Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 21.08.2021: Mbappe, Ndombele, Sarr, Duarte, De Jong, Diallo, Odegaard, Ramsdale

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 22, yumo kwenye orodha ya Man united ya wachezaji wanaolengwa kusajiliwa msimu ujao wa joto. (ESPN)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 24, ameiambia Tottenham kuwa yuko tayari kuondoka klabuni humo. (The Athletic - subscription required)
Tottenham wanakaribia kumsaini kiungo wa Metz na Senegal Pape Matar Sarr, 18(90min)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mlinzi wa Ureno na Granada Domingos Duarte, 26, pia analengwa na Tottenham (Express)
West Ham wanaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Sevilla na Uholanzi Luuk de Jong, 30. (90min)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Ujerumani Leon Goretzka, 26, yuko mbioni kukomesha uvumi unaomuhusisha na kuhamia Manchester United kwa kusaini kandarasi mpya Bayern Munich. (Goal)
Sheffield United inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Atalanta ya Serie A kwa mkataba wa mkopo kwa winga wa Manchester United na Ivory Coast Amad Diallo, 19(TuttoAtalanta, in Italian)
Manchester United wanafanya mazungumzo na wakala wa kiungo wa kati wa Monaco mwenye umri wa miaka 21 Aurelien Tchouameni juu ya uhamisho msimu huu wa joto. . (Mirror)
Leeds wamekubaliana masharti ya kibinafsi na winga wa Uholanzi wa Club Brugge Noa Lang, 22. (Voetbal Belgie, in Dutch)

Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa kushoto wa Uingereza na Manchester United, Brandon Williams, 20, aliripotiwa kupata kufantiwa vipimo vya matibabu huko Norwich Ijumaa. (Football Insider)
Inter Miami wana uhakika wa kuipiku Newcastle kwa kumsaini mchezaji wa wa Brazil Evtander, 23(Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal imemsajili kiungo Martin Odegaard kutoka Real Madrid kwa pauni milioni 30 wakati kipa Aaron Ramsdale akimaliza matibabu kabla ya kuhama Sheffield United.
Mchezaji wa kimataifa wa Norway Odegaard, 22, alihudumia nusu ya pili ya msimu uliopita kwa mkopo kwenye uwanjani Emirates.
Alicheza mechi 20 kwenye mashindano yote na alifunga mabao mawili.
Mkataba Ramsdale una thamani ya pauni milioni 24 pamoja na pauni milioni 6 zaidi katika nyongeza.














