Jinsi upasuaji wa kurekebisha maumbile ya mwili unavyoshamiri Uchina licha ya kuwa hatari

young woman rhinoplasty stock photo

Chanzo cha picha, Getty Images

Sawa na vijana wa rika yake Ruxin mwenye umri wa miaka 23 huangalia mitandao ya kijamii ya moja kwa moja kila siku, lakini anaangalia mkitu maalum- ''updates'' ama taarifa za hivi karibuni kabisa za upasuaji wa kubadilisha au kurekebisha maumbile ya mwili.

Ruxin anapanga kufanyiwa upasuaji utakaompa muonekano wa "kope mbili" ambapo upasuaji huo utamuongezea kope, akiwa na matumaini kwamba utayafanya macho yake kuonekana makubwa zaidi.

Mkaaji huyu wa Guangzhou mara kwa mara amekuwa akitumia app ya Gengmei kumsaka mpasuaji bora zaidi .

"Kuna kliniki nyingi sana hapa mjini, lakini ninataka kuhakisha ninakwenda kwenye kliniki bora zaidi. Ni uso wangu tunaouzungumzia hapa unajua ," aliiambia BBC.

Gengmei, neno linalomaanisha "mzuri zaidi" katika Lugha ya Kichina, ni moja ya majukwaa kadhaa ya mitandao ya kijamii nchini Uchina yaliyotengwa kwa ajili ya upasuaji wa kurekebisha na kubadili maumbile asili ya mwili, ambapo watumiaji wao huacha taarifa za upasuaji huo, ukiwemo upasuaji wa midomo na pua.

Matokeo ya utafutaji wa taarifa yanaweza kuchujwa kulingana na sehemu husika ya mwili, matibabu, na kliniki, miongoni mwa mengine.

China cosmetic surgery apps

Chanzo cha picha, Gengmei/So-young

Maelezo ya picha, App ya mtandao wa kijamii ya Gengmei (kushoto) na So-Young (kulia) zimewapata wimbi la watumiaji katika miaka ya karibuni

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2013, wametumiaji wa Gengmei wameongezeka kutoka watu milioni 1 hadi milioni 36. Zaidi ya nusu yao ni vijana wa kike wenye umri wa miaka ishirini na ushee. Sawa na Gengmei, ukumbi wa mtandao wa upasuaji wa So-Young umeshuhudia wimbi la watumiaji wake wa mara kwa mara likiendelea kuongezeka kutoka , milioni 1.4 mwaka 2018 hadi milioni 8.4 leo hii.

Umaarufu wa kurasa hizo unaelezea ni kwa kiwango gani mitazamo juu ya upasuaji wa kubadilisha au kurekebisha maumbile asilia ya mwili nchini Uchina, ambayo kwa sasa inafanya upasuaji zaidi kuliko nchi nyingine yoyote duniani baada ya Marekani.

Kulingana na ripoti ya Deloitte, soko la Uchina la bidhaa za kubadilisha sura na muonekano limeongezeka kwa karibu mara tatu kwa thamani katika kipindi cha miaka minne kutoka yuan bilioni 177 ($27.3bn; £19.7bn) katika mwaka 2019 - ukuaji wa mwaka wa 28.7%, juu ya viwango vya dunia vya ukuaji wa 8.2%.

Kama hii itaendelea, Uchina inaweza kuwa soko kubwa zaidi duniani la upasuaji wa kubadilisha maumbile asili ya mwili katikati ya karne, kulingana na gazeti la The Global Times.

Huku upasuaji maarufu ukiwa ni ule wa kutengeneza "kope mbili" na taya lenye muundo wa herufi V, upasuaji mpya unaibuka na kuvuma na kufifia, huku wa hivi karibuni zaidi ukiwa ni ule unaoufanya muonekano wa pua na wenye masikio yenye ncha , kulingana na ripoti.

Wajumbe wa Kizazi cha Z au Gen Z - wale waliozaliwa baada ya mwaka 1996 - hawaoni haya juu ya kufanyiwa upasuaji licha ya kwamba mada hiyo katika miaka ya nyuma ilikuwa ni mwiko.

Ruxin, anayefanya kazi katika duka la fasheni, anasema kwamba marafiki zake wa kike "huzungumzia wazi juu ya kufanyiwa upasuaji wa kubadilisha maumbile na muonekano wao ".

"Hatakama watu hawatangazi kibiashara kwamba wamefanyiwa marekebisho fulani ya muonekano wao, hawakani unapowauliza ."

Gao Liu's botched nose job

Chanzo cha picha, Weibo/Gao Liu

Maelezo ya picha, Watumiaji wa intaneti wa uchina walijibu juu ya hadithi ya kutisha juu ya upasuajiwa pua uliokwenda vibaya wa mchezaji filamu Gao Liu.

Alisema kuwa atahitaji kufanyiwa upasuaji zaidi kurekebisha pua lake, lakini madhara yake tayari yamekwisha mgarimu zaidi ya yuan zaidi ya 400,000 yuan katika mikataba ya filamu.

Wakati huo huo, kuhudhuria kwake kliniki kuliahirishwa kwa miezi sita, na hospitali ilitozwa faini ya yuan 49,000.

Watumiaji wengi wa mtandao wanasema adhabu haikuwa kali vya kutosha.

"Hii ni adhabu ya kumuadhibu mtu?" mmoja wa watumiaji wamtandao aliandika huku alitaka sekta ya upasuaji huo idhibitiwe.

Mwezi uliopita, tume ya afya nchini Uchina ilitangaza kampeni inayolenga watoaji wa huduma ya upasuaji wa kubadili viungo ambao hawana vibali nchini humo, pamoja na kufanya uchunguzi wa malalamiko ya wateja .

Kwanini wanahatarisha maisha yao?

Watu wengi nchini Uchina wanajali na kuupatia umuhimu mkubwa muonekano wao na kiu ya " warembo" huufanya upasuaji wa kubadili muonekana wa viungo vya mwili kuwa kitu kinachozungumziwa zaidi kwenye mitandao ya kijamii na cha kisasa , wataalamu waliiambia BBC.

Sheria za udhibiti zinahitajika

Hatahivyo kushamiri kwa upasuaji wa kubadilisha maumbile ya mwili unakuja na athari zake.

Kwa mujibu wa ripoti ya Global Times, Uchina ilikuwa na zaidi ya kliniki zaidi ya 60,000 zisizokuwa na vibali za kurekebisha maumbile katika mwaka 2019.

Kliniki hizo zilihusika na ''matukio ya kimatibabu'' zaidi ya 40,000 kila mwaka, wastani wa operesheni za kubadilisha muonekano wa mwili 110 hufanyika kila siku, ripoti iliongeza.

Katika visa vya watu mashuhuri zaidi, mchezaji filamu Gao Liu alishirikisha umma picha online za upasuaji aliofanyiwa uliomsababishia kovu katika sehemu ya mbele ya pua, ikimaanisha kuwa nyama ya pua imekukufa.

A livestreamer sells biscuits via live streaming in Tianjin, China

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, PICHA: Matangazo ya moja kwa moja ya mtandao nchini Uchina yamekuwa biashara kubwa-na wengi wanataka kuonekana vizuri mbele ya kamera kwa ajili yake.

Dkt Brenda Alegre,profesa wa masomo ya usawa wa jinsia katika Chuo kikuu cha Hong Kong, alisema kwamba "kufanana na muonekano huo kunaufanya uwe wa kupendwa zaidi , sio tu kwa mapenzi, bali hata kwa ajira".

Nchini Uchina, waombaji wa kazi mara nyingi hutakiwa kuwasilisha picha zao kwa waajiri watarajiwa . Baadhi ya matangazo ya kazi huelezea muonekano wa kipekee ,hususan kwa wanawake, hata kama hawahitajiki kufanya kazi .

Ripoti ya Shirika la Kimataifa la haki za binadamu - Human Rights Watch ya mwaka 2018 ilielezea kuhusu matangazo ya kazi za watu wenye muonekano wa kijinsia ikitoa mifano ikiwa ni pamoja na mtu lazima aonekane "wakupendeza" katika mauzo ya nguo , na lingine lililomtafuta mtoa mafunzo ya "mrembo na anayejua fasheni" .

Na wakati mitandao ukiwa ndio maeneo ya fursa zote za kazi - na yote inazingatia muonekano wa mtu-wataalamu wanasema kuna juhudi mpya za watu kufanyia kazi muonekano , zaidi ya nyakati zilizopita.

"Kwa kiwango fulani urembo unaweza kuwapatia watu fursa za kazi-kwa mfano kuna malipo ya fedha katika utangazaji wa moja kwa moja wa video na ubunifu wa maudhui mtandaponi ," makanu rais wa App ya Gengmei Wang Jun aliiambia BBC.

Gengmei anasema App yake inafanya kazi na wenye vibali pekee kwenye jukwa lake.

'Mzuri zaidi hadi mbaya zaidi'

Utamaduni wa magazeti makubwa ya uchina huwa pia yanakuwa na ukatili wakati mwingine. Mara kwa mara machapisho ya habari huwakosoa watu maarufu kwa muonekano wao wa maumbile yao asilia.

Mapema mwaka huu, kituo cha usanii wa picha cha Shanghai kilinadi maonyesho ambayo yaliorodhesha picha za wanawake kuanzia ''warembo zaidi hadi wabaya zaidi''

Lu Yufan, mpiga picha mwenye makao yake Beijing ambaye anaandika kitabu kuhusu upasuaji wa kubadilisha muonekano , aliiambia BBC kwamba alipokuwa anakua, watu mara kwa mara walikuwa wakweli juu ya muonekano wake.

Wazazi wake walimwambia kuwa anafanana na msanii wa TV - "si kwa upande wa urembo bali kwa ucheshi wake ", tanakumbuka mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29.

"Wakati nilipokuwa shule ya sekondari, wavulana waliorodhesha majina ya wasichana waliokuwa wabaya zaidi na wazuri zaidi kwa sura darasani kwetu . Waliniambia mimi nashikilia namba 5."

Beijing photographer Lu Yufan

Chanzo cha picha, Lu Yufan

Maelezo ya picha, PICHA: Mpigapicha wa Beijing Lu Yufan alitembelea kliniki kuandika kitabu chake lakini hakufanyiwa upasuaji

Bi Lu, ambaye alitembelea kliniki 30 za upasuaji wa kubadili muonekano kama sehemu ya mradi wake wa kuandika kitabu, aliongeza kuwa madaktari hawakusita kumwambia ni jinsi gani uso wake unaweza "kuboreshwa".

"Walikuwa washawishi kiasi kwamba nilishindwa kusema hapana, isipokuwa sikuwa na pesa za kufanyiwa upasuaji ," alisema.

Kwa Ruxin, utengenezaji wa kope ni nafuu, unagarimu dola 300 na 1,200.

Lakini ni hatua ya kwanza tu.

"Kama hii itakwenda vyema, huenda nikafanya zaidi. Ni nani asiyetaka kuwa mrembo zaidi ?"