Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Tigray: Sherehe zashuhudiwa Mekelle huku maafisa wa Ethiopia wakitoroka
Vikosi vya waasi katika Jimbo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray vimeuchukua mji mkuu wake, Mekelle, na kuzua sherehe za barabarani na kuwalazimisha maafisa kukimbia.
Wakazi shangwe na vigelegele, huku maelfu wakipeperusha bendera za kusherehekea ushindi
Serikali, ambayo iliuchukua mji wa Mekelle mnamo Novemba baada ya waasi kukataa mageuzi ya kisiasa na kuteka vituo vya jeshi, sasa imeitisha "kusitishwa mapigano kwa sababu za kibinadamu" katika eneo hilo.
Mapigano yamesababisha vifo vya maelfu kuwaweka wengine 350,000 katika hatari ya njaa
Zaidi ya watu milioni mbili wamehama makazi yao.
Kulikuwa na ripoti za hivi karibuni za mapigano mapya kati ya wapiganaji wa Tigray People's Liberation Front (TPLF) na vikosi vya serikali nje ya Mekelle.
Lakini mashambulizi ya haraka ya waasi siku ya Jumatatu yalisababisha kukamatwa tena kwa mji huo na waasi katika hali ambayo inaweza kuwa hatua kubwa katika mzozo huo mkali.
Taarifa iliyotolewa na kile kinachojiita Serikali ya Jimbo la Kitaifa la Tigray ilisifu "ushindi mzuri", ikisema Mekelle "sasa ilikuwa chini ya udhibiti kamili wa Vikosi vya Ulinzi vya Tigray".
Inatoa wito kwa watu na vikosi vya waasi "kukaa macho, bila kuchoka na kuwa macho kila wakati hadi Tigray atakapokuwa huru kabisa na vikosi vyote vinavyovamia".
Msemaji wa waasi Getachew Reda alisema hakuna hamu ya kusuluhisha mzozo huo akiambia CNN: "Malengo yetu yanadhalilisha uwezo wa mapigano wa adui ... Hatutaacha hadi Tigray iwafurushe wanajeshi wote maadui . Tutafanya kila linalowezekana "
Zaidi ya watu milioni tano wana uhitaji wa haraka wa msaada wa chakula, Umoja wa Mataifa umesema watu 350,000 wanakabiliwa na njaa.
Jumatatu, taarifa zimeanza kueleza kuwa wapiganaji wa Tigray - ambao walifanya mashambulizi makubwa wiki iliyopita walilazimisha utawala wa mpito kutoka Mekelle.
Getachew Reda, msemaji wa chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF), ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa mji upo chini ya mamlaka yao.
Baadhi ya watu wa Mekelle wameiambia BBC kuwa wanasheherekea kuondoka kwa wanajeshi wa serikali kuu.
Mtu ambaye hakutaka kufahamika kutoka serikali ya mpito ameiambia AFP kuwa"kila mtu ameondoka ", wakati mashahidi wawili wameiambia Reuters kuwa wanajeshi wa Tigray walikuwa wanaonekana Mekelle.
Serikali ya Ethiopia haijasema lolote kuhusu taarifa hizo za kuondoa majeshi yake.
Lakini imetuma taarifa Jumatatu kufafanua suala la kusitisha mapigano mpaka msimu wa kilimo uishe na vilevile kuruhusu wale wenye uhitaji wa kuweza kufikiwa na vilevile kutoa muda ili wanasiasa wapate suluhu ya mgogoro huo.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres, ambaye alizungumza na bwana Abiy siku ya Jumatatu , alisema wananchi wanalindwa , misaada ya kibinadamu , misaada ya kibinadamu inawafikia wananchi wanaohitaji na suluhu la kisiasa limepatika". Hatahivyo anategemea kuwa mapigano yataweza kusitishwa.
Kusheherekea na bendera
Katika siku ambayo mambo yalikuwa yanaenda haraka, wawakilishi wa serikali waliripotiwa waliripotiwa kuwa walikuwa wanapepea bendera kutoka Mekelle - na sio lazima Amani.
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto Unicef imetoa taarifa kulaani kitendo cha askari wa taifa la Ethiopia, ambao wanasema waliingia katika ofisi yao na kuharibu vifaa vyao vya satelaiti.
Chanzo cha habari huko Mekelle kimeiambia BBC kuwa watu wanasheherekea katika mitaa na kwenye mitandao ya kijamii kuonesha wafuasi wa waasi wa Tigray walitembea kwa gwaride huku wamebeba bendera.
TPLF imewataka wananchi kuwa watulivi na kushirikiana na majeshi yake.
Kwanini kulikuwa na mapigano Tigray?
Mwezi Novemba mwaka jana serikali ya Ethiopia ilitangaza kufanya mashambulizi kwa waasi wa waliokuwa chama tawala , the Tigray People's Liberation Front (TPLF).
Chama hicho kilikuwa na wafuasi wengi kilitofautiana na waziri mkuu Abiy Ahmed juu ya mabadiliko ya kisiasa katika taifa ambalo linategemea mfumo wa shirikisho m - ingawa pia TPLF ilivamia ngome ya jeshi Tigray.
Bwana Abiy, ambaye ni mshindi wa tuzo za Amani za Nobel alitangaza kuwa mgogoro umeisha mwishoni mwa Novemba lakini mapigano yalikuwa yanaendelea.
Maelfu ya watu waliuawa. Makumi maelfu walikimbia makazi yao na kuwa wakimbizi nchi jirani ya Sudan.
Pande zote mbili zinashutumiwa kukiuka haki za binadamu.
TPLF iliungana na kikundi kingine cha wapiganaji Tigray na kutengeneza jeshi la ulinzi Tigray.
Hofu ya njaa
Juni 10 , UN ilielezea hali ya njaa ilivyo kaskazini mwa Ethiopia.
Utafiti wa UN-ulisema watu 350,000 walikuwa katika janga kutokana na vitailiyotokea Tigray.
Kwa mujibu wa utafiti huo, chakula hakuna na ufikaji wa chakula katika eneo hilo umekuwa mgumu, hivyo hali ni mbaya watu wanakufa na njaa katika eneo kubwa.
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia chakula (WFP),na la watoto Unicef lilitaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kukabilana na janga hilo.
Lakini serikali ya Ethiopia ilikanusha madai hayo ya njaa katika taifa lake.