa ni kuzizuia China na Urusi na kupunguza ushawishi wa Urusi huko Asia ya kati."
Je Marekani itarejesha vikosi vyake Afghanistan?
Kwa mujibu wa Profesa Pasha Marekani haijiingiza kwenye suala hilo moja kwa moja. Anaongeza, "Marekani imejiondoa Pakistan katika miaka michache iliyopita. Marekani haijaifurahia Pakistan.
Marekani sasa itahitaji kiogozi kama rais wa zamani na amerijeshi mkuu Jenerali l Pervez Musharraf ambaye aliungana na Marekani wakati wa utawala wa Rais George Bush ulipovamia Afghanistan mwaka 2001."
"Msukumo utaongezeka dhidi ya waziri mkuu Minister Imran Khan, kwamba anaweza kumalizia muda wake madarakani ama la," aliongeza.
"Rais Suo-Daydon hakubaliani na vita nyingine kubwa Afghanistan, lakini kuna mazingira ambayo Marekani inaweza kujiingiza tena, moja wapo ni eneo la misaada ya kibinadamu, mazingira mengine ni kama utaibuka kwa vikundi vya kigaidi," nasema Profesa Dominic Tierney.