Abba Kyari: Kachero wa Nigeria anayesakwa na Marekani

Abba Kyari anasifika sana nchini Nigeria kwa kuwa "polisi mchapa kazi".
Ni afisa wa polisi aliyetunukiwa tuzo nyingi zaidi kwa kuchunguza kesi kubwa za uhalifu. Na hujumuika sana na wanasiasa na watu mashuhuri.
Mienendo ya Bw. Kyari sasa inachunguzwa tangu vyombo vya sheria vya Marekani kuonyesha kwamba anatafutwa kuhusiana na madai ya kuhusishwa na mshawishi na tapeli wa Instagram Ray Hushpuppi.
Afisa huyo wa polisi amekanusha kufanya hatia yoyote.
Wakosoaji wa Bw. Kyari, hawajatilia shaka madai hayo. Wanasema afiso mwenye miaka 46 - aliyetambuliwa na Rais Muhammadu Buhari kama shujaa - aliwahi kukabiliwa na madai ya ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu nchini Nigeria.
Bw Kyari, ambaye anashikilia cheo cha naibu kamishena wa polisi amepuuzilia mbali madai hayo akisema ni ya uwongo na kwamba hakuna hatua yoyote ishawahi kuchukuliwa dhidi yake kuhusiana na madai hayo.
Kusimamishwa na polisi
Ken Henshaw, mkuu wa shirika la kutetea haki la We The People, amesema Bw. Kyari had been rewarded by a system based on patronage which, in some cases, even punished people with integrity.
"Madai dhidi yake yanalingana na yale ambayo yametolewa dhidi ya polisi wa Nigeria, na maafisa wake wa ngazi za juu siku zilizopita, "alisema Bw Henshaw.
Lakini Kamishena wa polisi wa Nigeria amelazimika kumsimamisha kazi Bw. Kyari. Hatua ambayo inajiri baada ya Marekani kutangaza wiki iliyopita kwamba imeanzisha mashtaka dhidi yake kufuatia madai kuwa aliwezesha malipo kwa wafanyikazi wa polisi wa Nigeria kutoka Hushpuppi, ambaye jina lake halisi ni Ramon Abbas.
BBC imewasiliana na Bw. Kyari kupata tamko lake.

Chanzo cha picha, Hushpuppi/Instagram
Hushpuppi - ambaye alikuwa na mashabikii milioni 2.4 kwenye Instagram - alikiri mashtaka ya utapeli wa pesa huko Marekani baada ya kusafirishwa kutoka Dubai mwaka jana.
Akijinadi kama mwanabiashara katika jimbo la Ghuba , Mnageria huyo mwenye umri wa miaka 37-mara nyingi aliweka mtandaoni picha za maisha yake ya kifahari na alikuwa na kitengo cha video alichokiita Flexing - lugha ya mtandao wa kijamii inayoashiria kujigamba.
Lakini alikuwa sehemu ya wahalifu wa kimtandao ambao waliwatapeli watu na mashirika karibu dola milioni 24, nyaraka za mahakama zilidai.
'Pesa za Hushpuppi zilikuwa za nguo'
Maafisa wa Marekani wanadai katika hati ya kiapo kwamba Hushpuppi alimfanya Bw Kyari amkamate na kumzuila Vincent Chibuzor, ambaye alikuwa wametofautiana naye.
Bw. Kyarianadaiwa kumtumia Hushpuppi maelezo ya akauti ya benki kulipia kukamatwa huko,taarifa ilisema.
Katika majijibu ambayo yamefutwa katika ukurasa wa Facebook yalielezea kuwa madai hayo ni ya "uwongo" na kusema kwamba Hushpuppi alikuwa analipia nguo aliyokuwa ameshonewa.
"Aliona nguo za kinyumbani na kofia katika ukurasa wa mtandao wa kijamii na kuzipenda," alisema katika ujumbe wa Facebook, akiongeza kuwa Hushpuppi alituma pesa za kushonewa nguo.
Hati ya mahakama ya Marekani iliyowasilishwa na FBI inaonyesha maelezo ya madai ya mazungumzo ya WhatsApp kati ya polisi na yule mtu maarufu wa utapeli wa Instagram.
Ujumbe huo unadai kwamba Hushpuppi alilipa naira milioni 8 sawa na (dola 19,000; Pauni 14,000) kwenye akaunti zilizobainishwa na polisi wa Nigeria ambayo maelezo yao yalitolewa na Bw Kyari, kumzuilia Bw Chibuzor.
'Hakuna mtu aliyedai pesa'
Katika ujumbe mmoja, Hushpuppi anadaiwa kusema: "Mkuu nifahamishe jinsi nitakavyowasilisha pesa kwa maafisa wako. Nataka wamchukulie hatua kama mwizi aliyejihami," ambapo Bw. Kyari aliripotiwa kujbu: "SAWA nitakutumia maelezo yao."
Bw. Kyari pia amekanusha kufuta ujumbe aliyoweka Facebook.
"Hakuna mtu aliyedai pesa yoyote kutoka kwa ... Hushpuppi na hakuna mtu aliyepokea pesa yoyote kutoka kwake."
Badala yake alisema, alikuwa akijibu ombi la dharura kutoka kwa Hushpuppi ambaye alidai kulikuwa na tishio lililotolewa dhidi ya familia yake.
Kuwakomboa wtoto waliotekwa
Bw. Kyari ni afisa wa polisialiyepewa tuzo nyingi zaidi kuliko maafisa wengine wowote nchini Nigeria.
Alipokea tuzo ya rais ya ushujaa kutoka kwa Bw. Buhari mwaka 2016 baada ya kitengo chake kuwakomboa wasichana watatu wa shule waliotekwa mjini Lagos.
Pia alitunukiwa na serikali ya jimbo la Lagos, ambapo alipata tuzo ya utendakazi mwema kwa miaka mitatu mtawalio kati ya 2011 na 2013.
Kitengo chake "kinategemewa" sana hasa katika uchunguzi wa kesi mashuhuri.
Wakati msafara wa gavana wa jimbo la Benue ulipovamiwa mwezi Machi na watu wanaoshukiwa kuwa wafugaji , walipelekwa kuwasaka washambuliaji hao.
Timu ya Bw. Kyari pia ilitumiwa wakati mama yake Ngozi Okonjo-Iweala, Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO), alitekwa nyara mwaka 2015.
Ametumia nguvu ya mitandao wa kijamii kuonesha kuangazia ufanisi wake na mtindo wa maisha, unaweza kufikiria ni mshawishi wa Instagram
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Instagram ujumbe
Ukurasa wake unaangazia jinsi anavyojivunia ufanisi wa kazi yake na mtindo wa maisha wa kifahari.
Kuna picha yake na manyota wa filamu , wanasiasa na nyingine akiwa na mwanamuziki na nyota wa kimataifa wa Nigeria Davido. Hakuna hata picha moja inayoashiria amefanya makosa ya aina yoyote.
Lakini baadhi ya watu wanasema kuna upande mwingine wa Bw.Kyari.
Mnamo mwezi Disemba mwaka uliyopita, mfanyabiashara Afeez Mojeed, alimtuhumu kwa utapeli. Alikuwa akitoa Ushahidi mbele ya jopo la mahakama mjini Lagos ambalo linalochunguza kitengo cha polisi cha Sars kilichotuhumiwa kwa mauaji ya kiholela.
Wakati huo Bw. Kyari alikuwa naibu kamanda wa Sars mjini Lagos. Afisa huyo wa polisi alituhumiwa kwa kumzuilia Bw Mojeed mwaka 2014 na kuchukua pesa kutoka kwake.
Wakili wa Bw. Kyari amekana kuwa alifanya makosa yoyote.
Mwaka 2019, Tume huru ya kitaifa ya kutetea haki za binadamu nchini Nigeria na shirika la kimataifa la kutetea haki la Amnesty International zilimtuhumu Kyari kwa kutumia mali iliyochukuliwa kwa washukiwa wa utekaji ambao wameuawa na kitengo kingine cha polisi kujinufaisha yeye binafsi.














