Jinsi wanawake wa Mexico wanavyotumiwa kingono na wafanyabiashara ya madawa ya kulevya Mexico

Mwnamke

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 5

Jimbo la magharibi mwa Mexico la Sinaloa ni makao ya magenge hatari na sugu ya wauzaji wa mihadarati nchini humo. Pesa inayopatikana kutokana na mihadarati imeacha chapa yake kwenye mahusiano baina ya wafanyabiashara wa mihadarati na wanawake vijana-na kuchochea kiu ya kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha muonekano wa maumbile.

Kwenye dawati lake la kliniki katika mji mkuu wa jimbo hilo uitwao Culiacan, Dokta Rafaela Martinez Terrazas huketi kila siku kupokea wateja wanawake wanaotaka kufanyiwa upasuaji unaohusiana na kile kinachofahamika kama "narco-aesthetic".

"Kiuno chembamba … nyonga pana na makalio makubwa … Na kama ni upasuaji wa matiti wote hutaka yawe makubwa," anasema Martinez.

Mwanamke mwenye umbile hili la 'namba nane' mara nyingi hufahamika kama 'buchona' nchini Mexico - hususani kama anajua kuvaa mavazi na vipuri vya kuvutia kuvutia na vya bei kali vilivyotengenezwa na nembo maarufu za mavazi na vipodozi, mwenye mpenzi ambaye ni mlanguzi wa mihadarati.

"Wastani wa miaka ya wagonjwa wangu ninaowahudumia ni kati ya miaka 30 na 40. Lakini mara kwa mara wanawake vijana zaidi huja-hata walio chini ya umri wa miaka 18," anasema daktari.

"Huwa wanashindana wao kwa wao-ni nani -mwenye umbile bora kuliko mwingine -au mwenye kiuono chembamba zaidi ."

Dokta Rafaela Martinez Terrazaz

Chanzo cha picha, Ulises Escamilla

Maelezo ya picha, Dokta Rafaela Martinez Terrazaz huwaeleza wanawake kuwa baada ya mahusiano ya kingono na marafiki zao wa kiume miili itabaki kuwa yao na sio ya marafiki zao tena

Wanawake na wasichana wadogo wanaweza kuja kwa ushauri wa kimatibabu na mama zao au marafiki zao. Wengine huja na mwanaume, au hata peke yao.

"Mara kwa mara huja na wapenzi wao wa kiume ambao huwalipia garama ya upasuaji. Na kuna wanaume mbali mbali ambao hunipigia simu na kuniambia , 'Habari, daktari- Nitakutumia msichana umfanyie upasuaji wa kubadili umbo lake .'

"Mwanaume mmoja alinipigia simu, akasema , 'Mmoja wa wasichana wangu anakuja kukuona. Sasa daktari, unajua kile ninachokipenda. Usimsikie anachokisema- Ni mimi ninayekulipa ,'" Martinez anasema.

"Nilimwambia aelewane na mpenzi wake kwanza, kwasababu wakati mgonjwa anpokuwa katika chumba cha upasuaji, ni yeye atakayefanya maamuzi."

'la buchona' ni nini?

Kim Kardashian

Chanzo cha picha, Getty Images

  • Asili ya neno bado haijafanamika, lakini linatumiwa kumuelezea mtu aliyefanyiwa upasuaji wa kubadili umbo na kuwa sawa na namba 8, mavazi ya kuvutia ya bei kali na vipuri vya bei kali
  • Walanguzi na watumiaji wa mihadarati hupendelea wapenzi wa kike wa -Narcos-lakini wanawake wengi wanaofanyiwa upasuaji wa kupata umbile hili hufanya hivyo kwasababu ndio mtindo wa kisasa unaowafanya wapendeze wavaapo mavazi ya kila aina, sio kwasababu unahusiana na wauza wa madawa ya kulevya.
  • Umbo la Kim Kardashian (pichani juu) wakati fulani limekuwa likiitwa buchona

Mwanaume huyu amewapeleka wanawake wapatao 30 kwa dokta Rafaela Martinez wakafanyiwe upasuaji. Kwa takriban dola 6,500 (£4,700) kwa ajili ya upasuaji wa nyonga na kiuno ,upasuaji huwa ni ghali. Mara kwa mara malipo huwa ni ya pesa taslimu.

"Bila shaka, katika upasuaji wa aina hii pesa hutoka kwa wauzaji na wasafirishaji wa madawa ya kulevya ," Martinez anasema. "Nilikuwa nafikiri awali kwamba, ' ninachofanya sio kizuri. Sio kwamba sasa nimebadili mawazo yangu, lakini sifikirii ten asana kabla ya kumfanyia mtu upasuaji . Hii ni kwasababu uchumi hapa katika jiji la Sinaloa - migahawa, baa, hospitali-vyote vinategemea wauzaji wa dawa za kulevya ."

Dokta Martinez huwa anajaribu kuwatia moyo na kuwapa ushauri wanawake ambao upasuaji wao umegharamiwa na wapenzi wao.

"Ninamuuliza mgonjwa kama yuko SAWA juu ya upasuaji ambao mpenzi wake anataka aufanye . Wakati mwingine wanasema , 'Niko sawa tu, vyovyote anavyotaka'.

''Na ninawaelezea kwamba baada ya muda, hatakuwa mpenzi wake wa kiume tena, lakinji miili yao itabakia kuwa yao kwa maisha yao yaliyobaki hapa duniani. Kwahiyo lazima wachague kile wanachotaka-sio nini mpenzi wake wa kiume anataka ."

Katika chumba chake cha matibabu, daktari huona ushahidi wa aina fulani ya kandarasi, mara nyingi huwa kati ya wanawake na wanaume. Haya ni mahusiano ya kibinafsi yanayoandaliwa katika mji wa Sinaloa -baadhi wanaweza kusema yanayotumiwa na -wauzaji wa madawa ya kulevya.

"Kwa wauzaji wa madawa ya kulevya al maarufu nchini Mexico - narco ni muhimu sana kuwa na mwanamke mrembo kando yake … Ni kama ni lazima kwa kila mfanyabiashara wa dawa za kulevya ," anasema Pedro (sio jina lake halisi), muuzaji sugu wa dawa za kulevya .

Pedro ni mwanaume wa miraba minne, kwa muonekano anaweza kukadiriwa kuwa na umri wa miaka 30 na ushee , ambaye hataki kutambulika. Anajieleza binafsi kama mkufunzi wa kibinafsi, na alijiunga na mitandao ya wauzaji wa mihadarati katika mji wa Sinaloa.

"Wanaume huwa wanashindana baina yao kwa ajili ya mwanamke. Mke wako ni mtu ambaye atakuwa nyumbani akiwatunza watoto. Mwanamke mwingine uliyenaye zaidi ni ni kama vikombe vya maonyesho."

Unaweza pia kusoma

Mke wa mfanyabiashara wa mihadarati

Emma Coronel Aispuro, mke wa mkuu wa mtandao wa wafanyabiashara ya mihadarati wa Sinaloa , Joaquín "El Chapo" Guzmán, alikiri mashitaka mwezi Juni mjni Washington DC kwa kushiriki uuzaji wa mihadarati na mashitaka mengine mbali mbali. Aliripotiwa kukutana na Guzmán akiwa msichana mwenye umri wa balehe katika mashindano ya urembo katika mji wa Durango, Mexico, mwaka 2007, na kukubali kuolewa naye siku ile ile.

Ruka Instagram ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa Instagram ujumbe

'Na kuna kitu fulani cha msingi zaidi wanachokitaka'

"Wanaume hutawaliwa na tamaa - kwa makalio makubwa na matiti. Ni tamaa zaidi ya chochote," anasema.

Pedro amewahi kulipia upasuaji wa kubadili maumbo ya wanawake wawili.

"Labda mtu unayemfahamu anakwambia , 'Mpenzi wangu anataka matiti yangu yatengenezwe, au makalio, au pua yake iundwe anavyotak.' Na kama mwanaume alivutiwa naye, basi anakuwa mdhamni wake (sponsor) au baba wa ubatizo," anasema.Mpango unakamilika.

"Kwahiyo mwanamke anaweza kusema , 'SAWA, mwili wangu ni wako kwa miezi sita kama utalipia garama ya upasuaji ,'" anasema Pedro.

Na kandarasi au mikataba isiyo rasmi inaweza kuwa sio ya upasuaji tu, anasema.

"Mara nyingi kama mwanamke sio binti wa mtu fulani mwenye uwezo, huwa wanatafuta mpenzi wa kiume ambaye anaweza kuwasaidia ,"anasema. "Kwahiyo makubaliano yanaweza kuwa kwa ajili ya vitu kama gari, pesa au bidhaa za anasa."

Fikra kwamba mwanamke ni 'mali inayomilikiwa na mwanaume'

Wakati wanawake wengi katika jimbo la Sinaloa hupitia kipindi cha kutaka kuwa wapenzi wa wauzaji wa madawa ya kulevya, Gabriela ambaye amekuwa mpenzi wao anasema, anataka sasa kuwa na mwanaume wa aina tofauti - "mtu ambaye ana akili, mfanyakazi, ambaye anaheshima ".

Lakini aina hizo za wanaume ni nadra sana kupatikana katika jimbo la Sinaloa.

"Ni kawaida sana kwa mwanaume kuwa na wanawake watatu au wanne rasmi pamoja na marafiki wengine wengi wa kike. Ni sehemu ya utamaduni ,"anasema Gabriela.

"Na kile ambacho nimekiona kwa muda mrefu, wanaume wamekuwa ni watu wasiokuwa na aibu. Wanawake hufungwa macho na tamaa ya udhamini ya usaidizi wa kifedha - macho ambayo hayaoni, moyo ambao hauna hisia ,"

Wakili Maria Teresa Guerra anasema anafahamu wanawake wanaotaka kuachana na wauza mihadarati lakini inakua ni vigumu sana

Chanzo cha picha, Ulises Escamilla

Maelezo ya picha, Wakili Maria Teresa Guerra anasema anafahamu wanawake wanaotaka kuachana na wauza mihadarati lakini inakua ni vigumu sana

Utamaduni wa wauza mihadarati umeendeleza fikra kwamba wanawake ni mali "inayomilikiwa " na wanaume, anasema Maria Teresa Guerra, wakili ambaye kuwatetea wanawake katika Sinaloa.

Na hii inaongeza hatari ya unyanyasaji na mauaji dhidi ya wanawake, anaamini iwe kwa ghasia kutoka kwa mpenzi muuzaji wa madawa ya kulevya au hata kutoka kwa maadui wa mpenzi wake.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya sauti, Upasuaji uliotumbukia nyongo huko Romania