Jacob Zuma: Rais wa zamani wa Afrika Kusini ambaye uongozi wake ulikumbwa na utata mwingi

Chanzo cha picha, AFP
Jacob Zuma ndiye rais maarufu na mwenye utata mwingi Afrika Kusini kuwahi kuwa naye tangu enzi za uongozi wa Wazungu kumalizika 1994.
Amekuwa mwanasiasa mwenye roho tisa, akinusurika msururu wa kashfa ambazo zingeangamiza uongozi wa mtu yeyote yule.
Lakini bwana Zuma, mtu aliyezaliwa katika familia ya umasikini mkubwa ambaye alienda mafichoni ili kupigana dhidi ya ubaguzi wa rangi kabla ya kupanda na kuwa rais wa watu, hasingeweza kukwepa kashfa hizo kwa muda mrefu.
Alikuwa akikabiliwa na kura ya tisa ya kutokuwa na imani naye bungeni kabla ya kuondoka afisini , akiwa amelazimishwa kuondoka na chama chake mwenyewe cha ANC .
Na mashtaka hayo ya ufisadi yaliokataliwa hatimaye yaliweza kumnasa. Mwezi Aprili 2018, alishtakiwa kwa madai ya ulaghai na njama zinazohusiana na kashfa ya silaha 1999.
Kwa miaka mingi , ilikuwa sio rahisi kumpuuza bwana Zuma : Jina lake la Kizulu Gedleyihlekisa, lina maana ya mtu anayetabasamu huku akiwasaga wapinzani wake.

Chanzo cha picha, Reuters
Hakuwacha madaraka bila vita, lakini hatma yake ilikuwa imefika na akaamua kujadiliana jinsi atakavyoondoka madarakani.

Chanzo cha picha, AFP
Alipowania urais , alikuwa amepuuzwa kabla ya kuanza kufanya hivyo. Tukielekea katika uchaguzi wa 2009, alikuwa akikabiliana na madai ya ubakaji na ufisadi.
Aliondolewa mashtaka ya kumbaka rafiki wa familia aliyekuwa na virusi vya HIV 2006 - hatahivyo tamko lake katika mahakama kwamba alikuwa ameoga ili kuzuia kuambukizwa virusi vya HIV limeendelea kumwinda katika kipindi chake chote cha urais.
Kesi ya ufisadi ilikuwa mwiba , hata baada ya kutupiliwa mbali kwa njia ya utata wiki chache tu kabla ya uchaguzi ambao alichaguliwa tena kuongoza taifa hilo.
Mwaka 2017, mahakama ya juu iliamuru kwamba mashtaka 18 ya ufisadi lazima yarejeshwe dhidi ya Zuma.
'Rais wa raia'
Iikuwa haiba yake iliomsaidia bwana Zuma kuchukua madaraka 2009.
Wafuasi wake waliona umaarufu kama kitu kipya ikilinganishwa na mtangulizi wake Thabo Mbeki ambaye alionekana kuwa rais aliyejitenga sana na watu
''Ni mtu anayekusikiliza, hachukui maamuzi ya Mfalme msomi'', alisema mfuasi wake mmoja ambaye hakutaka jina lake kutajwa akimlinganisha na bwana Mbeki , ambaye wandani wake walishutumiwa kwa kuongoza mashtaka dhidi ya bwana Zuma baada ya kuchukua uongozi wa ANC 2007.
Malezi ya bwana Zuma na ukuzaji wake wa tamaduni umetajwa kuwa sababu kuu iliosababisha yeye kuwa maarufu miongoni mwa watu maskini nchini Afrika kusini hususan katika maeneo ya mashambani.

Chanzo cha picha, AFP
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 75 ni mtu anayejivunia ndoa ya wake wengi - akifuata tamaduni za Kizulu na kufikia sasa ana wake wanne.
Amefunga ndoa mara sita kwa jumla na ana watoto 21. Mmoja ya wake zake raia wa Msumbiji kate Matnsho alijitoa hai mwaka 2000.
Hatahivyo anajulikana kwa uzinzi wake na alizaa mtoto na mwanamke mwengine.
Haikuchukua muda mrefu raia walianza kuhoji kuhusu picha yake ya kujiita 'rais wa raia.'' Kufikia 2013 , alijipata mashakani kufuatia ujenzi wa nyumba yake mashambani katika eneo la Nkandla, kaskazini mwa jimbo la KwaZulu Natal kwa kutumia fedha za umma.
Kufikia kumbukumbu ya maombolezi ya rais wa kwanza wa taifa hilo Nelson Mandela, mwezi Disemba mwaka huohuo, wafuasi wa ANC walikuwa wakimzomea hadharani mbele ya mabalozi wa kigeni - ikiwemo rais wa Marekani Barrack Obama.
''Anakula wakati sisi tunahisi njaa'', raia mwengine alisema , akizungumzia kuhusu ujenzi wa nyumba yake ya Nkandla iliokamilika ikiwa na zizi la ngombe, ukumbi wa filamu, kidimbwi cha kuogelea , kituo cha wageni na nyumba ya kuku.
Miaka mitatu baadaye , mahakama ya juu nchini Afrika Kusini iliamuru , alikiuka katiba kwa kushindwa kulipa serikali fedha zilizotumika kukarabati nyumba yake ya Nkandla.
Rais aliomba msamaha kwa raia wa Afrika Kusini kutokana na kuchanganyikiwa kwake kulikosababishwa na kashfa hiyo na amelipa fedha hizo.
Lakini utata wa Nkandla ulipitwa na kashfa kubwa zaidi
Matatizo ya kisheria yaliomkabili Zuma:

Chanzo cha picha, Getty Images
- 2005: Alishtakiwa kwa kumbaka rafiki wa familia yake kabla ya kuondolewa mashtaka 2006
- 2005: Pia alishtakiwa na ufisadi uliohusisha mamilioni ya fedha za ununuzi wa silaha 1999, lakini mashtaka hayo yakaondolewa muda mchache kabla ya kuwa rais 2009.
- 2016: Mahakama iliagiza kwamba ashtakiwe na mashataka 18 ya ufisadi kuhusu kashfa hiyo - alikata rufaa lakini mwaka 2017 alishindwa kubatilisha uamuzi.
- 2016: Mahakama iliamuru kwamba alikwenda kinyume na kiapo alichokula kwa kutumia fedha za serikali kurekebisha nyumba yake ya kibinafsi huko Nkandla - alilipa fedha alizotumia.
- 2017: Mlinzi wa umma alisema kwamba anapaswa kuteuwa jopo ili kuchunguza madai alijipatia faida kutokana na ushirikiano na familia ya kitajiri ya Gupta - alikana madai hayo kama Gupta walivyofanya.
- 2018: Zuma aliidhinisha madai ya kuibia serikali.
- 2018: Mamlaka ya kitaifa ya kuwashtaki washukiwa alithibitisha bwana Zuma atakabiliwa na mashtaka 12 ya ulaghai.
Baadaye macho yote yakaelekezwa katika uhusiano wa bwana Zuma na familia ya kitajiri huku kukiwa na madai kwamba aliitumia kushawishi uteuzi wa baraza la mawaziri ili kupata kandarasi za serikali.
Wote Zuma na familia ya Gupta wamekana madai hayo , lakini chama cha ANC kikaagiza uchunguzi kuhusu kile katibu wake mkuu Gwede Mantashe alitaja kuwa udhibiti wa serikali unaofanywa na watu binafsi.
Mwezi Januari 2018, bwana Zuma aliidhinisha jopo la uchunguzi kuhusu madai hayo.
media captionAndrew Harding reports on allegations of high-level corruption in South Africa involving a British PR company
Maisha ya uchochole
Tukio kubwa la baadhi ya kashfa zake ni eneo alikozaliwa. Bwana Zuma alizaliwa katika eneo la Nkandla tarehe 12 Aprili 1942. Akilelewa na mamake mjane , na hakupata elimu rasmi.
Baadaye, akiwa na umri wa miaka 17, alijiunga na ANC , na kuwa mwanachama mtendaji katika wingi yake ya vijana, Umkhonto We Sizwe, mwaka 1962.
Wake wa Zuma :

Chanzo cha picha, AFP
Gertrude Sizakele Khumalo (aliolewa 1973)
Nompumelelo Ntuli (2008)
Thobeka Madiba (2010)
Gloria Bongi Ngema (2012)
Wake wa zamani :
Nkosazana Dlamini-Zuma (aliolewa 1972; na kutalakiana 1998)
Kate Mantsho (Aliolewa 1976; akafariki 2000)
line
Alishtakiwa kwa kupanga njama ya kuipindua serikali ya ubaguzi wa rangi na kufungwa jela kwa miaka 10 katika kisiwa cha Robben Island pamoja na Nelson Mandela.
Bwana Zuma anasemekana kuwapatia motisha mashujaa wa zamani wa chama cha ANC kwa kuimba nyimbo na ucheshi wake ndio sababu iliomfanya kuwa karibu na raia wa kawaida kabla ya kupanda na kuwa rais.
Baada ya kuachiliwa kutoka jela , bwana Zuma aliondoka Afrika Kusini , akiishi kwanza Msumbiji , na kuelekea Zambia kabla ya kupanda hadhi katika chama cha ANC hadi kufika katika kamati kuu ya chama hicho.
Alikuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza kurudi nyumbani 1990 wakati marufuku iliowekewa ANC ilipoondolewa ili kuingia katika majadiliano na serikali ya weupe walio wachache .
Huku akijaribu kumuondoa rais Mbeki madarakani , alipata uungwaji mkono miongoni mwa vyama vya wafanyakazi na chama cha kikomyunisti ambacho kinashirikiana na ANC - wakiamini kwamba angesambaza utajiri wa Afrika Kusini kwa watu masikini lakini chini ya bwana Zuma, uchumi ulisalia kuwa katika hali mbaya huku kiwango cha ukosefu wa ajira kikiongezeka kwa asilimia 28 , na maandamano ya kila siku yakifanywa na watu waliotaka huduma bora za msingi kama vile nyumba, elimu , maji na umeme.
Baada ya kuwa madarakani kwa miaka michache , baadhi ya washirika wake , kama vile kiongozi wa vijana Julius Malema , walimtoroka , wakimshutumu mtu huyo kwa jina 'JZ kwa kushindwa kuwasaidia watu maskini.

Chanzo cha picha, AFP
Pia kuna faida zilizoletwa na uongozi wa Zuma
Akiwa rais alifanikiwa kuwavutia wakosoaji wake wengi na wanaharakati wakati alipotangaza mabadiliko ya sera ya misaada mwezi Disemba 2010 - hatua hiyo imesaidia kusambaza dawa za kuzuia virusi vya HIV..
Afrika Kusini inakadiria watu milioni tano wanaoishi na HIV zaidi ya taifa lolote lile.
Shutuma
Mwandani wake wa zamani bwana Malema, pamoja na wanachama wenzake wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) walikuwa chini ya majaribio ya kumpindua .
Na baada ya mkewe wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma - kushindwa kumrithi kama kiongozi wa ANC , na hivyobasi kupoteza kwa Cyril Ramaphosa mwezi Disemba 2017 walihisi kumuondoa.
Miswada tisa ya kutokuwa na Imani naye iliwasilishwa siku kadhaa kabla ya Rais Zuma kutaka kutoa hotuba kwa taifa mwezi Februari 2018.
Wakati huohuo, bwana Ramaphosa - aliye maarufu kufuata nyayo za Zuma - na maafisa wakuu wa chama walikuwa wakikutana wakiandaa kumuondoa madarakani bwana Zuma na kuondoa madai ya ufisadi ambayo yalikuwa yakikikabili chama hicho kabla ya uchaguzi wa 2019.
Mwishowe , kile ambacho raia wengi wa Afrika Kusini walikuwa wakitaka kwa miaka mingi hatimaye kilifanyika - alijiondoa kama rais.












