Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
CHAMP: Fahamu silaha ya Marekani kujilinda dhidi ya makombora ya nyuklia kutoka Korea kaskazini
Wakati vita vya maneno kati ya Marekani na Korea kaskazani viliposheheni chini ya utawala wa rais Donald Trump , Marekani ilikuwa imeanza kuhisi joto la rais Kim Jong Un wa taifa hilo na kuanza kujiandaa kwa lolote lile .
Kando kando ya mji wa Albuquerque, katika jimbo la New Mexico , kundi moja la wataalam kutoka jeshi la angani la Marekani lilikuwa linatengeneza silaha ilio na malengo kadhaa : Kuzuia shambulio la kinyukllia la Korea kaskazini..
Silaha hio sio ya kawaida, ni silaha inayotumia mawimbi ya kielektroniki ambayo hayawezi kuwaathiri binadamu na inatumia teknolojia kama ile iliotumika kutengeneza tanuri ya Microwave.
Na kulingana na wataalamu kadhaa kuhusu masuala ya kijeshi waliozungumza na BBC Mundo , lengo lake kuu ni kuyafanya makomboya ya kinyuklia ya Korea kaskazini kushindwa kufanya kazi bila kufanya uharibifu.
Silaha hiyo imepatiwa jina la Microwave Interference Electronically High Power (CHAMP) na kwa msingi lengo lake ni kutoa mawimbi kutoka anga za juu yanayoweza kukaanga mifumo ya kielektroniki.
" Kwa kuzingatia hali ya teknolojia katika ulimwengu wa kisasa, ambapo karibu kila kitu hufanya kazi kwa njia ya kidijitali, aina hii ya kombora hutoa mawimbi makali ya kielektroniki yenye uwezo wa kukatiza au kufanya vifaa vya kielektroniki visifanye kazi, "kulingana na msemaji wa Kambi ya wanajeshi wa angani ya Kirtland huko Albuquerque..
Kambi hiyo ambayo ilikuwa mojawapo ya maeneo ya kutoa usaidizi kwa mradi wa kujenga bomu la atomiki wakati wa vita ya pili ya dunia , sasa inafanya utafiti kuhusu silaha hii mpya itakayotumia mawimbi ya kielektroniki.
" Silaha hiyo ya CHAMP ambayo ni kombora la masafa marefu lakini bila betri ya kulichaji, linaweza kurushwa kutoka ndege ya kivita aina ya B-52 , na linaweza kuruka umbali wa 1 . 127 kilometers , " kulingana na Fisher.
Lakini uzuri wake kama silaha ni zaidi ya shambulio la kiatomiki kutoka Korea kaskazini.
Silaha zinazotumia mawimbi ya kielektroniki
Hii sio mara ya kwanza kwa Marekani kutengeneza kombora kwa kutumia mawimbi ya kielektroniki.
Sharon Weinberger, muhariri mkuu wa sera ya kigeni alielezea BBC Mundo kwamba jeshi la angani limechunguza na kutumia mawimbi ya kielektroniki kama silaha miongo miwili iliopita
Kulingana na mtaalamu huyo , kifaa cha kijeshi kinachotumia mawimbi ya kielektroniki kilitumika nchini Afghanistan na Iraq kwa lengo la kulemaza mabomu na ndege zisizikuwa na rubani.
Lakini uzoefu wa jeshi la Marekani wa kutumia mabomu yanayotumia mawimbi ya kielektroniki ulianza miongo kadhaa iliopita.
Kitengo cha Pentagon , kinachofanya tafiti endelevu za kijeshi , kiliagizwa mwaka wa 1960 kuchambua madhara ya mawimbi ya kielektroniki kwa wanadamu.
"Yote hayo yalianza baada ya serikiali ya Muungano wa Usovieti kushambulia ubalozi wa Marekani mjini Moscow kwa kutumia bomu la aina hiyo'', anaelezea Weinberger , mwanzilishi wa 'Imaginaries of war', dharura ya Pentagon iliobadili ulimwengu. ".
Matukio hayo yaliofanyika ndio yaliosababisha utafiti wa mawimbi hayo uliofanywa na jeshi la angani ambalo liliwatumia tumbili ili kuweza kubani athari ya bomu hilo kwa bindamu.
Lakini licha ya utafiti huo dhidi ya binadamu kufeli, utengenezaji wa silaha kwa kutumia teknolojia hiyo umechukua mkondo mpya katika miaka ya hivi karibuni.
Tumbili hao walitumiwa kupima athari ya mionzi hiyo ya kielektroniki .
Ijapokuwa makombora ya mawimbi ya kielektroniki yaliorushwa kutoka kwa ndege hayajatumiwa katika vita vya ardhini, vipimo vilivyofanywa vimeifanya idara ya ulinzi ya Marekani kuhisi kana kwamba kuna mafanikio na matokeo hayo.
Vipimo
Ijapokuwa wataalamu wanahakikisha kwamba vipimo kadhaa vimefanyika ili kuthibitisha uwezo wake , kufikia sasa idara ya ulinzi ina maelezo kuhusu moja.
Jaribio la kwanza Iilifanyika katika jangwa la Utah 2012, miaka mitatu tu baada ya uchunguzi wa kwanza kuhusu aina hiyo ya silaha kuanza rasmi katika maabara ya jeshi la wanaanga katika kambi ya Kirtland.
Kulingana na Fisher , mwezi Oktoba mwaka huo, ndege aina ya B-52 ilifyatua kombora linalotumia mawimbi ya kielektroniki katika jangwa eneo lenye ukubwa wa kilomita 4,000.
Lakini je silaha hii ingetumika vipi kulemaza makombora ya nyuklia ya Korea Kaskazini?
Mawimbi ya kielektroniki dhidi ya silaha za kinyuklia
Msemaji wa kambi ya kijeshi ya Kirtland anasema kwamba utengenezaji wa silaha kama hiyo haukulenga kuwa kinga ya moja kwa moja dhidi ya makombora ya kinyuklia ya Korea Kaskazini.
Hatahivyo, utumizi wake kwa lengo hilo ulijadiliwa katika ikulu ya Whitehouse , walisema maafisa wawili walioripoti kwa runinga ya Marekani ya NBC.
Na kulingana na Bleek, mojawapo ya madhara ya mawimbi ya kielektroniki ambayo haikujadiliwa ni uwezo wa kuzuia makombora ya nyuklia kulipuka kwa kupitia kuyalemaza. Silaha hizo zinaweza kutumika kuyalemaza makombora ya kinyuklia na hivyobasi kushindwa kulipuka.
"Mawimbi hayo ya kielektroniki pia yanaweza kukaanga nyaya za kielektroniki na kulinda eneo kubwa dhidi ya mlipuko'' , anasema mtafiti wa kituo cha kimkakati wa kimataifa kilicho Washington.
"Iwapo Marekani itarusha kombora kuelekea katika himaya ya taifa la Korea kaskazini itaonekana kama uchokozi , bila kujali iwapo ni kombora la aina gani..
Bleek anasema kwamba hatua hiyo huenda ikasababisha madhara makubwa zaidi kwasababu taifa la Korea Kaskazini halitasubiri kubaini lengo la kombora hilo na badala yake kutumia fursa hiyo kulipiza kisasi kwa kurusha makombora zaidi.
Vilevile haijulikani , hadharani kombora hilo la kielektroniki litakuwa na madhara gani iwapo litalemaza kombora la masafa marefu la Korea kaskazini.
''Silaha za mawimbi ya kielektroniki zinaweza kuchukua jukumu kubwa katika katika operesheni ya kijeshi dhidi ya Pyongyang , iwapo hilo litafanyika , lakini pia sio suluhu ya vitisho vya silaha za kinyuklia zinazomilikiwa na Korea kaskazini " anahitimisha Bleek .