Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Barua iliyotumwa miaka 30 iliyopita hatimaye yamfikia mwenyewe
Barua iliyotumwa miaka 30 iliyopita kutoka Amerika Kusini mwaka 1991 hatimaye imemfikia mlengwa.
Neil Crocker, ambaye alikuwa akifanya kazi katika jeshi la majini la Uingereza, alikuwa akirejea kutoka mjini Malvinas/ Falklands akiwa kwenye manuari ya HMS Cumberland, na alipowasili nchini Chile alimuandikia barua baba mkwe wake.
Mapema wiki hii, barua hiyo iliwasilishwa katika sanduku la posta la baba mkwe wake nyumbani Portland Uingereza.
Crocker anasema "alishangaa" sana kuona tena barua aliyotuma miongo mitatu iliyopita.
Meli aliyokuwa akisafiria ilikuwa ikirejea kutoka ziara ya miezi mitatu huko Malvinas / Falklands na ilitia nanga kwa siku tano katika mji wa Valparaíso, pwani ya Chile.
Crocker alisema "bila kufafanua" kwamba anakumbuka akiandika na kutuma barua akiaelezea jinsi ''hali ya hewa na fukwe za mji huo zilivyokuwa nzuri."
"Nilituma barua kadhaa nyumbani na ukweli ni kwamba sikuwahi kuzifikiria tena."
Anasema baba mkwe wake aliye na umri wa miaka 89 "alichanganyikiwa kidogo"alipo pokea barua hiyo.
Barua hiyo iliyokuwa imetumwa "London 1991" ilionesha muhuri ya kuashiria iliwasili Uingereza wakati huo.
"Barua hiyo iliyochukuwa takriban miaka 30 kumfikia mlengwa hatimaye imewesili - ni kisa cha kushangaza."
Barua hiyo ilikuwa na stampu ya ya pence 22 za Chile pia ilikuwa na matundu ambayo Crocker anashuku huenda ilikuwa ya pini iliyotumiwa kudungilia mahali kwenye ubao wa habari maelezo.
''Sijui ilikuwa wapi lakini ni kitu cha kushangaza," alisema.