Mbwa wa kijeshi:Mbwa hawa walikuwa 'wanajeshi' hodari

PDSA

Chanzo cha picha, PDSA

Kati ya sifa zote nzuri anazo mbwa, labda ni uaminifu wao ambao unawapendeza sisi zaidi ya yote - na kwa sababu nzuri.

Hakuna uhaba wa visa juu ya mbwa kuweka maisha yao wenyewe kwenye mstari wa mbele kulinda, kutetea, au kuokoa wanadamu.

Mashujaa hawa wa kijeshi walichukua jukumu hilo kwa kiwango kipya kabisa wakati waliposajiliwa katika Vikosi vya Wanajeshi na walijitolea kuokoa maisha .

Hawa ni baadhi ya mbwa maarufu sana kuwahi kuhudumu katika jeshi.Wengi walikufa vitani na hata kuna mbwa wenye vyeo vikubwa jeshini .

Kuno

PDSA

Chanzo cha picha, PDSA

Kuno alikuwa mbwa wa kijeshi ambaye alikoa maisha ya wanajeshi wa Uingereza waliokuwa wakipigana dhidi ya wanamgamabo wa Al qaeda nchini Afghanistan .Alipewa tuzo ya Victoria Cross kwa ushujaa wake .

Wakati wa shambulio hilo ,mbwa huyo wa Belgian Malinois alikabiliana na mpiganaji mmoja wa kundi hilo na alipigwa risasi mara mbili miguuni .

Alfie na AJ

PDSA/PA WIRE

Chanzo cha picha, PDSA/PA WIRE

Alfie na AJ alihudumu katika jeshi la Uingereza kwa miaka sita na walipewa tuzo za OBE baada ya kustaafu .

Alfie na AJ walitambulika sana katika majukumu yao ya kunusa na kusaka vilipuzi

Treo

dg

Chanzo cha picha, Telehraph

Nchini Uingereza kulikuwa na mbwa wa kunua bomu kwa jina Treo na alipewa heshima kubwa zaidi ya jeshi la wanyama nchini Uingereza. Treo alipokea medali ya Dickin kwa kugundua mabomu mengi barabarani na kuokoa mamia ya maisha.

Sarbi

Mbwa huyo mweusi kwa jina Sarbi alikua mnyama wa 2 tu wa Australia kupokea tuzo ya Royal Society for the Prevention of Cruelty to Animals, tuzo ya kifahari ya ushujaa wa wanyama katika taifa hilo.

DG

Chanzo cha picha, DG

Sarbi alipelekwa kama mbwa anayegundua bomu mnamo Septemba 2008 wakati kitengo chake kiliposhambuliwa na wanamgambo wa Taliban.

Wanajeshi tisa, pamoja na mtunzi wa Sarbi, walijeruhiwa katika shambulio hilo. Sarbi alitengwa na kitengo hicho na alinusurika mwaka mzima ndani ya kitovu cha Taliban kabla ya kupatikana katika kituo cha doria cha kaskazini mashariki mwa Uruzgan na kuungana tena na msimamizi wake

Lex

Mbwa huyu wa kushangaza alionyesha uaminifu na ushujaa wake katikati ya vita. Wakati alipelekwa Fallujah na msimamizi wake, Cpl. Dustin Lee, wawili hao walipigwa na bomu la kutegwa kano ya barabara. Lee alijeruhiwa vibaya katika shambulio hilo.

OMD

Chanzo cha picha, OMD

Lex, mwenzake mwaminifu, alipigwa na kifusi, lakini aliweza kutambaa kwa Lee na kulala juu yake, akimlinda Lee hadi madaktari walipofika.wanajeshi wengine walilazimika kumvuta Lex ili Lee aweze kuhudumiwa